Wanasiasa msitufanye wajinga kuhusu mikutano ya kisiasa

Embu tummpe mda mama Samia si kasema tumpe mda tuwe wastaarabu tungojee tuone Magufuli alizuia kabisa mikutano hata ya ndan huyu karuhusu embu chadema na sisi tuonyeshe ustaarabu bas jmn vitu vingine mnatupa kazi kuwatetea msitake tuamini huenda lengo lenu Ni vurugu mbona mama anaenda vizuri tu,Ina maana cdm tukiomba kitu Basi tupewe mda huohuo jmn tukiambiwa tusubiri hatutaki ila kwa magu tulikaa kimya,mtu akionyesha uungwana na sisi tuwe waungwana jmn
 
We mpuuzi Sana, unataka mkutano wa nje ueleze nini, mda wa kampeni umeisha , au unataka uandamane
Ukweli ni mmoja tu kua Ccm na viongoz wenu nchi imeshawashinda toka muda mrefu sana ndo maana kila siku mnaleta visingizio.Magufulj alizurura na kuongea mwenyewe nchi nzima uku radio na vyombo vyote vya habari vikimpamba kwa miaka 5 bado nchi iko vile vile na shida zile zile alizoziacha kikwete ambaye wala hakuangaika kukimbizana na wapinzani.
 
Mikutano ya hadhdara inamzuia vipi kutekeleza majukumu yake?
 
Mikutano inaamsha awareness kwa wanaanchi na usiichukulie poa kabisa , sauti za wanasiasa zinatoa angalizo kwa serikali na kukosoa pale viongozi wanavyoenda tofauti, pia pitia mikutano wanachama wapya wanapatikana, mkitaka kuua vyama vya upinzani basi mzuie mikutano ya hadhara
 

Kumbuka vyama vya upinzani wengi kwasasa hawana majimbo ulitaka wakafanye wapi mikutano yao ya hadhara, maana kama sheria inataka waafanyie kwenye majimbo yao huoni huo ni upuzi, sasa chukuli kwa hali ilivyo sasa, nimekuona bonge la kiazi
 
Shida ya wanasiasa wengi wa upinzani Tanzania ni wa uchwara! na wachumia tumbo, wanaoifanya siasa kama ajira ya kuwapatia kipato, wakati katika nchi zilizoendelea kiuchumi na kubobea katika demokrasia, siasa ni platform ya kujitolea kutumikia umma.

Ndio maana kuna kipindi cha kupiga siasa kutafuta uungwaji mkono wakati maalum wa uchaguzi. Lakini baada ya uchaguzi kila raia ana kuwa bize kuangalia kama chama tawala kilichoshinda uchaguzi kinawatumikia wananchi kama ilivyoahidi kwenye ilani yake, ili waweze kukihukumu kwa kukinyima kura kwenye uchaguzi unaofuata ama kukipa kura kiendelee kuongoza nchi.

Na kosa kubwa na la kujutia ni ile tabia kuvidekeza vyama vya siasa kwa kuvipa ruzuku! ilhali kwa nchi zilizobobea kwa demokrasia, jukumu la kukihudumia chama cha siasa na wanasiasa ni la wanachama wenyewe kwa kupitia harambee mbalimbali.

Mwachani mama Samia achape kazi ya kuwatumikia wananchi.
 

Marekani kwani wamezuiwa? Si kuwa wakiitisha hakuna tu atakayekwenda?

Kwani hapa kabla ya kuzuiwa ilikuwaje?

Ikumbukwe mikutano ya siasa haikuwahi kuzuiwa kabla ya jiwe tangia kuwa kuhalishwa kisheria.

Kwani ilipokuwapo kulikuwa na lipi la kumfanya awaye yote kuizuia?

Mbona imekuwapo wakati wa Mwinyi, Mkapa na hata Kikwette bila shida?
 
Marekani wametoka kwenye uchaguzi juzi kati, je? Bado wanaendelea na mikutano ya siasa?
Ndugu WAMAREKANI wako huru kabisa kufanya mikutano ya siasa na hata maandamano wanapohitaji, HATA kama uchaguzi ulikuwa usiku wa jana yake. Hebu pitia katiba yao.
Yaonekana Mama ana nia ya kuendeleza UKANDAMIZAJI kama ilivyokuwa kwa Mwendakuzimu kutokana uoga wa ki CCM.
Haki kamwe haitakiwi kutolewa kama HISANI, ni kutaka kuturudisha kwenye udhalimu na kuvunja hata hii katiba hii ya sasa hivi.
 
Mpumbavu flani hivi ameandika! Sluggish!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…