kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 18,154
- 17,491
- Thread starter
- #41
Huwezi kuondoa makosa kwa kutenda makosa. Katiba hii sio ya Samia na wenzake, ni katiba yetu sote. Hivyo, ili iwe haifai lazima sisi wote tuione haifai, na sio kwa kutumia matakwa ya Lissu au chadema. Kumlazimisha Samia lazima abadilishe katiba leo bila Samia kutuhoji sisi kujua tunasema nini juu ya hilo sio sawa. Na kama Samia atabadilisha katiba tuliyomkabidhi atulindie bila kutuhoji sisi tutoe ridhaa au tukatae nasisi tutamuadhibu kwa kosa hilo kwakuwa kwetu sisi present is well known and secure. Kuna watu tunaohisi kuwa amani tuliyonayo sisi inatokana na namna katiba yetu ilivyo, hivyo kuibadilisha kifungu chochote kunatusababishia tuwe na fear of unknown and known origin. Hatujui kama mabadiliko yatatusababishia nini; mazuri au mabaya. Hivyo, mjadala mpana kwa wadau wote unahitajika, sio mihemko ya mtu mmoja.Sasa tunaona kuwa ina mapungufu, na tunataka tuirekebishe ili ikidhi matakwa ya nyakati na majira haya. Kuna makosa gani kuweka madai haya...?
Sisi sio Lissu na Lissu sio sisi, lazima tushirikishwe kwenye kufanya chochote kwenye katiba hii; ama sisi moja kwa moja au kupitia wawakilishi wetu wa kikatiba.
Mpaka sasa hatuna takwimu za wangapi wanataka mabadiliko na wangapi wanataka ibaki hivihivi, kwahiyo tunahitaji muda wa hilo.