Paul Makonda sijui ana matatizo gani mtu huyu!!?
Endapo kama angekuwa na akili nzuri kichwani mwake, basi angechagua kukaa kimya, wala asingependa kuanzisha malumbano na Watu hata na wale wanaomchokoza makusudi.
Je, ameshawahi kujiuliza ni kwa nini basi wale Watu ambao Dkt. Wilbrod Slaa aliwataja kwenye ile skendo ya orodha ya mafisadi ambayo ilijulikana Sana kwa jina la 'The List of Shame' mpaka leo wale watu waliotajwa hawajawahi kujitokeza hadharani kujibu mapigo au kwenda Mahakamani ili kumshitaki Dkt. Slaa? Anajua sababu za hao Watu kuendelea kukaa kimya????
Mimi namshauri aache kufanya hivyo, huko Mahakamani anaenda kujidhalilisha zaidi, wenzake watajipanga na kisha wataenda huko Mahakamani ili kumvua nguo zote kabisa na kumuacha 'uchi wa mnyama.'
Aidha, anapaswa akumbuke Doctrine of Equity ambayo ina-state kwamba "He who goes for equity must go with clean hands."