Wanaume mmekuwa chanzo cha Wanawake kupitia mateso kwa makosa yenu mliyoyafanya kwa Ex zenu

Wanaume mmekuwa chanzo cha Wanawake kupitia mateso kwa makosa yenu mliyoyafanya kwa Ex zenu

Nimeipenda hii my dear

Hii imemtoa miongoni mwa wababa zangu wadogo kwa bibi yangu mdogo, jamaa kaishi na demu wake wanapika na kupakua,baadae akampiga chini, kibaya zaidi akaoa kisha akaenda kukaa na mkewe katika chumba kile kile alichopanga

Mbona mwamba alipigwa ukichaa wa muda,ila bahati nzuri alikusudiwa yeye mwenyewe na si mkewe,sijajua anaendeleaje now

Kama hutarajii kumuona huyo bidada basi usimpe ahadi ambayo unajua hauta itimiza
Mbaya mkuu… mimi mpk Leo nina maumivu kwa yaliyomtokea ex wangu,, ukizingatia alikuwa bado Kijana mdogo mwenye malengo mengi na amepambana mpk kujipata anataka kula matunda ya kuteseka kwake mwanamke anamkatili uhai wake
 
inatokea bila matarajio
Hakuna hiyo mkuu,, wewe unakaa 6 year na mwanamke tangu akiwa msichana mpk anaelekea umamani then ushampotezea Watu ambao walikuwa serious wanataka kumuoa uka muhold ujaishia hapo umeshamzalisha halafu Leo kafika 32 et uwezi muoa unataka watoto wa 2000 dear utakufa vibaya wewe
 
Hakuna hiyo mkuu,, wewe unakaa 6 year na mwanamke tangu akiwa msichana mpk anaelekea umamani then ushampotezea Watu ambao walikuwa serious wanataka kumuoa uka muhold ujaishia hapo umeshamzalisha halafu Leo kafika 32 et uwezi muoa unataka watoto wa 2000 dear utakufa vibaya wewe
Kwanza kabisa siwezi fanya ujinga huo.
 
Kwetu sijawahi sikia wala kuona mchawi.. kwaiyo mimi siwezi kuwa mshirikina kwenye familia yetu.. mimi mwenzako ni pendapenda sijawahi kusema et huyu namganda.. nikiachwa Leo nikakutana na mwinginee nitampenda na yule nitamsahau
Ghai wale wale,,m mwenyewe nadumbukia kwa mwingine dubwiiii kuepusha matatizo.
 
Sio kila mahusiano lazima yafikie ndoa mkuu...
Na hata mkiwa 10, mwisho wa siku lazima mkubaliane na ukweli mchungu kwamba atakae olewa ni 1 tu...
Mkuu mimi nimekubali sio kila mahusiano yataishia kwenye ndoa je Zuchu atakubali
Ndio maana nimesema wanawake tumetofautiana mkuu
 
Inaumiza sana sana sana

Sasa hivi kumekuwa na matukio yakishamiri ya wanandoa kufariki baada ya ndoa ama siku chache kabla ya ndoa( mimi pia ni muhanga wa kukutwa na hilo tukio japo ilikuwa ni kabla ya ndoa nikapoteza mchumba kwa ajari.. hili sitaki kulizungumzia)

Kama wewe ni mfuatiliaji wa mitandaoni haswa page za kusherehesha utagundua hili jambo, hiki kitu kimekuwa kikipamba moto mno, wanaume kwa wanawake wanafariki muda mchache baada au kabla ya ndoa…

Ukipitia comments nyingi utakuta ni wanawake ndio wamecomment na nyingi zikiwa kama zinafikisha ujumbe kwa wanaume..

Wanaume acheni kuwaumiza mioyo wanawake ambao hamna malengo ya kuwaoa
Hiko hivi wanawake hatufanani kuna kina sisi ambao ukusema mahusiano yamekwisha unihitaji basi nitakubaliana na hali na kusahau na kusonga mbele kama injili, sasa omba mahusiano yako ukutane na kina sisi

Usije ukakutana na kina wale ambao hawajuagi kusamehe wala kusahau utajutaa kwanini ulizaliwa mwanaume,,, hao wanawake ndio hao sasa wabeba visasi ambao wako tayari kwenda kokote kufanya jambo lolote ili mradi akukomoe

Ndio hapo sasa unaposikia bwana/ bibi harusi kafariki miezi 2 baada ya ndoa ama siku 2 kabla ya harusi.. unasababisha watu wasiokuwa na hatia kudhulumiwa uhai wao

Imefikia hatua mpk unaogopa mwanaume atakaenioa ex wake alisamehe na kusahau au na mimi nitajumuishwa kwenye kisasi

Usiseme nimeachana nae kwa amani, wengine huonyesha hivyo mbele yako ukimpa kisogo ndio anaenda kukusemelea kwa babu yake

Nimeleta hili kwasababu kuna mwanaume mwenzenu huko kashasababisha vifo kwa mke na mtoto wake kisa ex wake

Wanaume mnatuhusisha kwenye matatizo ambayo hatuhusiki.. mimi siwezi kujua kila kitu kuhusu mwanaume anaetaka kunioa ukizingatia tumekutana ukubwani.. matokeo yake wanawake ndio tunateswa na ma ex zenu kwasababu zenu ambazo sisi hazituhusu

Imagine unaolewa na mwanaume kumbe alishaishi kinyumba na mwanamke mwinginee kwa ZAIDI Ya Miaka 10 na watoto wa 3,, hivi unafikiri mwanamke kama huyo, akisema analipa kisasi inakuaje??

Kama huna nia ya kuoa acha kumpotezea binti wa watu muda wake.. wanawake huwa tunatunza visasi moyoni anaweza kusema amekusamehe kumbe anakutafutia timing akumalize

Nawasilisha kama hivyo
Mtu kama anaenda ndivyo sivyo anaachwa vizuri tu. Na akijaribu kurusha makombora yatamlipukia mwenyewe. My wife is 100% safe. Yesu hakuja duniani kuzurura!
 
Back
Top Bottom