Wanaume, acheni kulazimisha utiifu kutoka kwa wanawake!

Wanaume, acheni kulazimisha utiifu kutoka kwa wanawake!

Waefeso 5:22-33​

22 Wake, watiini waume zenu kama mnavyomtii Bwana. 23 Kwa maana mume ni kichwa cha mke kama vile Kristo alivyo kichwa cha kanisa, ambalo ni mwili wake, naye mwe nyewe ni Mwokozi wa kanisa. 24 Basi, kama vile Kanisa linavyom tii Kristo, vivyo hivyo na wake pia wanapaswa kuwatii waume zao kwa kila jambo. 25 Ninyi waume, wapendeni wake zenu, kama Kristo alivyolipenda kanisa akajitoa nafsi yake kwa ajili yake ili 26 alitakase. Alifanya hivyo kwa kuliosha kwa maji na kwa neno lake 27 ili ajipatie kanisa linalong’aa, lisilo na doa wala kunjamano wala kitu kingine cho chote kama hicho; liwe takatifu na bila kasoro. 28 Vivyo hivyo waume wawapende wake zao kama miili yao. Anayempenda mkewe anajipenda mwenyewe. 29 Hakuna mtu anayeuchukia mwili wake mwenyewe, bali huulisha na kuutunza vizuri, kama Kristo anavyolitunza kanisa lake. 30 Sisi tu viungo vya mwili wake. 31 “Kwa sababu hii, mwanaume atamwacha baba yake na mama yake, naye ataungana na mkewe, na hawa wawili wata kuwa mwili mmoja.” 32 Hili ni fumbo gumu kueleweka, nami nasema kuwa ni kielelezo kuhusu Kristo na kanisa. 33 Hata hivyo kila mmoja wenu ampende mkewe kama anavyoipenda nafsi yake; na mke naye ahakikishe anamheshimu mumewe. Watoto Na Wazazi
Hapa tuko pamoja 💯

The right man will lead & the right woman will follow. Kinyume na hapo lazima tuumizane vichwa tu.

Mfano wa Nifah na Kaka Mzuri ndio haswa nnachozungumzia. Amepata mtu sahihi kwahiyo hahitaji kulazimishwa wala kujilazimisha kumsikiliza, kumfuata wala kumtii.
 
Mwenyejii nimecheka had machozi, juzi tyuh kuna mtu aliniuliza "unataka nifanyeje kwako ili uwe na furaha na amani" nkamjibu "nipendee yaan nipende had nichanganyikiwe nihisi duniani tunaishi mie na wee tyuh"

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
😆😆😆😆😆

Ni hilo tu kwakweli!! 😉
 
Uniheshim au usiniheshimu wala sio tatizo as long u dont intefere my biznes n life

Shida kwang inakuja pale una vuka mipaka ,yan umeshindwa kukaa hukoo ma dharau zako ukaamua kuja kunishushia my personality mbele za watu.

Hapoo sikuachi hata iweje.
 
Hello guys, bado tupo January, so Happy New Year!!

Ni muda sasa nimekua nikisoma na kusikia wakaka mnavyolaumu wanawake kukosa utii na heshima kwenye ndoa na mahusiano, kuwa jeuri sana na kuendekeza gubu.
Imefika mahali elimu na mafanikio ya mwanamke ndio vinaonekana kuwa chanzo cha matatizo haya, pamoja na mengine mengi.🙁

Binafsi sikubaliani nanyi hata kidogo.

Utii hauletwi na mtu kutokua "msomi"! Utii, kama vitu vingine vingi ambavyo hutolewa kwa hiari huwa havitolewi isipokua pale muhusika anapoonekana anastahili.

You can instill fear on a person, ukanunua nidhamu ya uongo, ngono, mapenzi ya kinafiki and so on...ila upendo, utii na kujaliwa ambako ni halisi (real/genuine) hutolewa kwa hiari, na hiari haishurutishwi hata siku moja. Si kwa mazingira (circumstances), uhitaji, pesa, hofu, wala nguvu ya mtu.

Tatizo linakuja pale mnapotaka kuchukua bila kutoa. Trust me, you can not take without giving!!

Wanaume nyie mnataka tuwapende, mnataka tuwajali (mbembelezwe na kupetiwa petiwa), tuwaheshimu, tuwatii, tuwasikilize, tuwa-appreciate etc. , ila nyie mnafanya juhudi gani kututengenezea mazingira/ kutuweka kwenye position ya kuwapa hayo yote na zaidi bila kujiona wajinga? Pengine tunafelishana in the sense that hamna anaetaka kuonekana mnyonge, nyie mnatuonyesha ubabe kwahiyo na sisi tunawaonyesha jeuri.

Hii pia inatokana na the fact that kuna baadhi wanakuwa na watu ambao sio sahihi kwao, either kwa tamaa, uzembe ama haraka ya kuingia kwenye mahusiano. Mtu wa hivi hata umbebe mgongoni, it will never change the fact that HAKUPENDI! Anaweza akawa anakuhitaji kwa sababu moja ama nyingine, but that's pretty much it.

Ukweli ni kwamba, ukiwa na mtu sahihi kwako na ukam-treat vizuri, she'll naturally become your peace...and vice versa!

Tukiacha kushindana, kila mmoja akaanza kumpa mwenzie kila anachoweza kumpa without conditions, judgement, or holding back, maisha yatakua rahisi sana.
Tafuta mume uolewe wewe!
 
Tatizo Upendo wetu mmeugeuza chanzo cha mapato. Ili uone umependwa hutaki kuoneshwa upendo pekeyake ule upendo wa lugha za mahaba na vizawadi eti ni hadi upewe hela ya kodi na takataka zingine ndio unaona unapendwa.
Ila wee extro unaonekana bakhili sana, khaaah
Kila mahusiano au mapenzi lazima uongelee suala pesa.

Kwan ukimpa huyo dear ako hela unapungukiwa nn?
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Tatizo Upendo wetu mmeugeuza chanzo cha mapato. Ili uone umependwa hutaki kuoneshwa upendo pekeyake ule upendo wa lugha za mahaba na vizawadi eti ni hadi upewe hela ya kodi na takataka zingine ndio unaona unapendwa.
Hili ni tatizo kweli...

Lakini bado mi ntaendelea kusema kwamba ukiona umegeuzwa kitega uchumi na upendo unaopewa unategemeana na kiasi cha pesa unachompa mpenzi wako basi jua you are just a means to an end, not the end itself, kwasababu ndicho nnachoamini.
 
Samahani, niko out of topic, hii tabia ya nyie wadada kuita wanaume "rafiki" huwa mkituita hivyo mnamaanisha nini hasa? Like mnamaanisha rafiki kama kiunganishi tu cha maneno, au mnamaanisha kuwa hamuwezi mpa papuchi huyo mwanaume ndo maana mnamuita rafiki Kelsea Mzee wa kupambania
Kiunganishi tu sina maana nyingine zaidi.
 
Back
Top Bottom