Wanaume na wazazi wenye watoto wa kiume, hii imeshawahi kuwatokea?

Wanaume na wazazi wenye watoto wa kiume, hii imeshawahi kuwatokea?

Hiyo hali haiepukiki ila ukubwa wake unatagemeana na mizizi iliyowekwa kipindi cha utoto wao na baba yao.

Mtoto ukimchekea sana utotoni akahisi ni marafiki basi katika balehe yake lazima atakupanda kichwani akihisi mnawezana.

Mtoto hapaswi kumuogopa mzazi ila kunapaswa kuwe na uelewa kuwa japo mzazi haogopewi ila nafasi yake ya uzazi haina mjadala, kwamba anachoamua mzazi ndio cha mwisho na hakihojiwi.

Haipaswi mtoto kuwa na nafasi yeyote ya kukaidi, kuhoji ama kujibizana na mzazi as long as bado anaishi katika himaya ya mzazi na bado anategemea mzazi.

Pia watoto wanapaswa kutambua kuwa wazazi wote wawili ni kitu kimoja sio kwamba mmoja ni 'fair' na mwingine ni mkuda.
Nyumba nyingi utakuta mzazi mmoja anajifanya mwema sana hasa mama na kumrushia uhaini wote baba. Hii inajenga taswira mbaya kwa baba mbele ya watoto.

Inapaswa itambulike kwa watoto wote kuwa maamuzi ya wazazi wote ni mamoja na kuwa ikitokea hukumu/agizo/maamuzi ni la wazazi wote.
Inapaswa wazazi waepuke kubishana juu ya maamuzi ya watoto wao mbele ya watoto. Hata kama hamkubaliani kuhusu jambo, inapaswa mfanyie pembeni mabishano sio mbele ya watoto.

Kubwa na la muhimu zaidi, mtoto hatakiwi kuwa na uhuru wa kuongea ujinga wowote juu mzazi mmoja kwenda kwa mzazi mwingine pasi na uwepo wa mzazi huyo. Yani haijalishi mtoto kakerwa kiasi gani, hatakiwi kuwa na ujasiri wa kwenda kuongea shiti juu ya baba mbele ya mama na mama nae aka support.

Nguvu ya ulezi bora inapatikana kwa umoja wa wazazi wote wawili.
Sio baba anatoa hukumu/adhabu, mama anamuita mtoto pembeni na kumbembeleza.
Shukrani za dhati kwa ushauri mzuri, nimeyachukua yote.
Asante sana 🙏
 
Mtoto wangu wa kiume alivyo balehe ukaribu na mimi ukapungua akawa karibu na baba yake. Wakati alivyokua mdogo mama this mama that na a.k.a ya mtoto wa mama aliitwa.

Sasa ni busy na baba ake nyumbani akiwa na issue mbio kwa baba ake, akiwa shule simu kwa baba ake 😪
 
Na mzee wao apunguze mihemko au hafaham wapo stage gani? Anyway hayo yote ni matokeo ya malezi ya awali ndio yanaleta majibu, pia kama wazazi mnapaswa kuwapa darasa swala la upevukaji na maadili ili wajue athari zake na faida maana kwenye hatua za ukuaji wanapitia mengi Sana hasa kwenye kufanya majaribio,, baba avae viatu vyake na mama avae viatu vyake inapopendeza zaidi kaeni kama Familia toen elimu ya ukuaji na uzazi kwa watoto!
Asante kwa ushauri, nimeupokea 🙏
 
Huo muda wa balehe ni hatari sana na ndiyo hupima uimara halisi kimalezi kwa wazazi.Hapo baba anapaswa awe baba kweli/father figure mwenyewe!Akili nyingi zitumike.Na,ni vema wazazi wawe mbele kiakili kuliko hao teenagers.Sijui unanielewa @bintiwazamani?
Nimekuelewa mkuu, asante 🙏
 
💯 💯 💯 💯 💯 💯
Kwenye upande wa malezi mzee hakuwa mkali sana ila alikuwa na misimamo yake na ukiikiuka ndio utajikuta unaumia.

Kukwepa maumivu ni kubehave inavyotakiwa, binafsi sikuwa mkorofi na kila ilipotokea sababu ya kutofautiana na mzee mtu wa kwanza kunionya na kunikumbusha ya hekima na heshima ni mama. Hata kama anakwaza vumilia huyo ndio baba yako mheshimu, mjali na umpende. Siwezi kuandika yote ila wamama mna mchango mkubwa sana kuepusha machafuko baina ya watoto na wazazi.
 
Nakumbuka Yapo maneno niliyoambiwa ambayo yalinijenga na kuniharibu pia....

Siku moja, nilimchenjia mjomba wangu' kwasababu alinikuta naongea na simu hivyo tukapishana kweli kweli na kurushiana maneno....

Akachukua fimbo na kunichapa ila baada ya kunichapa bila shaka alijutia alichokifanya na aliniambia maneno yafuatayo ambayo mara nyingi huwa nawaambia vijana maneno hayo hasa wanao sumbua na kukimbilia mahusiano

Kwasababu mahusiano kwenye umri huo ndio uleta changamoto zote hizo

Maneno hayo yalikuwa namna hii...

Alisema "UMEMUONA MAMA YANGU (ambaye ni Bibi yangu) UNAHISI HAKUWA NA WANAUME? na UNAHISI ALIKUWA NAO WANGAPI MPAKA UMRI ULE? Je, unahisi bado anayafanya unayotaka kuyafanya wewe? ALIYAFANYA SANAA NA KAYAACHA VIVYO HIVYO ITATOKEA KWAKO, JITAHIDI KWENYE KUFANYA LITAKALO KUWA NA MATOKEO KWA SASA AMBAYO NI SHULE TU'" "

ni maneno pekee ambayo yanaishi Kila siku iitwapo leo, na kwa bahati mbaya zaidi maneno hayo nimekuwa nayasema hasa kwa watoto wa kike ili waepuke mimba za utotoni hasa wakiwa shuleni lakini ubaya ninao waelekeza unakuta teyari yupo kwenye meza yangu na ni mjamzito teyari 🥲

Naishia kumfanyia counseling na kumkaribisha akapate huduma kwenye Idara ya MAMA NA MTOTO (RCH /CLINIC)

nachomaanisha anza kuwajengea msingi na uwape matamshi na maneno ambayo unaamini yataishi siku zote, katika hatua zao
 
Wewe ndio tatizo hapa!

Baba anapaswa kuwa final say, na subjects wake ndani ya nyumba ikiwemo wewe mnapaswa kujua Hilo!

Inaonesha wewe, ndiye kijogoo humo ndani, na baba ni fala tu! So watoto wameshasoma mchezo!
🤦‍♀️ Haya yote umeyajuaje mkuu?
 
Tusimulie tujifunze, ilikuwaje wewe ukawa shahidi wa haya.
Nilikuwa gangwe na jeuri yawezekana kuliko hao wa kwako.Kuna siku,nikiwa darasa la tano nakumbuka,nilitaka kuzipiga na mjomba wangu.Utovu wa nidhamu wa hali ya juu.Si hivyo tu.Elewa tu,nilikuwa jeuri si nyumbani,mtaani hadi shuleni.Ngumi mkononi.Nikiweka jina langu wazi,wanaonifahamu watacheka sana kwa kumbukumbu za kale.
Sasa basi,nimekuja kupata mtoto wa kiume mkubwa ni tabia zilezile nilizokuwa nafanya.Yaani ananionesha sinema ya yote niliyokuwa nayafanya.Wa kike ni waogawaoga ila wana kila chembechembe za ukorofi na utata tu.Mama yao hana hizo tabia.Watoto wangu ni kioo/taswira yangu kabisa.Kuna kipindi badala ya kuchukia,inabidi nicheke tu na kuelekea kilabuni kunywa komoni.
 
Kuna shida somewhere. Watoto hawana adabu hao. Muda wa balehe vijana au mabinti huwa na tabia ya kutest mamlaka kuu yaani wakubwa kwa maana ya wazazi au walezi.

Ni kitu cha kawaida kabisa kufanya hivyo kwasababu miili yao inaanza kubadilika kimfumo. Kuna hormones zinaanza kufanya kazi na hazikuwapo active mwanzoni.

Hizi hormones huwa ndio msukumo wa tabia unaanzia.

Kama ni mtoto wa kike ataanza kuwa mjeuri kwa mama yake na wataanza kugombana kwa vitu vya kipuuzi sana. Hapa mama na baba wakilegea basi huyo binti ataharibika.

Kwa kijana pia akifika hii stage hormone humsukuma kufanya matendo ya kujaribu kama anaweza kuwa na maamuzi binafsi ama la. Hiyo stage huleta shida kama baba atakuwa legelege na hatumii hekima ya maamuzi. Kijana ni rahisi sana kuharibika stage hii. Hapa ni mwendo wa mokanda na bakora pale kijana anapofanya matendo ya kijinga na alishapewa maonyo au maagizo au makatazo.

Kama hao vijana wako wameanza kujibizana na baba yao it means wanatest kama anawamudu..
 
Mtoto wangu wa kiume alivyo balehe ukaribu na mimi ukapungua akawa karibu na baba yake. Wakati alivyokua mdogo mama this mama that na a.k.a ya mtoto wa mama aliitwa.

Sasa ni busy na baba ake nyumbani akiwa na issue mbio kwa baba ake, akiwa shule simu kwa baba ake 😪
Pole mamie 🤗

Mimi kwangu ni viceversa, watoto wangu walikua karibu zaidi na baba yao mpaka nilikua naona wivu ila kwenye balehe imebadilika, ukaribu na baba yao umeisha kabisa.
 
NNi
Ulivyokua kijana na kipindi cha balehe (teen age), mahusiano yako na baba yako yalikuwaje?

Nina watoto wa kiume wapo kipindi cha balehe na hawaivi kabisa na baba yao, japo hapo zamani walikua wana ukaribu sana. Ugomvi hauishi, kila kitu kidogo lazima watoto wapate mihemuko au wapate hasira na baba yao naye anakasirika (they trigger each other kupita kiasi). Watoto pia hawana uoga kuongea mbele ya baba kama wakiambiwa kitu na hawana utayari (japo huwa hawavunji heshima au kutukana).

Hii hali ni mpya (kwa miaka kadhaa sasa) tokea waingie kwenye balehe (teen years). Wazazi ambao mmeshalea male teens (vijana wa kume wakiwa kwenye balehe) uzoefu wenu ulikuwaje na je baada ya balehe, ukaribu na mahusiano huwa yanarudi tena kama zamani?

Na wanaume wa JF, vipi na wakati unakua mahusiano yako na wazazi yalikuwaje?

Asanteni na Jumapili njema!

View attachment 3360276
Ni kawaida hutokea pale baba anaponirekebisha kila kitu huku najiona kukijua zaidi yake, nilimsumbua hicho Kipindi.

Now mdogo angu anamsumbua nimerudi nimemwambia aniachie namuelekeza taratibu.

#nrne
 
Kwenye upande wa malezi mzee hakuwa mkali sana ila alikuwa na misimamo yake na ukiikiuka ndio utajikuta unaumia.

Kukwepa maumivu ni kubehave inavyotakiwa, binafsi sikuwa mkorofi na kila ilipotokea sababu ya kutofautiana na mzee mtu wa kwanza kunionya na kunikumbusha ya hekima na heshima ni mama. Hata kama anakwaza vumilia huyo ndio baba yako mheshimu, mjali na umpende. Siwezi kuandika yote ila wamama mna mchango mkubwa sana kuepusha machafuko baina ya watoto na wazazi.
Asante sana 😍
Ni hekima kubwa sana inatumika, sana.

Uzuri mimi sina mihemuko na mara kwa mara huwa naingilia (privately / chumbani) kumtuliza baba watoto na kumkumbusha kuwa ni steji tu watoto wanapitia au kuwakumbusha watoto kuheshimu na kusikiliza hata kama hawakubaliani na baba yao.

Tatizo watoto wamerithi hizo mori na hasira za huko kwao, wao na baba yao ni copy & paste ya sura mpaka tabia.
 
Wewe uliyepata malezi mazuri, wakati unakua mahusiano yako na baba yako yalikuwaje.
Ulikulia nyumbani kipindi cha balehe au walikutupa huko shule za bweni?
Mimi kipindi nabelehe mzee aliniagiza nimuwekee maji ya kuoga, nikaenda kuchukua maji ambayo yalikuwa na uchafu wa majani ya miti,nikaweka hivyo hivyo bila kujali ule uchafu.

Alinipiga biti moja la kibabe,hadi baadae nilijitafakari sana kile kitendo changu na kuona kuwa sikuwa na utimamu katika akili.

So haya mambo hutokea na kijana asipofokewa au kuchezea kichapo ubongo wake unaanza kutengeneza kiburi,na tabia ambazo ni matokeo ya kukosa usaidizi na muongozo mzuri wa wazazi.

Ndio maana tunakataza sana usingle mother maana katika stage hii watoto huwa wanahitaji sana muongozo wa baba yao kinyume chake ni watoto kugeuka tatizo halafu majuto ni baadae.
 
Back
Top Bottom