Pre GE2025 Wanasiasa wenye msimamo mkali wanakaribia Kushinda, Kuongoza CHADEMA kuelekea 2025?

Pre GE2025 Wanasiasa wenye msimamo mkali wanakaribia Kushinda, Kuongoza CHADEMA kuelekea 2025?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Tatizo wanafadhiliwa na shirika la ujasusi la Marekani na Uingereza, kila mara wanamuita Lissu Ubelgiji kufanya naye vikao vya siri na kumpa mamilioni ya dola ili asababishe machafuko.

Cha kutanya ni kama alivyofanya Mugabe kwa Moses Tsvangirai, mpaka leo nchi iko chini ya wazalendo waliopigania uhuru
Uongo wa darasa la 2 F. Wa kitoto sana.
 
Siasa sio pesa tu ingekuwa pesa Lowassa angekuwa Rais wa Tanzania

Mkapa, Mwinyi na Magufuli wasingekuwa Marais

Siasa ni sayansi

Umeona uchaguzi wa Marekani

Trump katumia 350 us dollars na Kamala Katumia dollar bilion 1 lakini Trump kashinda !!

Pesa sio kila kitu kwenye siasa sema hapa kwetu CCM wanafanya wanavyotaka sababu ya Watanzania wamelala pono!!
Nakubaliana nawe endapo tutakubaliana kwamba siasa inahitaji mtaji wa kipesa kukamilishana na mtaji wa watu na mipango.
Mara kadhaa umemwona lisu akichangisha ili unachokiita sayansi kitekelezeke. Hata kuhamasisha na kufahamisha inahitaji pesa.
Kila kitu pesa i katkat.
Mbowe anahitajika sana CDM hasa kutia nguvu ya kipesa.
Lakin kiukweli amefeli kuleta matokeo chanya hadi kaanza kushtukiwa umamluki.
Kwa usingizi watanzania wamo, ni ngumu kutegemea nguvu ya umma. Njaa imekaza.
Watu wamezoea hali ngumu had wakaamin ni majaliwa.
Mbaya zaid wanaotaka kuwa mbadala hawaonekan kumaanisha kama wa Sahel.
Hata kumaanisha ki BUKUSI BUKUSI!
This country is too big to rely on only 3 brains (LISU, MWABUKUSI, HECHE)
 
Harakati ndani ya Chadema zinachangamka siku hadi siku..

CCM wamepuuza siasa za majadiliano na maridhiano ndani ya CDM na nje ya CDM..

Sio ACT wala vyama vidogo kwamba vinapatiwa ahueni...

Upande wa Chadema shida inaonekana Freeman Mbowe amekuwa mpole sana kwa dola hadi kufika kipindi anaambiwa amepewa Rushwa ..

Na hili limetokana na maridhiano ya Mbowe na Dola ambayo hayajazaa matunda yeyote...

Wahafidhina wanasema lazima Mbowe aachie Ngazi kwakuwa Chama hakiwezi kuendeshwa kwa siasa zile zile za miaka takribani kumi iliyopita...

Kwa sasa CDM ina mbunge mmoja tu wa kuchaguliwa, wachache zaid toka uchaguzi wa 2005...

Sababu za wahafidhina ni kwamba Mbowe amekuwa mpole sana kwa Dola na CDM kimekuwa chama cha majadiliano... "Wanataka mabadiliko"

Hatari ninayoiyona, wanaoongoza mapambano hayo hawana cha kupoteza, wakiongozwa na wafuatao..

1. Tundu Lissu
2. Petet Msigwa
3. Liberatus Mwangombe
4. Lyenda
5. John Jambo Media
6. John Heche
7. Saed Kubenea
8. Rose Mayemba
9. Wilbroad Slaa
10. Rose Mwakitwange
11. Lifeof Mshamba etc

Pamoja na kundi hili la wazi, bado kuna wanachama wengi wanadhani Mbowe ni kikwazo kwao kufanya harakati za kuhakikisha hawaendi kwenye uchaguzi mkuu hali ikiwa kama ilivyo na wanataka 'mabadiliko' ya uongozi haraka sana.

Kwa Mtazamo wangu kutokana na niayoyaona mtandaoni ni kama wanakaribia kushinda...

Na ukitazama kwa undani ni kama hakuna mbinu mbadala ya kufanya CDM iache "kukatwa" kama ilivyokuwa 2020....

Muda utakuwa rafiki mzuri, lakini muasisi wa yote haya ni kukwama kwa Maridhiano, au angalao, minimum reforms kutokufanya kazi kama ilivyoyarajiwa...

Siasa zetu kubadilika sana kuelekea 2025, pengine kuliko tulivyotarajia?

Muda utasema.
View attachment 3172856View attachment 3172859
Mbowe tu ndio anaiwezea Chadema kwa nyakati hizi za sasa.
 
Ndani ya CDM bado hawaaminiani kihusu kuachia madaraka hasa nafasi ya juu ya mwenyekiti. Halafu wanataka demokrasia ya nchi. Kituko hiki. Tungekua na watu makini wa kuhoji demokrasia Chadema wasingekua chama cha siasa hadi sasa hivi.😃😃😃😃😃😃.
Hawatak demokrasia kwa msingi upi?

Uchaguzi ukifika si kila mmoja atachukua form apambane na team yake?

Kujenga chama cha siasa kuwa kama CDM ni miaka na mikaka
 
Tatizo wanafadhiliwa na shirika la ujasusi la Marekani na Uingereza, kila mara wanamuita Lissu Ubelgiji kufanya naye vikao vya siri na kumpa mamilioni ya dola ili asababishe machafuko.

Cha kutanya ni kama alivyofanya Mugabe kwa Moses Tsvangirai, mpaka leo nchi iko chini ya wazalendo waliopigania uhuru
Propaganda ya kitoto kabisa hii ni punguani kama wewe tu anaweza kuiqmini.
 
Propaganda

Lissu ndiye kiongozi pekee aliyebaki Hana makando kando chadema

Weka na Heche

Chama kikienda na Hawa nakuhakikishia 2025 tutagawana mbao!!
Watu wana hamu sana na siasa za namna hii,

Tutafika kwa hayo mapambano?

Siasa za katikati pia CCM hawazitaki... Pengine wakazielewa hizi za kina Lissu
 
Tatizo wanafadhiliwa na shirika la ujasusi la Marekani na Uingereza, kila mara wanamuita Lissu Ubelgiji kufanya naye vikao vya siri na kumpa mamilioni ya dola ili asababishe machafuko.

Cha kutanya ni kama alivyofanya Mugabe kwa Moses Tsvangirai, mpaka leo nchi iko chini ya wazalendo waliopigania uhuru
Uongo wa darasa la 2 F. Wa kitoto sana
 
Propaganda

Lissu ndiye kiongozi pekee aliyebaki Hana makando kando chadema

Weka na Heche

Chama kikienda na Hawa nakuhakikishia 2025 tutagawana mbao!!
Mmhhh....!!! Mbao za wapi!? Chadema ni kama ndege wanaoogelea baharini au ziwani, ukiona kabakiza kichwa juu, unaweza kudhani mwili wake unafika mpaka kwenye kina cha bahari
 
Ili andiko limekaa kitapeli , Mbowe anaondoka pale endapo kura hazikutosha kupitia viakao halali vya chama , utakua pale mpaka wanachama watakapo sema inatosha, chadema ni tasisi ,ipo na maamuzi yake kupitia vikao halali
 
Unajua ukiitazama kwa jicho la mtoto wa chekechekea CCM ,utagundua kua ni CCM ambayo Ndani yake kuna GOVERNMENT -MILITARY SYMBIOSIS.


Aina hiyo ya Uhusiano ambayo chama na jeshi vinategemeana utakubaliana namm kua UNAHITAJI SIASA ZA KIANAHARAKATI KAMA ZA LISSU, SILAA , N.K.


hizi Siasa za Akina LISSU, Huwa zinafanikiwa Kwa sababu kua Moja, HUFANIKIWA KUTEKA MIOYO YA WATU NA KUWAJAZA HASIRA .

SIASA NI SUALA LA HISIA, KAMA ULIVYO MPIRA NA MAPENZI.... MTU YUPO TAYARI KUJIUA, PALE ANAPOONA KITU HAKIPO SAWA.

Hivo Kwa Afya ya CDM , Mbowe amuachie LISSU, Nyinyi ni mashuhuda mpelampela wa LISSU ,kwenye UCHAFUZI wa 2020, mliuona.
Siasa za Lissu ndo za uharakati ndani yake ndo uzaa matokeo kwa Afrika
 
Back
Top Bottom