Wanaume, acheni kulazimisha utiifu kutoka kwa wanawake!

Wanaume, acheni kulazimisha utiifu kutoka kwa wanawake!

Dr Lizzy Siku zote huwa unaongea facts, kila neno uliloandika naunga mkono 100%

Niwe mkweli, sijawahi kuwa na utii genuine kwa mwanaume maisha yangu yote kama ilivyo sasa kwa kaka mzuri, sipingani nae katika mengi, ni mara chache mno na ni pale ninapoona kabisa kwamba hili sio sahihi.

Kupitia yeye nimegundua kila mwanamke ni mtiifu kwa mwanaume anayempenda kweli, na mwanaume huyo akawa muungwana asiye na chembe ya shaka juu ya upendo wake kwako. Yani kwamba akisema kitu kwa kuwa unajua anakupenda unaona kitakuwa chenye manufaa/sahihi.

Lakini kwa mwanaume mbabe, asiyejali kwakweli asahau utii wa kweli kutoka kwa mwanamke. Huwa tunawadanganya kutii ila kiukweli ni tunawapuuza kuepusha ugomvi.
Ngoja nisave hii
 
Anayekupenda kweli kweli kabisa, atakulinda, atakutetea, atakupa uhuru, atakuonya na atakuficha Na hata kuomba fedha..maana wewe ni wa thamani kwake. Na hiyo ndio heshima... Sio kusikiwa tuu hata kusikia kwa watu wawili wanaopendana huo nao ni usikivu
Still kuna watu hawatoi huduma bila kuombwa, yaani furaha yake asikie anaombwa hela ya kusuka, nk. Sasa mtu wa hivi mdada asipoomba hela kwake ataipataje?
 
Still kuna watu hawatoi huduma bila kuombwa, yaani furaha yake asikie anaombwa hela ya kusuka, nk. Sasa mtu wa hivi mdada asipoomba hela kwake ataipataje?
Mwanaume akijua unamtii na hujatanguliza shida zako mbele atakuhudumia kadri ya uwezo wake, bila hata kuomba. Ukiona hakupi basi anavipaumbele vingine vya msingi kuliko shida zako.
 
Hello guys, bado tupo January, so Happy New Year!!

Ni muda sasa nimekua nikisoma na kusikia wakaka mnavyolaumu wanawake kukosa utii na heshima kwenye ndoa na mahusiano, kuwa jeuri sana na kuendekeza gubu.
Imefika mahali elimu na mafanikio ya mwanamke ndio vinaonekana kuwa chanzo cha matatizo haya, pamoja na mengine mengi.🙁

Binafsi sikubaliani nanyi hata kidogo.

Utii hauletwi na mtu kutokua "msomi"! Utii, kama vitu vingine vingi ambavyo hutolewa kwa hiari huwa havitolewi isipokua pale muhusika anapoonekana anastahili.

You can instill fear on a person, ukanunua nidhamu ya uongo, ngono, mapenzi ya kinafiki and so on...ila upendo, utii na kujaliwa ambako ni halisi (real/genuine) hutolewa kwa hiari, na hiari haishurutishwi hata siku moja. Si kwa mazingira (circumstances), uhitaji, pesa, hofu, wala nguvu ya mtu.

Tatizo linakuja pale mnapotaka kuchukua bila kutoa. Trust me, you can not take without giving!!

Wanaume nyie mnataka tuwapende, mnataka tuwajali (mbembelezwe na kupetiwa petiwa), tuwaheshimu, tuwatii, tuwasikilize, tuwa-appreciate etc. , ila nyie mnafanya juhudi gani kututengenezea mazingira/ kutuweka kwenye position ya kuwapa hayo yote na zaidi bila kujiona wajinga? Pengine tunafelishana in the sense that hamna anaetaka kuonekana mnyonge, nyie mnatuonyesha ubabe kwahiyo na sisi tunawaonyesha jeuri.

Hii pia inatokana na the fact that kuna baadhi wanakuwa na watu ambao sio sahihi kwao, either kwa tamaa, uzembe ama haraka ya kuingia kwenye mahusiano. Mtu wa hivi hata umbebe mgongoni, it will never change the fact that HAKUPENDI! Anaweza akawa anakuhitaji kwa sababu moja ama nyingine, but that's pretty much it.

Ukweli ni kwamba, ukiwa na mtu sahihi kwako na ukam-treat vizuri, she'll naturally become your peace...and vice versa!

Tukiacha kushindana, kila mmoja akaanza kumpa mwenzie kila anachoweza kumpa without conditions, judgement, or holding back, maisha yatakua rahisi sana.
upewe maua yako faster, you nailed it Dr 🥰
 
Mwanaume akijua unamtii na hujatanguliza shida zako mbele atakuhudumia kadri ya uwezo wake, bila hata kuomba. Ukiona hakupi basi anavipaumbele vingine vya msingi kuliko shida zako.
Umejibu kama vile unamjibu mwanamke 😃
Hilo swali limetokana na uhalisia fulani. Kuna workmate wangu ana hilo tatizo tena kwa mke wake wa ndoa kwa vitu vya msingi. Hivi mwanamke wa ndoa sio kipaumbele kwa mmewe?
 
Samahani mkuu nilijua ni ke.

Mwanamke wandoa nikipaumbele Kwa mumewe, lakini mnapoishi pamoja ela yakusuka sio jambo Muhimu kama ela yakula haipo.
 
Samahani mkuu nilijua ni ke.

Mwanamke wandoa nikipaumbele Kwa mumewe, lakini mnapoishi ishi pamoja ela yakusuka sio jambo Muhimu kama ela yakula haipo.
Well, kusuka nimetumia tu kama mfano, halafu sizani kama mwanamke wa ndoa anaweza omba hela ya salon huku anajua home hakuna chakula.

Ninachomaanisha ni kwamba pamoja na mwanaume kujua kwamba mkewe ni jukumu lake lakini hampi hela yoyote bila kuomba. Namaanisha nje ya matumizi ya familia, hata aone mke wake hana nguo, n mpaka mwanamke aombe ndio apewe.
 
Point ni kwamba mwanamke anaekupenda hata kuomba fedha kiholela Nifah embu tia neno apa ni kweli au si kweli??
Katika mjadala ambao siupendi ndio hayo masuala ya kuombana pesa katika mahusiano, ni mambo ya kipumbavu sana.

Hakuna uhusiano wowote kati ya mapenzi ya kweli na pesa. Mwanamke hawezi kusema anampenda mwanaume kiukweli sababu ana pesa, ni uongo.
Na mwanaume hawezi kusema anapendwa kiukweli sababu ana pesa, ni uongo pia.

Ufike wakati tutenganishe haya masuala, wenye ajenda hizo wana maana nyingine tofauti mapenzi.
 
Swali langu halikuhusu kuomba pesa kama sehemu ya mahusiano. Swali langu lilihusu mwanamke ambae yuko kwenye ndoa kuomba pesa kwa ajili ya matumizi yake ya msingi kama kununua nguo nk.
 
alright
 
Mafunzo ya ndoa yanaanzia kwa wazazi wako, wao wenyewe wanavyo ishi, kama mama amuheshimu baba basi asilimia kubwa,huyo mke atakuwa hivyo hivyo. Then juhudi za malezi ya wazazi hasa upande wa kiroho, hapa napo hujenga mke aliye imara kwani ndoa ni tendo la kiroho. Baada ya hapo japo siku hizi tume vipuuza sana Jando na Unyago,hizi mila zilisaidia sana kutengeneza wanawake shoka na wanaume mashababi sana.

Siku hizi kwanza wazazi wenyewe wapo hovyo, hawa fuatili maswala ya kiroho na hata haya maswala ya mila ambazo ni chanya kwa makuzi ya kiroho hawana time nayo. Hapo ni ngumu mwanamke kuja kuwa mke bora na kumuheshimu mwanaume na hata mwanaume atakuwa mwanaume asiyejua majukumu yake.

Ndio maana siku hizo kutokana na kuvipuuzia hivyo vitu,watoto tumewaachia walimu mashuleni, wafanyakazi wa ndani na wanaharakati watulele watoto na hamna ujinga ambao ambao tumeulea na kuupeleka mpaka kwenye mitaala mashuleni wa 50/50 na usawa wa kinjia.Huu ujinga una impact mbaya kwa mtoto wa kiume, kwani mtoto wa kiume hitakiwi ufikiria kuwa sawa na mwanamke na vile vile humfanya mwanamke awe na kiburi, jeuri tu kwa sababu ya kuambia yy ni sawa na mwanaume na hasa zaidi akiwa na hela/elimu ndio kabisa.

Ila kama wazazi wametimiza majukumu yao ya malezi kiroho na kimwili, wao wenyewe wanavyo ishi vizuri nyumbani na still wame mfunda kupitia mafunzo ya jando na unyago. Huyo mwanamke hata awe Prof atamuheshimu na kutimiza majukumu yake na hata mwanaume atakuwa na mume bora.

Tatizo siku hizi hatuna mifumo ya kumuamdaa kijana kwa maisha ya ndoa na sio kwamba haipo,ipo ila tumidharau.
 
Swali langu halikuhusu kuomba pesa kama sehemu ya mahusiano. Swali langu lilihusu mwanamke ambae yuko kwenye ndoa kuomba pesa kwa ajili ya matumizi yake ya msingi kama kununua nguo nk.
sio lazima awe kwenye ndoa, hahahah kama unampenda mwanamke wako utampa tu hela ya matumizi kwa moyo mmoja bila kuwaza unahonga
hii dhana ya kuwaza unahonga ndio inaumiza wanaume wengi, na kuna wanaume bahili hadi huruma
unashindwa nini kumhudumia mwanamke wako kwa uwezo wako uliopewa na muumba? mimi huwa nashangaa sana sana
 
Umejibu bila kusoma comments zilikotoka.
Siongelei huo upande unaotetea wewe. Fanya reference
 
Back
Top Bottom