Mikopo Consultant
JF-Expert Member
- Oct 28, 2024
- 529
- 1,150
Ukiwa Arusha mjini, mitaa ya Unga Limited, sasahivi yamebakia kuwa magodown, ila wazazi wetu wanatuambia miaka ya 70 na 80 kulikuwa na utitiri wa viwanda vingi sana. Na hiyo ni Arusha; ukienda na mikoa mingine kama Dar es salaam, Mwanza, Mbeya, Tanga na Morogoro, utakutana na similar story. Kwa ufupi Tanzania ilikuwa kabisa inaelekea kuwa industrial economy
Ila sasa cha kushangaza, Tanzania huge industrialization phase haikuchukua zaidi ya miaka 20 (kuna haja ya kutafiti hili suala kwa kina na kujiuliza ni kwanini). Mwaka 1995, asilimia karibu 90 ya viwanda vilikuwa ni kama vipo mfu.
Wasomi wengi sana wa Tanzania walijaribu kuchapisha maandiko kuhusu kufeli kwa Tanzania industrialization na wengi wao wanaishia kutaja ‘generic reasons’ kama; mitaji, rushwa, nguvu kazi n.k na kusahau sababu kubwa kwa upande wangu mimi ambayo ni ‘kushindwa kwa intelligensia ya kuvilinda viwanda’.
Kwahiyo hata wanasiasa wa sasa, wanadhani kwamba shida za kushindwa viwanda ni hizo ‘generic reasons’ ila ki ukweli kabisa mimi naweza kusema, Tanzania ya viwanda ilihujumiwa na ‘sabotage’ ambayo iliweza kufanikiwa kutokana na kushindwa kwa intelijensia ya kulinda hivi viwanda.
Mfano mdogo tu, kama kiwanda chako kina mfumo wa Bulb za Tred halafu mtu aliyekabidhiwa jukumu la kununua Bulb, akanunua Bulbs zenye meno, matokeo yake unadhani ni nini? (huo ni mfano jinsi subotage inawea kukwamisha mambo) na huwa ni ngumu sana kwa mameneja kufuatilia vitu vidogo vidogo kama hivi, lakini, wataalamu wa sabotage wanakuambia hivo vitu vidogo vidogo ndo vyenye nguvu kuangusha taasisi, kwasababu ni rahisi sana kuvi overlook.
Ama mitambo yako inatakiwa ifungwe na screw za 6inch halafu zinanunuliwa screw za 4 inch. Ama unatakiwa kujenga ghorofa kwa kutumia nondo za 15mm halafu zinanunuliwa nondo za 10mm
Maana ya hiyo mifano ni nini? Ukiwa na system kama hiyo, ambayo ipo intact kwenye taasisi zako, maana yake kutatokea mambo yafuatayo
Sasa nimeona ndugu yetu David Kafulila anakuja na PPP yake kwa kasi, embu ningemuomba aje na plan ya namna Tanzania itaweza kulinda viwanda vyake, na sio tu viwanda, hata hizi miradi za SGR na miundo mbinu mingine inapaswa kuwa na strategies za kuwa protected, ki inteligensia dhidi ya 'sabotage'
Taifa la America wapo vizuri sana kwenye haya mambo, nilivyoona andiko la CIA kuhusu sabotage ambalo limeandika mwaka 1944, ndo nikajua kwamba kumbe hawa jamaa bwana wamejipanga kila idara. Kuna manual moja waliandika CIA ambayo kwa sasa ipo declassified, ina title 'Simple Sabotage Field Manual' imeandika mwaka 1944 ila imekuwa declassified miaka ya karibuni, hii manual ilitolewa maalum kwa ajili ya kuwasaidia undercover wa CIA kuweza ku sabotage na kuviua viwanda vya nchi za ki communist. Kwahiyo humo wameelezea tricks mbalimbali za sabotage, japo ina setting ya manufacturing, ila maudhui ya kitabu yana apply sehemu pana zaidi.
Mambo kama haya na mengineyo, ya kufanana na haya, ndo yananishawishi kwamba, watu ambao hawana elimu nzito na high IQ, wasisogeze kabisa pua kwenye uongozi wa taasisi za nchi hii.

- Kupotea rasilimali, ukienda store utakutana na maboksi ya materials mpya ambazo zimenunuliwa lakini hazitumiki kwasababu zina specifications tofauti
- Cost structure lazima ibadilike, kutokana na frequent maintenance. Sasa kama machine ilihitaji 6inch screws wewe ukaifunga 4inch, what do you expect?
- Total collapse lazima itokee, kwasababu hakuna namna hiyo system itakupa efficiency ya Zaidi ya 90%, maana yake hata output haiwezi kuzalishwa efficiently. (Na hichi nadhani ndicho kiliikumba Tanzania yetu ya viwanda)