Nashindwa kukielezea hapa, naomba mtu anayekimbia sana marathon na amekutana na hii style ya kibasi amueleweshe mdau tafadhali.
Ila ngoja nijaribu, ni kikundi cha wakimbiaji ambao wanakimbia pamoja kwa pace moja hawaachani, wanaanza pamoja wanamaliza pamoja. Maranyingi hawa wanafanyaga mazoezi pia pamoja ili kuhimilibpace yao. Huwa wanaimba huku wanakimbia au wanakuwa na kispika wanaweka miziki mbalimbali kupoteza uchovu.
Kinaitwa kibasi sababu wote mnaanza kituo kimoja mnashuka kituo kimoja pamoja, yaani mwanzo wa mbio hafi mwisho wa mbio.
Hawana lengo la kuwa mshindi wa kwanza au wa pili au watatu wao ni kukimbia na kufurahia mbio kama sehemu ya starehe aka starehe inayoumiza ila unaipotezea kama huumii vile...[emoji28][emoji28][emoji28]
Mfano ni kikundi cha vijana wanaofanyaga mazoezi ya kukimbia huku wamevaa jezi zenye nembo ya Wasafi.
That way...[emoji6]
Short story made long...[emoji2356][emoji2356][emoji849]