Wanaume mnaocheza vikoba mnatia aibu

Wanaume mnaocheza vikoba mnatia aibu

Upatu ndio vikoba au ina tofauti mbona hamtueleweshi vizuri
Sisi tuko watu 10 na kila mmoja anatoa 6m kwa mwezii na baada ya miezi kumi kila mmoja anakuwa amechukua zake x 10
Sasa kama ni aibu basi na iwe tu 😄
Kama vikoba ina tofauti tuelimishane
Upatu ndio mnaocheza mnakuwa mnapeana pesa Kwa kiwango sawa mnapanga muda kama ni wiki au mwezi anapewa mtu pesa

Vicoba ni kama bank jamii yenyew wanaweka hisa/amana Kwa wiki au mwezi inategemea mnavokubaliana Kwa muda mliyokubaliana pia lakin Huwa wanakopeshana Kwa riba na kunawengine hawana riba pia na mara nying humalizwa baada ya mwaka au miak miwili na washiriki Huwa wengi pia
 
Hebu elezea vizur mkuu ni mnazikusanya halaf mnakopeshana? Maana ukisema mnakua mnachangiana ni mzunguko wa mwezi had mwezi sasa hela yakufanyia kitu haraka inakuaje hapo au mfano mpo sita na wewe ni wa sita si unasubiri hadi ufikiwe? sasa kusubiri ufikiwe si ungezitunza mwenyewe tu kwa nidham. Kuliko risk za huko maana wabongo tunajuana, Au mimi naelewaje?
Mi nafikir hii inasaidia Kwa wenye malengo ya muda mrefu na wanahitaji pesa nying
Kunamtu ana kipato Cha million Kwa mwez lakin kusave laki 5 ni changamoto ndo Huwa wanatumia njia hii
 
Huwa mnaliwa sana sababu ya vikoba mi mke wangu nilimwambia nikisia vikoba nakunyonga


Mpaka sasa mwaka 12 huu sijamuona

Wanaliwa sana kupata hela ya marejesho
Juzi sista angu kataitiwa laki 5 na ushee rejesho bora akaniambia kaka ake nikaclear vipi angewafata wahuni

Sent using Jamii Forums mobile app
Kiukweli km mtu haupo makini hali ni ngumu hasa kipind Cha marejesho na wengine ndoa zinavunjika kabisa vikoba nafikir vinawafaa walio na kazi au biashara na vinawasaidia
 
Huwa mnaliwa sana sababu ya vikoba mi mke wangu nilimwambia nikisia vikoba nakunyonga


Mpaka sasa mwaka 12 huu sijamuona

Wanaliwa sana kupata hela ya marejesho
Juzi sista angu kataitiwa laki 5 na ushee rejesho bora akaniambia kaka ake nikaclear vipi angewafata wahuni

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwahiyo angekopa CRDB wangemsamehe deni?

Umalaya ni hulka ya mtu, aina uhusiano na Vicoba.
 
Back
Top Bottom