Wacha nijisimulie,
Angalizo, nilifeli kufupisha habari.
Safari moja wakati hizi marathon ndo zinaanza ikiongozwa na Kilimarathon, bosi wangu alikuwa anachangia na akawa anapewa nafasi kadhaa watu anaotaka washiriki, so safari moja itakotea Zanzibar marathon, sikuwa na mwili wa athletic [emoji1], ila wa kinyamwezi zaidi nikachukua nafasi moja wapo anazopewa boss nikaenda Zanzibar. Ila mahala pa kulala, usafiri na chakula unajitegemea.
Huyo nikachukua kit yangu, boti la jioni hadi Zanzibar nikachukua chumba maeneo ya stone town maana kulikuwa kumejaa wadau. Huku na kule usiku nikaenda forodhani aiseeeh wadau kama wote wanapena vituo tuu vya kuhama, hasa wanaume walikuwa wanasema ukikesha halafu asubuhi yake unakimbia ukishapewa medali yako unaenda kuzimua na mzinga mmoja na supu halafu unaingia kwenye usafiri wa kurudi nyumbani unalala kama roba la kuli.
Basi nikakutana na wadau niliosoma nao chuo, watu wanajikipu figa utasema wanamiaka 20 kumbe 50+...1[emoji39][emoji39][emoji39]
So ilikuwa marathon yangu ya kwanza kushiriki na ya mwisho. Nikavutiwa na amsha amsha, nikaunga tela ila nikawapa angalizo asubuhi nikishindwa kukimbia kutokana na uchovu wa kutokulala usikukucha na usingizi ntachukua medali ya mmoja wenu.
Mmoja akaniambia Kasie usijali hapa kama unavyotuona hatupoi, hatulali, tuko na kibasi chetu saa kumi tunarudi vyumbani kuoga na kuvaa nguo za kukimbilia kisha mchakamchaka unaanza. Shurti kilomita 10 ziishe.....[emoji12][emoji12]
Tukaanza kuhama viwanja, zanzibar siku hiyo watu hawakulala hadi saa kumi hii hapa, tukarudi vyumbani nikasikitika tuu nimelipia chumba cha bure halafu sijakilalia.
Baada ya kuoga kidogo nijitupe kitandani nilale, qakati nakitizama kitanda saa 11 alfajiri nasikia nagongewa mlango, Kasie kibasi kinakusubiri wewe tuu huyo nikatoka mchaka mchaka ukaanza na spika ya miziki ya amsha amsha hadi uwanja wa kuanza mbio.
Tulipopigiwa kipenga cha kuanza mbio za kilomita 10 hao tukaanza mdogodogo aiseeh usingizi wote ulikata. Sijui kuna maajabu gani ila tunakimbia wote kwa pace moja na hatuachani lengo wote tumalize mbio kiongozi wetu anatuhamasa tumekesha wote medali tutachukua wote ila kila mtu atarudi kwake mwenyewe [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Baada ya kupokea medali, maana kilomita 10 ziliisha nilikuwa na furaha tukaamsha tena mchakamchaka hadi eneo la kunywa supu, wakati nakunywa supu mmoja wa wale wadau akaniambia Kasie marathon ina mambo mengi sana, ukijiingiza humo na huwezi kuhimili unapotea.
Hii njia sisi tunatumia ya kibasi inatulipa sana hatulali na mademu maana kwenye hizi marathon mitego mingi wengine wameungua, mimba zisizotarajiwa zinatungwa magonjwa ya zinaa na kadha wa kadha.
Sasa sisi wazee wenzako tunajiepusha na hayo kwa style ya kutokulala, wanawake wanaotufata wataishia kununuliwa pombe tena kidogo maana hata sisi hatunywi sana ili tuweze kukimbia asubuhi. Ila wanawake wapo wanaojiuza, wapo mashoga wanatafuta mabwana, wako kila aina ya sampuli, akili mukichwa.
Ila marathon ina ulevi na starehe flani ukiuanza huachi hadi uchoke mwenyewe.
So nilirudi na bothya saa sita mchana na kibasi changu kwenye boti tena hatukulala amsha amsha kama zote za vurugu za marathon, yule mdau akaniambia, namna hii unapata wapi muda wa kutongoza demu na kulala nae. Kibasi hakipoiiii tunajiandaa na marathon nyingine Morogoro ya trailer nini nini sijui huko, nashukuru nikarudi nyumbani salama.
Kila mtu na mtazamo wake na namna anachukulia mambo, mabaya yapo na mazuri ya jambo yapo vilevile.
Akili mukichwa.
Kasie Matata.