Strong ladg
JF-Expert Member
- Jul 15, 2021
- 1,357
- 3,114
Analelewa na watotoUkioa au kuolewa lazima mmoja wapo.atatangulia mbele ya haki je aliye baki ulelewa na nani ? Wanandoa maelfu wamesha wapoteza wenza wao na awawezi kuoa tena au kuolewa ...hivyo logic ya mleta uzi ni MAVI YA BATA
Kama umetambua hivyo ..basi unganisha dot kuona ujinga wako ..nani kakuambia kuwa ndoa ndiyo kuwa na watoto na kutokuwa na ndoa ndiyo ugumba?Analelewa na watoto
Hoja zako nyepesi sana..kwani kukosa kuoa au kuolewa kunakufanya usizae?Wadau wa JamiiForums,
Naomba tujadili swali hili kwa uwazi na hoja za msingi.
Katika jamii yetu ya sasa, kumekuwa na ongezeko la wanaume wanaosema hawana mpango wa kuoa na wanawake wanaosema hawana mpango wa kuolewa. Kila mmoja ana sababu zake, na bila shaka kila mtu ana haki ya kuamua namna anavyotaka kuishi maisha yake.
Lakini kuna jambo moja ambalo ningependa tulitafakari kwa pamoja: Ujana una mwisho, nguvu za mwili hupungua, na uzee ni hatua ambayo wengi wetu tunaweza kuifikia.
Leo unaweza kuwa na kazi nzuri, biashara, fedha, marafiki na uwezo wa kujihudumia bila kumtegemea mtu yeyote. Lakini je, umefikiria maisha yako yatakuwaje utakapofikisha miaka 70, 80 au 90, hasa pale afya itakapokuwa imeanza kudhoofika?
Najua kuoa au kuolewa siyo dhamana ya kupata mtu wa kukutunza uzeeni. Wapo walio kwenye ndoa lakini wanaishi maisha ya upweke, na wapo wenye watoto ambao hawapati msaada wowote kutoka kwao.
Hata hivyo, kwa wale ambao mmeamua kwa hiari yenu kutokuoa au kutokuolewa, ningependa kufahamu mipango yenu ya maisha ya uzeeni.
Je, mnategemea ndugu, wapwa, marafiki, nyumba za kulelea wazee, au mmejiandaa kifedha kuajiri watu watakaowahudumia?
Na je, ikitokea mmezeeka, mmeugua na hamna uwezo tena wa kujihudumia, nani atakayekuwa karibu kuhakikisha mnapata matunzo yanayostahili?
Lengo langu siyo kupinga maamuzi ya mtu ya kutokuoa au kutokuolewa, bali kuelewa namna watu wanaochagua maisha hayo wanavyojiandaa kukabiliana na changamoto za uzee.
Swali langu kuu ni hili: Wanaume msiotaka kuoa na wanawake msiotaka kuolewa, mkizeeka mtalelewa na nani?
Karibuni kwa mjadala wenye hoja na kuheshimiana. Ningependa zaidi kusikia majibu kutoka kwa watu ambao tayari wameamua kutokuingia kwenye ndoa.
Mungu alimsaidiaje huyo mzee?Kuna mzee mmoja alifariki Aghakhan alikaa pale zaidi ya mwaka hakuna hata mtoto mmoja alikuja wala mke wake wote walikuwa wanaishi Marekani. Walikuja siku ya kuzika baada ya kama siku 3 wakageuza. Mgawanyo wa mali zake robo tatu ikiwemo flat aliyokuwa akiishi Upanga walipewa nurse, dada wa kazi, dereva na baadhi ya wasaidizi wake.
Somo kubwa nililolipata kwake kwa mwanaume siku zote una vitu viwili tu vitasimama na wewe mpaka kaburini Mungu na pesa yako nje ya hapo jiandae kwa mvunjiko mkubwa sana wa moyo. Silaha ya mwanaume ni Mungu na pesa yake hivyo vingine ni ziada tu. Tekeleza wajibu wako ila usijisahau siku za giza.
Dunia kutokuwa na huruma hakuna uhusiano na kuoa wala kuolewa.Baada ya kusoma uzi huu mwanaume rudi kijijini kwenu akaoe na mwanamke tafuta mme uolewe. Dunia haina huruma.
Nimeiweka ktk perspective ya mtu anayeamini hivyo. Huyo Mzee nilikuwa karibu naye niliona mpaka dakika mwisho alikuwa anaomba Mungu wake.Mungu alimsaidiaje huyo mzee?
Kati ya ELIMU NA PESA CHAGUA PESA BALI KATI YA AKILI NA PESA CHAGUA AKILI ..... mwenye pesa ni zaidi ya mwenye wake au waume wengi.Nimepitia changamoto za kulazwa hospitali hivi karibuni na ni ka practice jinsi pesa inaweza nisaidia bila kuhitaji msaada wa mtu yeyote, nimelazwa na nimepata huduma zote za msingi pasipo msaada hata wa ndugu
Ndo maana bichwa lako liko ndani ya dryer, unaongea huku umejaa losheni usoni.Hao kataa ndoa wacheni kuwachukulia serious ni watu wenye familia na ndoa zao kabisa !
Vyovyote vile tutakufa tuWadau wa JamiiForums,