Wanasheria Waelimisheni Viongozi Wetu Kitu Kinachoitwa "Vicarious Liability", Hata Kama Wewe Hujaua, Kama Muuaji ni Mtu Wako, Then Unawajibika Wewe

Nitarejea
 
Wakati "PII" ama "PASCO" mi namwita "MWANANZALA" anadadavua kuhusu VICARIOUS LIABILITY ni wakati muafaka na sahihi achimbe kidogo kuhusu "FALSE FLAG"

FALSE FLAG
FALSE FLAG
FALSE FLAG

Nikumbuke visa vichache nilipokuwa mdogo..... ambavyo visa vyote muhusika mkuu ni mdogo wangu....!

1. KISA CHA KWANZA
Bwana mdogo siku ya sherehe alikunywa soda tatu...... (miaka ya kati ya 80) DOUBLE COLA, MIRINDA na AKARUDIA DOUBLE COLA....! tukiwa tumelala usiku akakojoa, akanisogeza pale alipokojoa ..... alipohamia akakojoa tena..... akahamia miguuni, nako akakojoa tena......! akabadilisha shuka la kujifunika..... lake lenye mikojo akanifunika akachukua lililo safi langu.....
Hakika asubuhi NILIKIONA CHA MTEMA KUNI.....! Wakati huo mimi nilikuwa nimeshaacha kukojoa kitandani.....! niliumia sana , sikuwa na namna nyepesi ya kujitetea bali kuadhibiwa na kuimbiwa "KINDUMBWENDUMBWE"
NILIUMIA SANA.......

2. KISA CHA PILI
Kama kawaida nyakati hizo kulikuwa na kabati la vyombo ambapo kunakuwa na VYOMBO VYA WAGENI......
Bwana mdogo siku hiyo akaona anywe maji kwa kutumia glasi ya wageni...... akasogeza stuli kwenye kabati, akachukua glasi .... akanywa maji .... wakati anairejesha glasi lkabatini ikamponyoka na kuvunjika......
jioni wakati mama anarudi kutoka kazini .... dogo alikuwa wa kwanza kumpokea mama na kusema KAKA AMEVUNJA GLASS YA WAGENI....... "UUUUWIIIIIIIIIIII" sitaki kukumbuka kichapo nilichopokea....!

MATOKEO:
kwenye kisa cha kwanza K cha kukojoa kitandani, baada ya siku kadhaa ikaanza kusikika harufu ya uvundo wa mikojo chumbani, usafi wa kina ulipofanyika ilipatikana BUKTA ya bwana mdogo yenye mikojo chapa chapa, ndipo ilidhihirika KOJO lile alilimwaga nani........
wakubwa huwa hawaombi msamaha...... Basi akaagizwa mjomba ikifika jumamosi anipeleke SENEMA , tukaangalia kwenye gazeti kutakuwa na senema gani, NEW CHOX, AVALON, ODEON, EMPIRE, EMPRESS ........ nikachagua EMPIRE na EMPRESS , ambapo kulikuwa na senema ya SEVEN STEPS OF KUNGFU (kama bado nakumbuka) na nyingine niyoweza kuikumbuka kwa sasa ( nikanunuliwa na BAZOKA) nilifurahi sana kwa zawadi zile
Kwenye kisa cha pili : napo ilikuja kudhihirika baada ya jioni mama kumwangalia dogo vizuri, kumbe ile glass ilipovunjika, wakati anaokota vipande vya chupa vilimkata kidogo.......
mama aliishia kusema MTAKUJA KUNIUMIZIA MWANANGU KWA MAKOSA WANAYOFANYA WENGINE


Tukirejea kwenye VICARIOUS LIABILITY....... BASI TUSIACHE KUTAZAMA "FALSE FLAG"
 
Ni kweli kabisa sisi Wakatoliki tuna tubu kabisa dhambi ya kutotumiza wajibu.

Nimekosea mimi, nimekosa mimi nimekosa sana.
 
Huko kuacha legacy ya kukumbukwa vizazi na vizazi je, wenzake watakubali?
 
Vicarious liability,hii ni shule muhimu,Mungu awafungue macho Viongozi wetu watambue Kuna karma
 
wanatumwa na nani kwenda kuua watu?
 
Kaz Kweli Kweli, Mwingine tena!
 
Mfani Iddi Amini wa Uganda alikuwa anauwa waganda mwenyewe au watu wake? Ukishindwa kuwapata wanaua na kiteka na wewe ndiyo umeaminiwa na wananchi kuwalinda sasa unafanya nini hapo kwenye nafasi hiyo? Mbona hii ni elimu ndogo sana ina maana Viongozi wetu hawajui juu ya huo uwajibikaji?
 
Msikilize Buddha anasema nini:
A monk commands a monk saying,"Tell so- and-so,let so-and-so tell so-and-so,let so-and-so deprive so-and-so of life," there is an offence of wrong-doing. The murderer accepts,there is an offence of wrong-doing. He deprives him of life, THERE IS NO OFFENCE FOR THE INSTIGATOR,there is an offence of wrong-doing for one who gives the order and for the murderer.

Lakini hapo awali Buddha ameweka mazingara kama haya lakini akasema instigator ana hatia.

I can only imagine kwamba instigator hana hatia akifanya mambo kwa siri.
Lakini kama akijitokeza hadharani basi lazima aunganishwe katika hiyo kesi.

Kwa hiyo kama watu wamenifuata mimi wananiuliza,"Tell us your honest opinion,yule mtu anapaswa kufanya nini?"
Mi nikisema yule mtu ni habithi siwezi kulaumiwa akiuawa.

Halafu pale anasema THERE IS NO OFFENCE FOR THE INSTIGATOR but there is an offence of wrong-doing for the one who gives the order and for the murderer.
An offence of wrong-doing is not a real offence. Ni kama kusema someone is "naughty".
Makosa makubwa yakifanyika Buddha has other ways of describing them.
 
Wanasheria aggresive si ni kama ww? Kwahiyo unaamini kwa mahakama hizi za simu moja hata uwe mwansheria aggresive kuna lolote utafanya?
 
Masuala ya uhai ni mazito sana, amri mojawapo inasema Usiue na kanisani tunakumbushwa mara nyingi wakati wa misa juu ya amri hiyo.

Samia akiwa mwanamama wa kiislam anaweza kuaminika kwa kauli yake. Lakini nafasi yake ya urais ni mamlaka makubwa na taasisi zote zipo chini yake.

Kama ameitenda hiyo dhambi ya mauaji na atubu kwa uwezo wake wote na nia itoke moyoni mwake. Bahati nzuri Uislam au Ukristo kwa ujumla unatambua nini maana ya kutubu pale unapokosea.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…