Wanaume, acheni kulazimisha utiifu kutoka kwa wanawake!

Wanaume, acheni kulazimisha utiifu kutoka kwa wanawake!

always the fittest will survive, kama ilivyo kwenye kila nyanja ya maisha, ndivyo ilivyo kwenye mahusiano, ni uhalisia

Fittest in which areas?
.emotional intelligence
.emotional maturity.

Wacha mtifuano uendelee, wacha debate zipambe moto, wacha kila upande ujenge hoja zake muhimu don't get physical.
 
Nshaona, lakini mwanamke hapendi na kutii sehemu isiyo na maokoto hasa wanawake wa mjini. Wanatafsili upendo wakweli ule unaombatana na maokoto na si upendo peke ake kama alivyosema mkuu Extrovert .
Na ni jukumu lako wewe kama mwanaume kutambua sababu ya utii wa mwanamke wako kwako. Kama sababu ni maokoto muache mapema maana siku ukiyakosa utautafuta utii wa mwanamke wako mpaka kwa viongozi wa dini na hutaupata.
Uamuzi ni wenu
 
Na ni jukumu lako wewe kama mwanaume kutambua sababu ya utii wa mwanamke wako kwako. Kama sababu ni maokoto muache mapema maana siku ukiyakosa utautafuta utii wa mwanamke wako mpaka kwa viongozi wa dini na hutaupata.
Uamuzi ni wenu
Ndio maana watu wenye busara na hekima wanashauri vijana waoe mapema kabla hawaja na uchumi imara, ili kuweza kubaini upendo na utii wakweli ambao hauna msukumo wa maokoto. Sema vijana tunakaza vichwa sana, tunaogopa ndoa tukiwa hatuna uhakika wa kula. Just imagine unapata mwanamke anaekutii na kukupenda ukiwa na uwezo wakumpatia mlo mmoja au miwili, unashindwa kutafuta shida zake za Muhimu lakini bado anaonyesha utii.

Lakini wanawake wasasa ukiwatongoza wanauliza suali la kwanza anauliza unafanya kazi gani, ndio suali la kwanza. Ili apime heshima anayoweza kukupatia na kuangalia security ya maisha yake kwako. Kisha baada yahapo atakupa utii wa size ya mfuko wako ulivyo.
 
Hapa tuko pamoja 💯

The right man will lead & the right woman will follow. Kinyume na hapo lazima tuumizane vichwa tu.

Mfano wa Nifah na Kaka Mzuri ndio haswa nnachozungumzia. Amepata mtu sahihi kwahiyo hahitaji kulazimishwa wala kujilazimisha kumsikiliza, kumfuata wala kumtii.
Mwenyewe nimenyooka hadi najishangaa 😂😂
 
Umesema upande mmoja. Upande wa pili ni, Heshima ni tabia na malezi.

Uwezo wa kuonesha heshima ni busara. Na malezi ya watoto wengi ambao ndio wanawake wa sasa sehemu hii ilisahaulika sana.

Heshima ya kweli Iko ndani ya moyo wa mtu. Kinachoonekana kwa wengine ni treatment tuu inayojengwa juu ya heshima iliyoko ndani ya moyo wa mtu.

Kama.mtu hakulelewa kujiheshimu yeye mwenyewe, na wanaomzunguka, vumilia tuu Hilo ni zigo lako. Wanawake/Wanaume wote self-centered, wale wa take me as I am, hawawezi kamwe kuwa na heshima... Mnaweza mkaigiziana tuu kwa muda... Ila the truth is heshima ni zao la upendo genuine.

Na wengi Wala hatupendani kihiiivyo, tunacheza tuu character kwenye igizo la mahusiano.

Anayekupenda kweli kweli kabisa, atakulinda, atakutetea, atakupa uhuru, atakuonya na atakuficha..maana wewe ni wa thamani kwake. Na hiyo ndio heshima... Sio kusikiwa tuu hata kusikia kwa watu wawili wanaopendana huo nao ni usikivu.
Anayekupenda kweli kweli kabisa, atakulinda, atakutetea, atakupa uhuru, atakuonya na atakuficha Na hata kuomba fedha..maana wewe ni wa thamani kwake. Na hiyo ndio heshima... Sio kusikiwa tuu hata kusikia kwa watu wawili wanaopendana huo nao ni usikivu
 
Back
Top Bottom