Wanaume mnalalamika sana, tumewachoka!

Wanaume mnalalamika sana, tumewachoka!

majoto nafasi ya kukwambia kuwa mapenzi sio pesa nikiipata unadhani utanielewa? Hivi huwa mnatumia muda kiasi gani kujua kuwa mwanaume yupo serious? By the way mnapiga mizinga isiyoeleweka kutaka pesa kwa malengo ya kutupima aisee hichi kipimo sio acha tu tutoke nduki ha ha ha ha!

Kuna vitu vingi tu utavijua kwa mtu aliyeserious ikiwa ni pamoja na muonekano wake nashindwa kuvielezea hapa watu hawafanani. Hata wewe unatakiwa umfate mtu aliye serious sio mpiga mizinga .... he he heeeee mbona mtatoka nduki kama kipanga....
 
Wanaolalamika sio wanaochunguza tabia, ni wale wanaotaka vya bure. Kumchunguza mtu ni muhimu sana
Kwa hiyo kila nikiomba tuwe pamoja ili nikufahamu vizuri nivumilie mizinga ? kwa sababu kuwepo pamoja sio kugegedana
 
there is no way wewe umeolewaa....kama umeolewa mmeo anajutaaa anatamani apewe nafasi ya kuchagua mkee mwinginee[emoji28] [emoji28] [emoji28]

Atafute aone mizinga mipya inavyoumiza ha ha haaaa na ole wake akichagua mwingine nakuja kwako
 
Hiyo point yako ya "vya bure hakuna" inamaanisha ninyi mnatuuzia *k* sema tu ww unashindwa kuwa honest about it. Bhasi kuanzia leo na mimi ntaanza tabia ya kukomoa wadada kwa kuwaomba pesa ili ngoma iwe droo majoto

Kazi ni kwako ni hapo mtakapokutana wapiga mizinga wawili.... itajulikana tu nani zaidi... ila humu hatutaki makelele ya ooh mzinga ..... oohhh sijui nini
 
Huwa mnapiga mizinga, mkikataliwa ndo mnakuja na kauli za " unashindwa kunijali".

Ha ha haaa umenikumbusha wa yule aliyeachwa kwa kutokuwa na pesa!! kabaki anali lia tu humu maskini
 
Kuna wanaume wana mapenzi dhati ila sio wepesi kutoa toa pesa hovyo kama wendawazimu na hii ipo pia kwa baadhi ya wanawake wanakuwa na mapenzi ya dhati, lakini hawawezi kukupa nafasi ya kuchezea mwili wake kabla ya ndoa hawa watu wapo na tunaishi nao kwenye jamii. Sasa inapotokea eti mwanaume umekutana na mwanamke mkaanzisha mahusiano baada ya siku moja, mbili, tatu au wiki mwanamke huyo anaanza mizinga isiyokuwa na kichwa wala miguu eti wenyewe wanaita ndio kipimo... Aisee mimi naona hakuna kipimo wala nini hizo ni njaa tu tena wakati mwingine unakutana na mwanamke smart, lakini unashangaa anakuomba vitu visivyoeleweka eti kipimo... Kipimo!?
 
Hebu tuangalie upande wa pili wa shilingi Kirikou Wa Kwanza. Kwa nini mwanamke anaomba, inawezekana umemjengea kwamba uko vizuri kipesa, na umeshaanza kumpa viahadi vya kumsaidia ili kumvuta wakati huna lolote la zaidi. Wakati mwingine wanaume muwe wakweli, unavyotaka kujionyesha una hali ambayo huna inaweza kukugharimu.... muachage kujitutumua..... hiyo ni moja ya sababu
 
Nimefanya utafit mdogo tu humu nimegundua wanaume mnalalamika sana kuhusu wanawake kuwaomba pesa, kuwapiga mizinga, kutotosheka na mnachowapa na mengine kibao. Jamani eee hebu acheni kulalamika kwa kuwa hayo mmeyataka wenyewe. Unatafuta mwanamke ili uwe unamwaga grisi chafu hapo na unataka akuhurumie asikuombe chochote! Haiwezekani hata kidogo. Wewe kama unajiona unahitaji mwanamke kwa nini huoi? kwa nini usimchukuwe jumla? muweke ndani maisha yaendeleee....Lakini hii biashara ya malalamiko yasiyo ya msingi humu tumeichoka! Acha wawapige mizinga hadi mtie akili na kutafuta ufumbuzi ambao ni wa kubeba jumla. Hamjifunzi wa baba zenu? hamuoni wametulia na mama zenu?

Tofauti na hivyo mtaishia kulishwa malimbwata, kudharauliwa, kupoteza muda kuwaza maumivu ya kutendwa badala ya kuwaza na kupanga maisha. Ukweli ni kwamba simhurumii hata kidogo mwanamume anayepigwa mizinga! Pigweni tuuuuuuu.... good day kwa wapigwa mizinga wote
Dada umemwaga povu kama umemeza cd ya mchiriku.

Anyway yes tutaendelea kulalama huku tukifundishana mbinu mpya za kuziba vijiwe vyenu.
Kuna baadhi ya dada zetu mmezidi, si wanaume wote wanakuja kwa tamaa... wengine wana malengo kabisa lakin baadhi yenu cha kwanza njaa njaa njaa..

Unajua hata kama unashida jaribu ku behave basi. Mwambie mwenzio kistaarabu.. sio unapiga baruti kama mfanyakazi wa TRA..
Kabla ya kuja kwako ulikuwa unaishije?

Real man Tutaendelea kuwaonya mpaka mtakapo kaa sawa maana kuna wenzenu hawana hizo tabia.. ila nyie ma slay queens ndio mnajiona wa hali ya juu.

Na wanaume wanaotoa pesa hovyo nao tutaendelea kuwapa somo mpaka wakae sawa. Sio unatoa toa hela kwa midemu ambayo haisomeki.
 
Nimecheka tu... maana si kwa mchiriku huu Detective J ... nimekuelewa bana illla ukweli unabaki pale pale. Unajiona unataka burudani tafuta mke, nje ya mke mizinga haikwepeki.
 
Mwanamke anayekuona uko serious wala hawezi kukuomba pesa leo leo, ila akikuona ni mtaka vya bure anaamua kukukimbiza kwa kukuomba pesa, anajua tu utakimbia na makelele kibaoo ... marioo wanapata tabu sana.... hakuna kubebwa ovyo.... mtajie pesa mbiiiooooo
Una concept but hii haifanyi kazi kwa wanawake wote. baadhi ya wanawake hata ukiwa na malengo na umeonyesha dhahiri bado watapiga vibomu.

Ni hivi nimeshawa kuwa na mwanamke, nikampeleka hadi nyumbani . mwanzoni alikuwa powa tu.. lakin baada ya kumtambulisha vibomu vikaanza.. vocha mm, chakula mimi, ada mimi( alikuwa anasoma), hela ya weekend mimi.

By then sijatoa mahar hapo. Na nilimuonya lakini akakataa kujirekebisha.
Nikampiga disco kwenye matokeo maana alishindwa mitihani yangu.
 
Ukitaka kumkimbiza mwanamume mpenda vya bure muombe pesa. Utakapoona unaombwa pesa at the beginning ujue unatishiwa nyau ili ukimbie...ukitoa zinaliwa na zinaombwa nyingine. Muonyeshe mwanamke kama uko serious hatakuomba pesa, na akikuomba jiamini kumwambia mapenzi/mahusiano si kuombana pesa, atakuheshimu na kukuangalia kwa upya kwamba uko serious.
Nilimpenda dada mmoja hivi nikawa naye miezi mitatu tukikutana nae ni story tu .sasa siku hiyo akaniambia Unajua mimi nakupenda sana wangu. unajua anenipenda mama yangu mzazi tu, akanyamaza tulipoachana akanitumia sms ya kuomba 20k nikamwambia wangu sasa hivi sina vumilia kidogo akanitumia sms achana na mimi kwanza wewe ni mwanaume suruali [emoji56][emoji56][emoji56]
 
Back
Top Bottom