Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 57,761
- 216,011
Unapata mchumba mpenda dini, mnafunga ndoa na hata kanisani anaaminika kiasi cha kupewa uwongozi katika moja ya kamati za kanisa kwakua ana mahudhurio mazuri na pia ana heshimu wakubwa na wadogo katika kauli zake.
Nyumbani mnasali sala asubuhi na jioni, tena mnajikabidhi katika mkono ya Mungu kabla hamjalala. Maisha yanaendelea mpakawmnafanikiwa kununua IST na nyinyi mnaondolewa katika idadi ya wasafiri wa mwendokasi.
Sasa mume anaanza tabia ya kuchelewa kurudi. Mara anaanza kurudi Jumamosi asubuhi, anamkuta mke yuko kwenye sala ya asubuhi, inakua kama ameonyeshwa mlango wa lock uo kituo cha polisi. Ataanza ooh kuna mtu ninamcheck mara moja. Lakini ukimwambia nikimaliza kusali nina andaa chai anatulia.
Haya maneno nimeyasikia mara nyingi sana kwenye women forum. Hii tabia ya kuanza kukimbia ibada baada ya kuchelewa kurudi ina uhusiano wowote na yaliyotokea mlikotoka?