Hata hao TFF wenyewe na Kamati zao sio wa kuwaamini, wanatumiwa na wanasiasa, mfano lile suala la Manara na Hersi mpaka leo bado halijatolewa maamuzi na TFF, nani atawaamini hawa kwenye kutenda haki kwa mchezaji?
Binafsi, nimekuwa nikiamini haki iko upande wa mchezaji toka siku ya kwanza, kwani siku zote mikataba hutakiwa kujieleza kama ilivyo, haitakiwi kuleta habari nyingine nje ya hapo za utaratibu au vyovyote, kwani hayo ni mazoea tu yasiyokuwa na maana yoyote kisheria.
Kama umejibana mwenyewe kwenye vipengele vya mkataba ulioingia na mchezaji wako, usitegemee kutokea kwenye "utaratibu" au utatokea kwenye huo "utaratibu" kama upo kwenye vipengele vya mkataba husika, lakini kama haupo, jilaumu mwenyewe, wala hapa usitegemee ukubwa wa jina la timu yako.
Kimsingi Yanga walikuwa wanalazimisha utaratibu ufuatwe ili wapate nafasi ya kumtongoza mchezaji, tena kwa kuwatumia hao wanasiasa wanaoingilia maamuzi ya TFF hivi sasa, huu ni ukweli halisi, na mashabiki wao nao wakauvaa huu usanii wa viongozi wao, utopolo msinune mkiambiwa ukweli huu, Feisal hawataki, wala haki haipo upande wenu, kubalini tu hii habari iishe.