Wanabodi
Nimejitolea kuwa mwalimu wa kujitolea wa somo la katiba, sheria na haki, ili kuwaelimisha Watanzania kuhusu haki zao na wajibu wao.
Kujitolea kuwa mwalimu somo la katiba, na sheria, nimehamasishwa na yeye mwenyewe
Rais Samia ana nia njema Watanzania wapate haki, ila Watanzania hawajui Haki! Je, Tumsaidie kuelimisha umma Katiba, Sheria na Haki au? hebu msikilize mwenyewe akizungumza
View: https://youtu.be/PZ_8JFw_5LM?si=LqdibxLmRJXzlhQY ni kufuatia hoja hii, ndipo mimi nikajitolea
Kipindi cha TV, Kutoa Elimu ya Katiba, Sheria na Haki, Kuanza Jumapili Hii Kupita Channel Ten
View: https://youtu.be/ZJIKhnZCf04?si=LdYf8WVJTIKw8KCu
Somo la leo ni somo la kitu kinachoitwa vicarious liability. Haya ni mahusiano ya uwajibikaji wa kisheria yanayoitwa fiduciary relationship, yaani uhusiano wa uwajibikaji Kama mke na mume, mzazi na mtoto, daktari na mgonjwa, mwalimu na mwanafunzi, wakili na mteja wake.
Hii fiduciary relationship inampa uwajibikaji wa kisheria wahusika hao, ikiwemo mzazi kuhukumiwa kwa makosa ya mtoto wake wa umri wa chini ya miaka 14.
Kinga hii pia inahusu kutotoa ushahidi dhidi ya mtu huyo, mfano mke akijua mumewe ni jambazi, na ni muuaji, anaweza kusema kuwa anajua mumewe ni jambazi na muuaji ila ana kinga ya fiduciary kutowajibika kutoa ushahidi dhidi ya mumewe. Vivyo hivyo kwa sisi mawakili, unaweza ukawa ni wakili wa muuaji, akakiri ameua kwa 1st degree murder, wewe japo ukweli unaujua, utamshauri akanushe na utamtetea hadi hiyo murder case inageuka manslaughter.
Sasa kuna mauaji mengi yanayotokea na kuwahusisha watu wasiojulikana, kiukweli sio wasiojulikana wote ni wasiojulikana kweli, kuna baadhi ya mauaji yanafanywa na watu "wasiojulikana" kumbe kiukweli watu hao sio "wasiojulikana" bali ni 'wasiojulikana'.
Ili kuwatambua "wasiojulikana" na 'wasiojulikana' tembelea
Shambulio la Lissu: Wajue wasiojulikana watakaojulikana na 'Wasiojulikana' ambao kamwe, hawatajulikana
Hivyo vitendo vyovyote vinavyofanywa na 'wasiojulikana' kwa kujifanya ni "wasiojulikana", then anayewatuma ana wajibika nao vicariously.
Hoja hii ni kufuatia hoja hii humu jf Naunga mkono hoja, mtu mwenye wajihi kama huu,
Siku ya Wanawake Duniani: VP Samia Suluhu: "Womanly, Genuine, Humble, Simple na Down To Earth!” hawezi hata kuua panya!, kama ni kuua labda mbu, mende na sisimizi.
Ila kwa vile yuko serikalini na yeye ndie mkuu wa serikali, na anajua kuna mazingira fulani, serikali zote duniani huwa zina waua watu hatarishi kwa usalama wa nchi, dissidents, na kabla hawa dissidents hawajauliwa lazima CinC asaini ile death warrant, then death warrant yoyote ikisainiwa, aliyeua ni aliyesaini death warrant na sio wale watekelezaji.
Ikitokea makosa ya watu wake kumuua kwa makosa mtu safi kwa kudhaniwa ni dissident, then the blood of that person is upon aliyetoa hiyo order kwa niaba yake.
Na kunapotokea vifo ambavyo vingezuilika kwa kufanya kitu lakini hakikufanyika, then damu iliyomwagika is upon yule ambaye angezuia lakini hakuzuia.
Hivyo tumeshauri
Kama Walioua ni "Wasiojulikana" Then Karma, Albadir Itawahusu, ila kama ni 'Wasiojulikana', Hata Albadir Haisaidii Kitu, Wametimiza Tuu Wajibu Wao!
Hata yale matukio ya utekaji, utesaji na mauaji enzi za kipindi kilee... watu humu tulishauri
TISS Ikanushe tuhuma za uvamizi, utekaji, utesaji na mauaji!. Wasijadiliwe na Bunge kwa uwazi bali wachunguzwe, wakithibitika wafumuliwe! hao majamaa wali mute kimya, wakijua hawawezi kufanywa lolote, lakini mwisho wa siku aliyewajibishwa na top boss wao!.
Hivyo ni muhimu sana kwa viongozi wetu kuijua hii vicarious liability kwa vifo vyovyote vya kizembe vinavyotokea chini ya mamlaka yao hata kama hawatashitakiwa popote, lakini hukumu ya haki hapa duniani ya karma ii juu yao!.
The Power of Karma- Ndio hukumu pekee ya haki kamili hapa Duniani. Unahukumiwa kwa matendo yako! tena tumewashauri watu waache kupiga ramli chonganishi
Tuacheni ramli chonganishi: Tusihukumu tusije tukahukumiwa. Karma ndio pekee hutoa hukumu ya haki hapa duniani!
Kanuni yenyewe ya vicarious liability ni hii
"Vicarious liability exists due to the legal doctrine of respondeat superior, which essentially means “let the master answer.” Employers, parents or others with a superior legal relationship to someone who does harm are expected to answer for those who are under their control.
Vicarious liability rules also exist in order to provide protection to victims of injury. Often, an individual employee or a child will not have the resources to provide compensation to those they harm through their negligence or wrongful actions. But companies and parents generally do.
Through the doctrine of vicarious liability, those who have resources (including the ability to buy insurance) and who were in a position to prevent harm but who failed to do so can be held accountable so victims do not go uncompensated"
Tanzania tuna bahati nzuri sana hatuna wanasheria aggressive wa kutetea watu, vinginevyo tungetumia private investigations kuwabaini hawa 'wasiojulikana' na kuwatundika msalabani, hii ingewafanya viongozi wetu kuwa more responsible for the life of its citizens.
Paskali