Wanaume mnaokasirika kasirika humu, mnaishije na wake zenu?

Mimi nataka kukaa na wewe walau mwezi mmoja tu ili unisaidie kupona kabisa hili tatizo. Kama umeolewa, hebu fanya umdanganye Mr umepata mualiko wa kwenda kutangaza neno Wilayani Lushoto Mkoani Tanga. Najua atakuamini tu
 
Sijui shida ni nini? Anaweza kuignore watu wote akapambana na wewe kiulaloulalo mpaka unajiuliza au ananijua🤔

Shida ni afya ya akili. Mental health disorders. Mtu anataka muanze kutambiana JF, ambako hamjuani. Hata ukimwambia uhalisia wako hawezi kubali. Mtu analeta hoja, ukim prove wrong anakutukana matusi ya nguoni. 😁
 
Unafikiri kwanini hali imebadilika?

Ni kizazi, JF ina vizazi kama vitano hivi. 2006, 2010, 2015, 2020,2026. JF ilishavamiwa hii. Ni kwenda nayo hivyo hivyo.
Imagine, mtu anakufuta inbox kwa lengo tuu la kuja kukuprovoke, kukutukana na kujimwambafy, wakati hapa tunatumia majina bandia. 😁
Mtu anajifanya kukujua na huku unatumia jina bandia. 😁
 
Wanawake wana maneno ambayo hata kama ulikuwa hautaki kuongea utalazimishwa kuongea.

Ebu fikiria Khamis aliyemchoma mkewe kwa magunia mawili ya mkaa jinsi alivyoreact baada ya kupewa jibu la kuudhi.

Khamis: Mbona umechelewa kurudi nyumbani ulikuwa kwa wanaume?

Mkewe:Kama nilikuwa kwa mwanamme na wewe nenda kwa mwanamme ukabanduliwe.
(Hapa mwanammke angesema na wewe nenda kwa mwanamke wako ukambandue khamis asingekasirika)
 
Shemasi wa zamu unataka tukuoe ili ujue uhalisia wetu?
 
Shida ni afya ya akili. Mental health disorders. Mtu anataka muanze kutambiana JF, ambako hamjuani. Hata ukimwambia uhalisia wako hawezi kubali. Mtu analeta hoja, ukim prove wrong anakutukana matusi ya nguoni. 😁
Tunaishi na vichaa mitandaoni naona! Namimi sijui kumpooza mjinga, akija kama punguwani naenda naye sambamba kama alivyokuja! Akipoa namimi napoaa!🤗
 
Wa umu mnachangia mada kana kwamba ninyi mnaweza kila jambo lakini hamkumbuki mwanaume ni mwanaume tu
Ukiwa mwanaume ndio ukose hekima? Punguzeni hasira mnapoingia humu ili tuelewane!
 
Usiogope mwanamke au wanaume anayekasirika ogopa ambaye hakasiriki

"Mtu shupavu sio yule ambaye hakasiriki ila akikasirika hafanyi jambo lolote baya"

Mwisho wa kunukuu
 
Tunaishi na vichaa mitandaoni naona! Namimi sijui kumpooza mjinga, akija kama punguwani naenda naye sambamba kama alivyokuja! Akipoa namimi napoaa!🤗

Mimi nampuuza tuu. Nipo hapa JF kuburudika na kuhabarika. Mtu hakujui, humjui, hajui wewe ni nani, anawezaje kukuumiza kichwa!
JF ndio sehemu pekee tunabishana na mental health patients.
Hapa JF, ndipo unaweza bishana na mtu kuhusu utajiri ilihali hana hata godoro!
JF mtu anaweza kukutambia ana utajiri, kampuni baada ya wiki akaanzisha uzi anaomba kazi! 😁
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…