Wanaume mnaokasirika kasirika humu, mnaishije na wake zenu?

Sijamaliza kusoma lakini nimeelewa. Ni hivi, maisha ya jf ni tofauti sana na maisha na mke wako. Jf kila mtu ni tajiri usafir n ndege. Asilimia kubwa tunamiliki magari majumba biashara kubwa kubwa kwa iyo jf hatupangwingwi coz we are the bosses na kikubwa zaid wote tunajiweza bed seven inch zetu tunaringa kulinga. Na kuhusu maisha ya na wake zetu hiyo ni siri ya ndan na sio siri kuna watu humu wanachapwa na wake zao hadi kulala chini wanalala bt wakiwa humu jf room wao ni vidume. Sijataja mtu. Let me finish my breakfast ya konyagi na mkate nakuja.
Mkuu umeacha nimecheka vibaya sana aise
 
JF inatumika vibaya na watu wajinga, ukionyesha hisia za kupenda, kutaka kusaidia, kuhurumia basi manipulators, swindlers, conmen and scammers emerges, wanachukua advantage hiyo kukutapeli, iwe ni hela, mapenzi, biashara n.k
Mimi kuna mtu mmoja around 2015, alileta uzi kwamba ana shida ya usikivu (Healing loss), kibinadamu nikamhurumia, nikamuomba anipe namba, nikamchangia nauli na kumuhaidi kumsaidia afike mjini akutane na Specialist wa masikio, just to know exactly what was behind his ears. Kweli yule mtu nilimtumia nauli, fedha ya malazi na nikafanya appointment na mshikaji wangu yupo hapo Muhimbili. Japo fedha ilikuwa kidogo tuu lakini baada ya kuituma, alinambia tuu ameipata na baada ya hapo hakukuwa na mawasiliano. Simu ile haikupatikana tena, na mshikaji wangu akaniuliza one day tunacheki boli, yule mgonjwa wetu vipi?.
Nikakosa jibu, nikamwambia stori nzima, akanambia niwe makini sana na hisia zangu. Don't show love, love will get you killed. 😁
Aisee yule jamaa namkumbuka sana hata mimi na ID yangu nyingine niliaanza kuingia kingi nikaanza kusakanya washkaji wako nje wanitafutie hata used hearing aid nimpatie, kwa vile msaada wangu haukuwa fedha bali ni kifaa moja kwa moja nikaanza kuona kama anipotezea, nikaona ahaaa kumbe kuna kitu unataka zaidi ya msaada wa kweli nikapotezea
 
Off course, jamaa hakuwa anamaanisha kupata msaada, na wenda kweli tatizo analo.
 
Wanaume, mpo? Nawauliza kwa upole kabisa, lakini kwa uzito wa moyo: Hivi nyie mnaokasirika kasirika hapa JF, mnaishije na wake zenu majumbani?

Naongea na wewe mwanaume, ambaye kila unapoandika mada, unapojibu maswali, unapochangia hoja, maneno yako hayakosi ukali, kejeli, hasira na wakati mwingine hata matusi. Sasa najiuliza, kama unaongea maneno ya namna hiyo mbele ya watu usiowaona humu, je ukiwa mbele ya mke wako hali ikoje?

Mke wako akipika chakula akakitia chumvi zaidi, kunakuwa na amani nyumbani au mvua ya maneno makali ndo inaanza kunyesha? Je, akichoka na kukosa nguvu, na siku hiyo akashindwa kukupa haki yako ya ndoa, unamwelewa kweli, au ndo hasira zinapopanda kama moto?

Hasira isiyodhibitiwa haijengi, inabomoa. Haiponyi, inaumiza. Na mara nyingi, huanza kidogo tu, lakini huishia kuvunja ndoa, kuharibu watoto, na kuondoa amani kabisa nyumbani.

Mwanaume uliumbwa kuwa kiongozi wa nyumba, lakini sio kwa kelele wala ukali, bali kwa hekima, upendo, na uvumilivu. Ukali sio uanaume. Matusi sio mamlaka. Hasira sio nguvu.

Kuna roho ya hasira ambayo imewakamata baadhi yenu wanaume. Hii roho inawasukuma kusema maneno ambayo hata mioyo yenu haikusudii kuyasema. Inawafanya muonekane wakali hata pale ambapo hapahitaji ukali.

Hasira ya mara kwa mara sio tu inaharibu mahusiano, bali pia inapunguza siku zako za kuishi. Moyo unachoka, mwili unachoka, akili inachoka. Unajiumiza mwenyewe bila kujua.

Leo nakutia moyo, wewe unayesumbuliwa na hali hiyo, inaweza kukutoka!

Yesu Kristo anaweza kukupumzisha. Anaweza kukutoa katika minyororo ya hasira. Anaweza kukupa moyo mpya wa upole, subira na unyenyekevu.

Njoo kwa Yesu sasa kwa imani, mwambie ukweli katika sala hii fupi. Omba hivi:

“Ee Mungu, nina tatizo la hasira, niondolee hali hii, niokoe, nifanye upya, katika Jina la Yesu, amen.”

Ukiomba hivyo kwa dhati, hakika Yesu hatakuacha, atakusaidia kuwa mpole na mwenye kiasi.

Mungu aibariki ndoa yako, na nyumba yako idumu kuwa mahali panapotiririka maziwa na asali.

Amen!
Simple tuu tunaweka ukuta hakuna Maziwa na mwanamke ni mwendo wa amri na it works.

Kwa observations zangu wale wanaojifanyaga kucheka Cheka na wake zao ndio ndoa zao Zina shida kweli kweli na wanaachana tofauti na Alfa male wanaotoa amri tuu.

Zamani baba alikuwa na boma lake wanawake wanaenda kwake Kwa zamu ya kuliwa tuu hakuna Maziwa na mwanamke.
 
Wanaume, mpo? Nawauliza kwa upole kabisa, lakini kwa uzito wa moyo: Hivi nyie mnaokasirika kasirika hapa JF, mnaishije na wake zenu majumbani?

Naongea na wewe mwanaume, ambaye kila unapoandika mada, unapojibu maswali, unapochangia hoja, maneno yako hayakosi ukali, kejeli, hasira na wakati mwingine hata matusi. Sasa najiuliza, kama unaongea maneno ya namna hiyo mbele ya watu usiowaona humu, je ukiwa mbele ya mke wako hali ikoje?

Mke wako akipika chakula akakitia chumvi zaidi, kunakuwa na amani nyumbani au mvua ya maneno makali ndo inaanza kunyesha? Je, akichoka na kukosa nguvu, na siku hiyo akashindwa kukupa haki yako ya ndoa, unamwelewa kweli, au ndo hasira zinapopanda kama moto?

Hasira isiyodhibitiwa haijengi, inabomoa. Haiponyi, inaumiza. Na mara nyingi, huanza kidogo tu, lakini huishia kuvunja ndoa, kuharibu watoto, na kuondoa amani kabisa nyumbani.

Mwanaume uliumbwa kuwa kiongozi wa nyumba, lakini sio kwa kelele wala ukali, bali kwa hekima, upendo, na uvumilivu. Ukali sio uanaume. Matusi sio mamlaka. Hasira sio nguvu.

Kuna roho ya hasira ambayo imewakamata baadhi yenu wanaume. Hii roho inawasukuma kusema maneno ambayo hata mioyo yenu haikusudii kuyasema. Inawafanya muonekane wakali hata pale ambapo hapahitaji ukali.

Hasira ya mara kwa mara sio tu inaharibu mahusiano, bali pia inapunguza siku zako za kuishi. Moyo unachoka, mwili unachoka, akili inachoka. Unajiumiza mwenyewe bila kujua.

Leo nakutia moyo, wewe unayesumbuliwa na hali hiyo, inaweza kukutoka!

Yesu Kristo anaweza kukupumzisha. Anaweza kukutoa katika minyororo ya hasira. Anaweza kukupa moyo mpya wa upole, subira na unyenyekevu.

Njoo kwa Yesu sasa kwa imani, mwambie ukweli katika sala hii fupi. Omba hivi:

“Ee Mungu, nina tatizo la hasira, niondolee hali hii, niokoe, nifanye upya, katika Jina la Yesu, amen.”

Ukiomba hivyo kwa dhati, hakika Yesu hatakuacha, atakusaidia kuwa mpole na mwenye kiasi.

Mungu aibariki ndoa yako, na nyumba yako idumu kuwa mahali panapotiririka maziwa na asali.

Amen!
Ni kosa kubwa sana kufananisha real life scenario na maisha ya mitandaoni.. Its almost childish and stupid.
 
Mtu hunena yale yaliyoujaza moyo wake. Moyo wako ukijaa hasira na matusi, utayatoa tu kwa njia ya kinywa chako au kwa maandishi (Lk 6:45). That’s a no-brainer

Kwa maana kutoka ndani ya moyo wa mtu hutoka mawazo mabaya, uasherati, wizi, uuaji, uzinzi, tamaa mbaya, uovu, udanganyifu, ufisadi, wivu, matukano, kiburi na upumbavu. Maovu haya yote hutoka ndani ya mtu, nayo ndiyo yamtiayo mtu unajisi (Mk 7:20-23)
 
Utaigiza kila siku? Ipo siku tu uvumilivu utakushinda utajianika wazi wazi..
Tukiwa tunahitaji jambo letu kuigiza lazima unapakwa asali kisha unasukumiziwa nyuki wenyewe wakukute na ushahidi
 
Mtu hunena yale yaliyoujaza moyo wake. Moyo wako ukijaa hasira na matusi, utayatoa tu kwa njia ya kinywa chako au kwa maandishi (Lk 6:45). That’s a no-brainer

Kwa maana kutoka ndani ya moyo wa mtu hutoka mawazo mabaya, uasherati, wizi, uuaji, uzinzi, tamaa mbaya, uovu, udanganyifu, ufisadi, wivu, matukano, kiburi na upumbavu. Maovu haya yote hutoka ndani ya mtu, nayo ndiyo yamtiayo mtu unajisi (Mk 7:20-23)
Duuuuh.. sasa mbona moyo wangu unachemba nne na damu top. Vikinitoka hivo vitu patatosha kweli madam??
 
Biblia inaposema moyo, haimaanishi moyo unaosukuma damu, bali nia, mawazo au maisha ya ndani ya mtu. Kwahiyo, kama ndani ya mtu kuna mema, yatatoka mema; kama ndani kuna mabaya, yatadhihirika tu.
 
Kua makini na hiko kitabu, usije ukachanganyikiwa. Hivi unaelewa unachoniambia hapo???
 
Mimi nampuuza tuu. Nipo hapa JF kuburudika na kuhabarika. Mtu hakujui, humjui, hajui wewe ni nani, anawezaje kukuumiza kichwa!
JF ndio sehemu pekee tunabishana na mental health patients.
Hapa JF, ndipo unaweza bishana na mtu kuhusu utajiri ilihali hana hata godoro!
JF mtu anaweza kukutambia ana utajiri, kampuni baada ya wiki akaanzisha uzi anaomba kazi! 😁
Hili ninaushuhuda nalo, mwaka 2023 Kuna id ilikua inaswampa kwenye Uzi wa kimasikhara inapiga porojo halafu inaenda kumalizia Uzi wa usiku wa manane, Sasa kuna siku naona wameshikana maneno na I'd nyingine japo alikua sahihi ila alitoa Lugha kali na maudhi anajikweza kwa sifa za uofisa wa jeshi🤣🤣
Hamadi namkuta Uzi wa ajira za polisi anauliza ronja🤣🤣🤣, anajielezea jinsi anahangaika ameanza kutafuta nafasi ya ajira tangu mwaka 2021.
Nikamfata PM Uzuri akawa mnyenyekevu kila nikimchamba anajibu kama Padri. 🤣🤣🤣 Mungu alikua upande wake, nikageuka tena kuwa jiwe la pembeni, kuna sehemu nikamuelekeza akapige hodi na kulia sana, nikiwa na mimi nachochea 🤣🤣 Akabahatika, Sasa hivi hana makasiriko kiranja wa matumaini. Kawa Mfano wangu kama anonymous.
 
Mungu wako mwenyewe ana gubu anakasirika hovyo kiasi kwamba kaharibu maisha ya viumbe wengi ikiwepo wasio na hatia.

Tunajifunza kutoka kwake ondoa hofu
 
Ukiwa mkali Mwanamke anakuona humfai ukiwa mpole pia anaona humfai, wanaume tusikubali kuwa kama Samson kwa Dalila watatuuwa huku tunajiona.
 
Kua makini na hiko kitabu, usije ukachanganyikiwa. Hivi unaelewa unachoniambia hapo???
Achana na uongo wa shetani eti ukisoma Biblia utachanganyikiwa. Biblia ni kitabu kinachofunua siri ya uzima wa milele, ndio sababu shetani anajaribu kuwashawishi watu wasikisome ili siku ya mwisho waangamie kama yeye. Mpinge shetani aache kukupotosha.
 
Back
Top Bottom