Wanasiasa wanashinikiza suala la FEI TOTO na kuleta VITISHO

Chizi Maarifa

JF-Expert Member
Joined
Jul 29, 2013
Posts
10,931
Reaction score
24,816
Nawafahamu watu hawa. Ndiyo ambao walimwita Fei Toto na kumchimba mkwara. Wakaharibu zaidi wakati sisi tunaenda kuongea na mama yake amkanye mwanawe wao wakaona wamwite yeye.

Screenshot 2023-01-07 at 11-00-26 Saleh Jembe (@salehjembefacts) • Instagram photos and videos.png

===
Alichoandika Saleh Jembe kwenye Ukurasa wa Instagram

WANASIASA ACHENI KAMATI ITENDE HAKI, MSISHADADIE DHULMA..

Taarifa zinasema kiungo @feisal194 ALIWEKA MSIMAMO kuwa hayuko tayari kurejea Yanga kwa kile alichoamini ni dharau au kutopewa thamani....akasisitiza yu tayari hata kutocheza mpira iwe kwa kufungiwa au vinginevyo lakini ASIRUDI.

Tusijikite kwenye kulaumu kokote (Yanga au Feisal), lakini tutambue Fei ni kijana na anajitambua kwa kuwa anapigania maisha yake. Yanga nao walimlea kwa muda waliyekuwanae lakini muhimu ni haki katika hili.

Kamati imekaa na majibu yalipatikana jana (SIJUI KWA NINI HAYAKUTANGAZWA)...vizuri sana ikawa haki na ushauri viongozi wa kisiasa ambao wanapenda mpira na klabu zao wakae kando na waiache kamati ifanye kazi yake sahihi ili mwisho kusiwe na hisia za KULAZIMISHWA, KUSHAWISHIWA AU VINGINEVYO....

Hakuna haja kwao kupiga simu wakihoji matokeo au kutaka yawe ya upande fulani...hili ni suala la kisheria lina njia zake sahihi...

HAKI ITENDEKE KWA MUJIBU WA MASWALI NA MAJIBU KIKAONI PIA KWA HESHIMA YA KAMATI, MPIRA NA HATA SHIRIKISHO LA SOKA KWAMBA HAKI IPO BILA SHINIKIZO LA MATAJIRI AU WANASIASA...
 
Hata hao TFF wenyewe na Kamati zao sio wa kuwaamini, wanatumiwa na wanasiasa, mfano lile suala la Manara na Hersi mpaka leo bado halijatolewa maamuzi na TFF, nani atawaamini hawa kwenye kutenda haki kwa mchezaji?

Binafsi, nimekuwa nikiamini haki iko upande wa mchezaji toka siku ya kwanza, kwani siku zote mikataba hutakiwa kujieleza kama ilivyo, haitakiwi kuleta habari nyingine nje ya hapo za utaratibu au vyovyote, kwani hayo ni mazoea tu yasiyokuwa na maana yoyote kisheria.

Kama umejibana mwenyewe kwenye vipengele vya mkataba ulioingia na mchezaji wako, usitegemee kutokea kwenye "utaratibu" au utatokea kwenye huo "utaratibu" kama upo kwenye vipengele vya mkataba husika, lakini kama haupo, jilaumu mwenyewe, wala hapa usitegemee ukubwa wa jina la timu yako.

Kimsingi Yanga walikuwa wanalazimisha utaratibu ufuatwe ili wapate nafasi ya kumtongoza mchezaji, tena kwa kuwatumia hao wanasiasa wanaoingilia maamuzi ya TFF hivi sasa, huu ni ukweli halisi, na mashabiki wao nao wakauvaa huu usanii wa viongozi wao, utopolo msinune mkiambiwa ukweli huu, Feisal hawataki, wala haki haipo upande wenu, kubalini tu hii habari iishe.
 
Swala la Feisal halihitaji mwanasiasa kuingilia kati, tulisha waaambia mmemwingiza choo Cha kiike mchezaji.

Sasa inabidi mkubali mli mpotosha mchezaji Kwa tamaa zenu na ghramazake inabidi mchezaji na familia yake wazi bebe wakati nyinyi mmesha kimbia.
 
Nawafahamu watu hawa. Ndiyo ambao walimwita Fei Toto na kumchimba mkwara. Wakaharibu zaidi wakati sisi tunaenda kuongea na mama yake amkanye mwanawe wao wakaona wamwite yeye.

View attachment 2471728
Suala la fei toto liko wazi sana wala alihitaji mtu yeyote kuingilia kati msianzishe ujinga ujinga wenu hapa kuwasingizia wanasiasa, leteni huo ushahidi kuonyesha wanasiasa wanavyoingilia, Vitu viko wazi na sheria ziko wazi alafu mnaleta habari za kwenye vijiwe vya kahawa hapa
 
Hata hao TFF wenyewe na Kamati zao sio wa kuwaamini, wanatumiwa na wanasiasa, mfano lile suala la Manara na Hersi mpaka leo bado halijatolewa maamuzi na TFF, nani atawaamini hawa kwenye kutenda haki kwa mchezaji?

Binafsi, nimekuwa nikiamini haki iko upande wa mchezaji toka siku ya kwanza, kwani siku zote mikataba hutakiwa kujieleza kama ilivyo, haitakiwi kuleta habari nyingine nje ya hapo za utaratibu au vyovyote, kwani hayo ni mazoea tu yasiyokuwa na maana yoyote kisheria.

Kama umejibana mwenyewe kwenye vipengele vya mkataba ulioingia na mchezaji wako, usitegemee kutokea kwenye "utaratibu" au utatokea kwenye huo "utaratibu" kama upo kwenye vipengele vya mkataba husika, lakini kama haupo, jilaumu mwenyewe, wala hapa usitegemee ukubwa wa jina la timu yako.

Kimsingi Yanga walikuwa wanalazimisha utaratibu ufuatwe ili wapate nafasi ya kumtongoza mchezaji, tena kwa kuwatumia hao wanasiasa wanaoingilia maamuzi ya TFF hivi sasa, huu ni ukweli halisi, na utopolo msinune mkiambiwa ukweli huu, Feisal hawataki, wala haki haipo upande wenu, kubalini tu hii habari iishe.
Mbumbumbu akili zenu ni kisoda sana, Mkataba wa fei na yanga umeuona mpaka useme haki iko kwa mchezaji? Ebu tuonyeshe huo mkataba uliokufanya utoe hukumu yako kwamba fei ndio mwenye haki
 
Swala la Feisal halihitaji mwanasiasa kuingilia kati, tulisha waaambia mmemwingiza choo Cha kiike mchezaji.

Sasa inabidi mkubali mli mpotosha mchezaji Kwa tamaa zenu na ghramazake inabidi mchezaji na familia yake wazi bebe wakati nyinyi mmesha kimbia.
Punguza makasiriko basi... Mbona unatokwa na povu kila sehemu ya wazi ya mwili wako.
 
Punguza makasiriko basi.... Mbona unatokwa na povu kila sehemu ya wazi ya mwili wako.
Hamna povu apo, waliomshauri Yuko sahihi Kuvunja mkataba ndio wanao takiwa wawajibike Kwa lolote lisilo jema, nafikiri kabla ya maamuzi ya kumshawishi mchezaji yote ayo waliyafikiria.
 
Una makasiriko na unatoa povu sana.
 
Kwenye hili swala watu wengi wanaongozwa na hisia zaidi kuliko uhalisia. Hata ukisoma comments utaona mwenyewe na mpaka hapa tulipofika hakuna kitu unaweza badilisha juu ya fikra za wengi wanaoendelea kupotosha watu ambao hawaelewi chochote katika hili.

Mfano mleta mada anasema kwemye kikao Feisal katamka hataki kucheza Yanga tena yupo radhi hata afungiwe lakini hajaleta ushahidi kama hayo maneno ni ya kweli au la. Sasa ukikutana na wakurupukaji akili fupi anayachukua hayo maneno kama yalivyo ndio zinakuja zile comments Feisal hawataki, mwingine anaanza kuamini Feisal yupo sahihi. Nakubali anaweza kuwa haitaki Yanga kweli lakini kwa nini tumlishe maneno na kuanza kupotosha wengine.

Tuache kamati ifanye kazi yake tusijaribu kutengeneza chuki kati Feisal na mashabiki kwa kutumia hili ndio maana niliwahi kusema hili swala la Feisal lipo kimkakati kuna watu wanalitumia kwa manufaa yao binafsi. Usipotoshe usikubali kupotoshwa hata Feisal kapotoshwa na wanataka waendelee kuwapotosha wengine. Noo
 
Suala la fei toto liko wazi sana wala alihitaji mtu yeyote kuingilia kati msianzishe ujinga ujinga wenu hapa kuwasingizia wanasiasa, leteni huo ushahidi kuonyesha wanasiasa wanavyoingilia, Vitu viko wazi na sheria ziko wazi alafu mnaleta habari za kwenye vijiwe vya kahawa hapa
Hao ndio walewale wapotoshaji waliompotosha Feisal
 
Mbumbumbu akili zenu ni kisoda sana, Mkataba wa fei na yanga umeuona mpaka useme haki iko kwa mchezaji? Ebu tuonyeshe huo mkataba uliokufanya utoe hukumu yako kwamba fei ndio mwenye haki
Nimewaambia muache hasira, tatizo lenu mnaongozwa na mahaba niue kwa timu yenu.
 
Kwenye hili swala watu wengi wanaongozwa na hisia zaidi kuliko uhalisia. Hata ukisoma comments utaona mwenyewe na mpaka hapa tulipofika hakuna kitu unaweza badilisha juu ya fikra za wengi wanaoendelea kupotosha watu ambao hawaelewi chochote katika hili.

Mfano mleta mada anasema kwemye kikao Feisal katamka hataki kucheza Yanga tena yupo radhi hata afungiwe lakini hajaleta ushahidi kama hayo maneno ni ya kweli au la. Sasa ukikutana na wakurupukaji akili fupi anayachukua hayo maneno kama yalivyo ndio zinakuja zile comments Feisal hawataki, mwingine anaanza kuamini Feisal yupo sahihi. Nakubali anaweza kuwa haitaki Yanga kweli lakini kwa nini tumlishe maneno na kuanza kupotosha wengine.

Tuache kamati ifanye kazi yake tusijaribu kutengeneza chuki kati Feisal na mashabiki kwa kutumia hili ndio maana niliwahi kusema hili swala la Feisal lipo kimkakati kuna watu wanalitumia kwa manufaa yao binafsi. Usipotoshe usikubali kupotoshwa hata Feisal kapotoshwa na wanataka waendelee kuwapotosha wengine. Noo
Wewe unaetaka uoneshwe mkataba kama wewe unao tuwekee hapa tuuone, vinginevyo unahangaika tu; nakuona unapingana na taarifa za waandishi wa habari wenye network ya taarifa kwa ajili ya mahaba niue tu kwa timu yako.

Na unaposema suala la Feisal lipo kimkakati nawe tuwekee ushahidi hapa, usituokotee maneno ya kujiliwaza ili kuuridhisha moyo wako ukataka nasi tuyaamini.

Ajabu wewe ndie unajiona una akili! Kuwa na adabu dogo, haya mambo ya mikataba ni zaidi ya mahaba niue kwa klabu yako.
 
Back
Top Bottom