Wanaume kuwa na tabia za kikekike ni janga linaloikumba Nchi yetu

Hii kitu ni upuuzi wa hali ya juu, yaani mwanamume anayepiga goti wakati anamvalisha mwanamke pete ni MPUMBAVU sana
Kuvalishana pete ni utamaduni wa kukopa kwa jamii ya magharibi, Africa hatukuwa na kitu kinachoitwa pete. Tena pete za kuvalishana kama ishara ya upendo and blah blah.

Hivyo: walipoiga huo utamaduni wahusika wanawapigia magoti wanawake zao kama ishara ya kuwaomba mkono kukubali kuolewa nao. Maana yake anayeomba ndiye anayenyenyekea ili apewe, Hamuwezi kuchukua utamaduni wa watu na kuuedit, either muendelee kupiga goti au hilo swala la pete lisiwepo sababu si utamaduni wetu from the first place.

Sisi waafrica tumeiga kila kitu halafu tunalazimisha kuvicustomize viwe vya kwetu na kuharibu maana nzima ya jambo husika. Tuwaachie wahusika utamaduni wao wa kuvalishana pete huku Me akiwa amepiga goti.

My two cents.
 
Hii style ya wanaume kucheza muziki kwa kukata mauno sijawahi kuielewa kabisa, enzi zetu ilikua wanawake ndo wanasifiwa kwa mauno lkn naona siku hizi mambo yamegeuka
 
Kisaikolojia zipo tabia za kike.
Ingawaje zipo tabia ambazo jinsia zote tunaweza kuwa nazo.
Pia zipo tabia ambazo kiasili zinanguvu zaidi kwa jinsia ke kuliko Me. Na kinyume chake.

Kuhusu umbeya hiyo ni tabia inayowavutia zaidi wanawake kutokana Saikolojia ya Wanawake kupenda kujadili zaidi personal issues na hisia zao kwa wengine.
Hii ni tofauti na wanaume ambao kisaikolojia wao huvutwa kujadili zaidi matukio na matendo.

Ishu ambayo itanifanya niongee ni kuwa Mwanaume kuwa mbeya( sio vizuri) kama Mwanamke ( kwake ni sahihi kutokana na maumbile).

Sio tusi kumuita Mwanamke mbeya.
Sio tusi kumuita mwanamke anajipodoa au ni mrembo.
Ila kwa upande wa pili ni tusi.

Kwa upande wa wanawake tatizo ambalo wengi wenu mnaona kama ninawachukia ni kuhusu kupenda Kitonga na uvivu na tabia zingine ambazo sio nzuri.
Je wanawake wote duniani wako hivyo mkuu
 
WANAUME KUWA NA TABIA ZA KIKEKIKE NI JANGA LINALOIKUMBA NCHI YETU.

Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli.

Nyakati za zamani nikiwa nakua zipo tabia ambazo tuliaminishwa ni tabia za kike(inaweza kuwa ni kasumba), ambazo ilikuwa mwiko kwa mwanaume kuwa nazo.
Ilikuwa ni aibu na fedheha kwa kijana kuwa na tabia za namna hiyo.

Nilipofika Kidato cha tano na sita nikaanza kuona muelekeo tofauti wa kile nilichoaminishwa nikiwa mtoto. Ilikuwa mara yangu ya kwanza kuona Wanaume Wambeya, wenye Majungu, Kijichi na wivu wa kipuuzi. Nilisikitishwa sana.

Hivi mwanaume unaonaje woga kum-face mtu na kumchana ukweli ikiwa kama anakosea au unaona hakufurahishi?

Hivi mwanaume unamchukiaje mtu iwe ni Mwanamke au mwanaume mwenzako ambaye hamuingiliani wala kuhusiana kwa jambo lolote?
Hivi mwanaume unamuoneaje wivu mwanaume mwenzako kisa amekuzidi jambo fulani?

Nikamaliza chuo na sasa nipo mtaani kwa kitambo. Aiseeh! Mengi nilichoaminishwa nikiwa mdogo yalikuwa ni uongo mtupu. Labda ilikuwa kweli lakini Wanaume wa sasa ndio wamebadilika na kuwa tabia za KIKEKIKE.

Kula chuma; tabia za kike ambazo vijana wengi wa sasa wapo nazo,

1. Wanaume wengi wa sasa ni Wambeya kuliko Wanawake.
Ni kawaida siku hizi kijana kuwa mbeya. Kuongea mambo ya wengine huku akisahau yake.
Ni kawaida hapo mtaani unapoishi ukipita kijiweni vijana wakaulizana; huyu jamaa anakaa wapi, anafanya kazi gani, ana nini?
Bora hata anayeuliza angekuwa demu tungesema anatafuta Bwana sasa wewe mwanaume mzima unauliza habari za wanaume wenzako ili upate nini?
Umbeya ndio mwanzo wa uchawi na matabia mengine ya hovyo.

2. Chuki za kijingajinga.
Hivi unaanzaje kumchukia mtu ambaye hakuhusu, hukujui wala humjui(ila unataka kumjua)
Unamsikia kijana kama chizi utasikia linasema; huyu dada simpendi anajishaua sana, anaringa sana, hasamilii, sijui anapaka sijui MakeUp za kishamba, n.k.
Au tabia ya kuchukia vijana wenye ubize na kazi zao. Utasikia unaona hiyo bajaji sio yake amepewa na Mjombaake, mara ooh! Ile gari ya mkopo. Ooh! Jamaa hasalimii utadhani salamu inakuongezea maisha. Hizo ni tabia za kikekike.
Kama unataka kusalimiwa Oa, zaa watoto wape chakula wakusalimie Boya wewe.
Haya Hivi huyo dada unayemchukia unamsaidia nini wewe ambaye maisha yako tuu yanakupiga chenga.

3. Majungu na kusengenya.
Hivi hamuwezi kuishi maisha yenu pasipo kuwapiga wenzenu majungu. Hiyo tabia ilihusishwa na jinsia ya kike. Lakini kadiri miaka inasonga ukweli unabainika kuwa hata wanaume wenye Majungu na kusengenyana ipo.
Na hili inatokana na kuoneana wivu, chuki lakini pia na roho mbaya.
Unamsema mwazeko alafu mara nyingi wenye tabia hizo wengi wanasaidiwa au ni Watu walioshikwa mkono yaani wapo sehemu fulani kimazabezabe.

4. Hasira na kuendeshwa na mihemko.
Siku hizi ni kawaida kumkuta kijana analia ati kisa amefanyiwa jambo fulani hata kama ni dogo.
Au unakuta kijana anasusasusa kama jinga fulani.
Au kijana hataki kuambiwa ukweli na kama ikitokea ukimwambia ukweli ati anakuchukia. Hizo tabia wanazo wanawake. Mwanaume ni yule kiume ambaye yupo tayari kuambiwa ukweli na akaustahimili. Sio unaambiwa ukweli unanuna au unarusha ngumi kama mpuuzi hivi.

5. Woga hasa kwa Maboss
Mwanaume mzima unakuwa bendera fuata upepo kama mwendawazimu. Ati chawa! Haya sawa kuwa chawa kwa vitu vya maana, hilo limekushinda.
Woga unasababisha unafiki. Unachekacheka kama Mwanamke mbele ya boss hata kama unaona kabisa hapa Boss kakosea. Hizo ni tabia za kike Boya wewe.

Inakuwa ni aibu kwa Mkeo na watoto. Ati baba yao anatabia za kiajabuajabu. Mwoga, sio jasiri (sio mwanaume).

6. Kuchunguza Maisha ya wengine.
Ufukunyuku ilikuwa tabia za wanawake kufukunyuana mpaka wajue mwenzake anamiliki nini ndani ya nyumba. Lakini siku hizi vijana ndio wamegeuka wafukunyuku.
Hivi kijana unamiaka zaidi ya 25 unafuatilia maisha ya mtu mwingine unataka akuoe au?
Ujue anamiliki nini? Amepataje pesa ya kununulia kiwanja au gari? Ndani kwake ana nini? Unataka akugeuze Mke?
Au ndio unatafuta...? Acha tabia za kiajabuajabu, wewe ni mwanaume.

7. Wivu na tamaa.
Vijana wivu sio tabia ya kiume. Hupaswi kumwonea mwanaume mwenzako wivu wala kuwa na tamaa ya vitu alivyonavyo mwenzako.
Ridhika na kazi yako, Ridhika na mshahara au kipato chako. Fanya kazi kwa bidii. Kupata ni majaliwa. Wajibu wako ni kuchapa kazi kwa bidii na weledi wa hali ya juu, wakati wako ukifika utapata.

Sio uanze kusumbua Watu. Kutafuta Watu ubaya na kuwapa majina yako mabaya ya chuki.

Maisha yasikuendeshe kama kiberenge. Fanya maisha yako na Ridhika na hali yako.

8. Kujipodoa kikike kike.
Wengi wanaotafuta kuwa handsome boy huishia Kufirwa na kuwa Mashoga.
Unataka uzingatiwe kwa utanashati umekuwa mlimbwende?
Unakuta kakijana Kamepaka Kokoto kichwani, Lipustiki midomoni, Kamepaka MakeUp usoni. Kametoboa masikio au kuweka Hereni za kubandika, kamejipigilia unyunyu kananukia, alafu kana onyesha mapaja au kanavaa visuruali vinavyoyatepesha matako yake yawe laini. Utaacha Kufirwa kweli kwa upuuzi wako?

Tabia ya kike ni pamoja na kujipendezesha ili upendwe na Wanawake, uwavutie, wengi huishia kubaya.

Vaa kama mwanaume. Hata kama ni utanashati uwe wa kiwango cha kati kurudi chini.
Vaa suruali nzito ya kium kama unatoka mtoko inaweza kuwa Kadeti, jeans au kitambaa.
Sio uvae vikaptura au nguo za mazoezi wakati haupo kwenye mazoezi.

Pensi vaa lakini angalau zitoke kwenye Goti kwenda chini na kisikubane. Ukisema nisikupangie maisha Fresh,

Ongea kama mwanaume. Usiwe mtu wa lawama lawama kama kinga fulani hivi.

Usiwe mtu wa kuendeshwa na vitu hizo ni tabia za kikekike.

9. Kugombea mademu.
Kugombea demu ni tabia za kike hizo. Wanawake ndio wanagombea wanaume kwa sababu wanaume ni wachache lakini pia wanaume wenye Quality ni wachache zaidi.
Sasa mwanaume mzima unalilia Mapenzi kama jinga fulani hivi.
Unampigia mwanamke magoti kama mwehu. Hizo ni tabia za kipuuzi.

Mwanamke anakuletea maringo piga chini. Kwani lazima wewe uwe naye. Kulazimisha mapenzi ni dalili ya ukike, hujiamini.
Mtu umemfuata, umemueleza hisia zako, kakuringia au analeta manjonjo, sawa ukasema labda ndio Mikogo ya wanawake ili uwambeleze. Taikon atakuambia bembeleza lakini sio uzidishe mipaka.

Mwanamke hakutaki unamlazimisha wa nini Boya wewe.
Ashakuona humfai, au labda hapati anayoyataka. Kwa nini ulazimishe. Matokeo yake ndio ninyi mnaenda mpaka kwa waganga wa kienyeji kisa mapenzi. Hizo ni tabia za kikekike...

Tenda Haki, usiwe mtu wa kulinda pinda, nyoosha maelezo. Usiwe mwoga.

Mtu yeyote (hasa Haters au Watu wasiopenda kujadili mambo kwa hoja"ukweli") asikupangie Maisha kama unachofanya hakikudhuru wewe, familia yako na future yako. Hakikisha unaelewa Watu na kuwaweka kwenye makundi yao.
Hata kama ni mimi Taikon. Kama siongei hoja nipuuze tuu.

Acha nipumzike sasa.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam

Tunashukuru kwa kuwafikia hawa wanawake toleo la pili
[mention]CityHunter1 [/mention] & [mention]Ritz [/mention]
 
sasa huyu [mention]Ritz [/mention] tumuweke kundi gani
 
Wewe kumbe ndio uelewi...

Jogoo mwenyewe anaonga kuku jike kwa kumuitia Chakula hili ampande sembuse Binadamu... Kuhonga, kutoa ahadi, na kutongoza kwa aina yoyote ni njia ya kujaribu kumshawishi mwanamke kwa kumvutia.

Uwezi kuwa na mwanamke akafu husionge, karibu ya wanaume wote huonga... Kuhonga kupo kwenye muktadha mbalimbali, kumpeleka dinner ni kuhonga chakula, kumpa nauli akufuate ni kuhonga....kitu chochote unachotoa hili upate ushawishi kwa mtu ni kuhonga

Shida mnadhani kuhonga mpaka mtu atoe gari au nyumba... vitu, Pesa au Zawadi zozote unazompelekea mwanamke ambaye sio mke wako ni kuhonga.
 
Brazaa unafoka..
Kaka kaka unafoka
Oaa weee una foka mnooo
😂😂😂😂😂😂🙌🙌🙌🙌🙌
 
Back
Top Bottom