Wanaume msiotaka kuoa na wanawake msiotaka kuolewa mkizeeka mtalelewa na nani?

Wanaume msiotaka kuoa na wanawake msiotaka kuolewa mkizeeka mtalelewa na nani?

Waliofiwa na wenza wao je wakizeeka watalelewa na nani?. Waliopeana talaka je?.Hiyo imani kwamba ukioa/kuolewa na kupata watoto eti watakulea uzeeni kwako ni matumaini tu. Kuna watu wana wake/waume na watoto na bado wakizeeka hawana wa kuwalea wapo kwenye vituo vya wazee mfano kile cha Msimbazi Centre wanalelewa na masista. Kuna ambao walikua nao lakini kifo kimewachukua wanaenda kulelewa na watu baki.
 
Ukioa au kuolewa lazima mmoja wapo.atatangulia mbele ya haki je aliye baki ulelewa na nani ? Wanandoa maelfu wamesha wapoteza wenza wao na awawezi kuoa tena au kuolewa ...hivyo logic ya mleta uzi ni MAVI YA BATA
Analelewa na watoto
 
Akili za kimaskini always zinawaza ujinga ujinga😄😄😄

Nasemaje,,,,,

📌KATAAA NDOA,LINDA UHURU WAKO..!!

SABABU ZANGU ZA KUPINGA DHANA YA KULELEWA BAADA YA KUZEEKA AU WAKATI WA MAGONJWA:

1.HAKUNA UHAKIKA WA KUWA UTAKAYEKUWA NAYE KWENYE NDOA ATAKUWA NA WEWE MPAKA UZEE WAKO.

2.UKIWA NA PESA UMEMALIZA MATATIZO.STOP PEDESTRIALIZING PEPOLE.ISHI MAISHA YAKO.NO BODY GIVES A DAMN ABOUT YOU.KILA MTU ANAWAZA JINSI YA KUKUTUMIA KWA FAIDA ZAKE.

3.TAFUTA HELA,,,,TAFUTA MALI HIYO NDO AMANA YAKO!!!!SIO WATOTO SIO MKE WALA NDUGU,,,,PESA NA MALI NDIO AMANA YAKO!!!!?
 
Wadau wa JamiiForums,

Naomba tujadili swali hili kwa uwazi na hoja za msingi.

Katika jamii yetu ya sasa, kumekuwa na ongezeko la wanaume wanaosema hawana mpango wa kuoa na wanawake wanaosema hawana mpango wa kuolewa. Kila mmoja ana sababu zake, na bila shaka kila mtu ana haki ya kuamua namna anavyotaka kuishi maisha yake.

Lakini kuna jambo moja ambalo ningependa tulitafakari kwa pamoja: Ujana una mwisho, nguvu za mwili hupungua, na uzee ni hatua ambayo wengi wetu tunaweza kuifikia.

Leo unaweza kuwa na kazi nzuri, biashara, fedha, marafiki na uwezo wa kujihudumia bila kumtegemea mtu yeyote. Lakini je, umefikiria maisha yako yatakuwaje utakapofikisha miaka 70, 80 au 90, hasa pale afya itakapokuwa imeanza kudhoofika?

Najua kuoa au kuolewa siyo dhamana ya kupata mtu wa kukutunza uzeeni. Wapo walio kwenye ndoa lakini wanaishi maisha ya upweke, na wapo wenye watoto ambao hawapati msaada wowote kutoka kwao.

Hata hivyo, kwa wale ambao mmeamua kwa hiari yenu kutokuoa au kutokuolewa, ningependa kufahamu mipango yenu ya maisha ya uzeeni.

Je, mnategemea ndugu, wapwa, marafiki, nyumba za kulelea wazee, au mmejiandaa kifedha kuajiri watu watakaowahudumia?

Na je, ikitokea mmezeeka, mmeugua na hamna uwezo tena wa kujihudumia, nani atakayekuwa karibu kuhakikisha mnapata matunzo yanayostahili?

Lengo langu siyo kupinga maamuzi ya mtu ya kutokuoa au kutokuolewa, bali kuelewa namna watu wanaochagua maisha hayo wanavyojiandaa kukabiliana na changamoto za uzee.

Swali langu kuu ni hili: Wanaume msiotaka kuoa na wanawake msiotaka kuolewa, mkizeeka mtalelewa na nani?

Karibuni kwa mjadala wenye hoja na kuheshimiana. Ningependa zaidi kusikia majibu kutoka kwa watu ambao tayari wameamua kutokuingia kwenye ndoa.
Hoja zako nyepesi sana..kwani kukosa kuoa au kuolewa kunakufanya usizae?
 
Kuna mzee mmoja alifariki Aghakhan alikaa pale zaidi ya mwaka hakuna hata mtoto mmoja alikuja wala mke wake wote walikuwa wanaishi Marekani. Walikuja siku ya kuzika baada ya kama siku 3 wakageuza. Mgawanyo wa mali zake robo tatu ikiwemo flat aliyokuwa akiishi Upanga walipewa nurse, dada wa kazi, dereva na baadhi ya wasaidizi wake.

Somo kubwa nililolipata kwake kwa mwanaume siku zote una vitu viwili tu vitasimama na wewe mpaka kaburini Mungu na pesa yako nje ya hapo jiandae kwa mvunjiko mkubwa sana wa moyo. Silaha ya mwanaume ni Mungu na pesa yake hivyo vingine ni ziada tu. Tekeleza wajibu wako ila usijisahau siku za giza.
Mungu alimsaidiaje huyo mzee?
 
Alafu nyie vichogo mkikaa mnawaza tu kutushawishi tujiunge kwenye hilo kundi lenu la wagonjwa wa akili...

Pambaneni na njia mlioichagua ya kuishi maisha ya kuwaridhisha wanajamii ili tu MFIT IN.

📌KATAA NDOA,LINDA AFYA YAKO YA AKILI!

#KENGE WAHED,,,GADDEMIT!!!!

#YBWYB!!!
 
Baada ya kusoma uzi huu mwanaume rudi kijijini kwenu akaoe na mwanamke tafuta mme uolewe. Dunia haina huruma.
Dunia kutokuwa na huruma hakuna uhusiano na kuoa wala kuolewa.

Duniani hapa kila kitu ni pesa.

Ukishakuwa na pesa, huwezi kosa huduma.

Baada ya mke wa Reginald Mengi kufariki, Mzee Mengi alivuta pisi mpya Jackline ikawa inamtunza sababu ya pesa.

Ukiwa na pesa huwezi kosa wa kukutunza.
 
Mungu alimsaidiaje huyo mzee?
Nimeiweka ktk perspective ya mtu anayeamini hivyo. Huyo Mzee nilikuwa karibu naye niliona mpaka dakika mwisho alikuwa anaomba Mungu wake.
 
Mimi binafsi najiandaa endapo nitafanikiwa kufika umri huo wa kuhitaji msaada niwe na uwezo wa kulipa mtu wa kunipa huduma hiyo ama kulipia kuishi kwenye nyumba za wazee (naamini miaka hiyo nikifika hicho kitu kitakuwa kawaida sana hapa bongo)
 
Nimepitia changamoto za kulazwa hospitali hivi karibuni na ni ka practice jinsi pesa inaweza nisaidia bila kuhitaji msaada wa mtu yeyote, nimelazwa na nimepata huduma zote za msingi pasipo msaada hata wa ndugu
 
Kati ya ELIMU NA PESA CHAGUA PESA BALI KATI YA AKILI NA PESA CHAGUA AKILI ..... mwenye pesa ni zaidi ya mwenye wake au waume wengi.
 
Wadau wa JamiiForums,

Naomba tujadili swali hili kwa uwazi na hoja za msingi.

Katika jamii yetu ya sasa, kumekuwa na ongezeko la wanaume wanaosema hawana mpango wa kuoa na wanawake wanaosema hawana mpango wa kuolewa. Kila mmoja ana sababu zake, na bila shaka kila mtu ana haki ya kuamua namna anavyotaka kuishi maisha yake.

Lakini kuna jambo moja ambalo ningependa tulitafakari kwa pamoja: Ujana una mwisho, nguvu za mwili hupungua, na uzee ni hatua ambayo wengi wetu tunaweza kuifikia.

Leo unaweza kuwa na kazi nzuri, biashara, fedha, marafiki na uwezo wa kujihudumia bila kumtegemea mtu yeyote. Lakini je, umefikiria maisha yako yatakuwaje utakapofikisha miaka 70, 80 au 90, hasa pale afya itakapokuwa imeanza kudhoofika?

Najua kuoa au kuolewa siyo dhamana ya kupata mtu wa kukutunza uzeeni. Wapo walio kwenye ndoa lakini wanaishi maisha ya upweke, na wapo wenye watoto ambao hawapati msaada wowote kutoka kwao.

Hata hivyo, kwa wale ambao mmeamua kwa hiari yenu kutokuoa au kutokuolewa, ningependa kufahamu mipango yenu ya maisha ya uzeeni.

Je, mnategemea ndugu, wapwa, marafiki, nyumba za kulelea wazee, au mmejiandaa kifedha kuajiri watu watakaowahudumia?

Na je, ikitokea mmezeeka, mmeugua na hamna uwezo tena wa kujihudumia, nani atakayekuwa karibu kuhakikisha mnapata matunzo yanayostahili?

Lengo langu siyo kupinga maamuzi ya mtu ya kutokuoa au kutokuolewa, bali kuelewa namna watu wanaochagua maisha hayo wanavyojiandaa kukabiliana na changamoto za uzee.

Swali langu kuu ni hili: Wanaume msiotaka kuoa na wanawake msiotaka kuolewa, mkizeeka mtalelewa na nani?

Karibuni kwa mjadala wenye hoja na kuheshimiana. Ningependa zaidi kusikia majibu kutoka kwa watu ambao tayari wameamua kutokuingia kwenye ndoa.
Vyovyote vile tutakufa tu
 
Back
Top Bottom