Wanataka kutoana roho kwa mali alizoacha marehemu baba yao General mbuge

Unaweza share experience tuone lakini Kuna namna inapunguza migogoro inategemea na familia
Mzazi anaweza gawa mali katika upendeleo mkubwa,...hivyo wosia ukachukuliwa kama ni feki kwa baadhi ya warithi na hivyo kuto kukubaliwa na kudhua taharuki,.......ni vyema zaidi sheria ikawekwa juu ya mgawanyo wa mali, itakayo onyesha bayana baada ya mmiliki kufariki, mali zitagawanywa kama sheria itakavyo na si WOSIA,...... kiufupi sikubaliani SANA na wosia...
 
Hapo kosa ni la mzee, Kwa nini hakupangilia vitu kabla umauti haujamfika?
 
Mkuu wote mlikua watoto wa Baba mmoja kwanini msinge gawana wote?
 
Mkuu mfano wewe una wake wawili na watoto kumi sasa hapo uandae urithi wanini?
 
Lakini ukishaa andaliwa kisheria ukathibitishwa na mwanasheria

Tuseme Kuna upendeleo sasa katika wosia ule, jee yule aliyepunjwa ana haki ya kwenda kushtaki ? Ilhali wosia umezingatia taratibu zote kisheria?
Tuelemishane
 
Kama kawaida yetu Bongo...apo utaanza kusikia marehemu alikua anadaiwa na blah blah nyingi ikiwemo wameuziwa
Na nyaraka za kugushi zitatengenezwa faster na tarehe kurudishwa nyuma! Yaani sijui kwa nini kuna watu wanapenda kuchezea mali za Marehemu wakati warithi halali wapo!!??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…