Binti wa zamani
Platinum Member
- Nov 19, 2011
- 15,052
- 36,866
- Thread starter
-
- #41
Shukrani za dhati kwa ushauri mzuri, nimeyachukua yote.Hiyo hali haiepukiki ila ukubwa wake unatagemeana na mizizi iliyowekwa kipindi cha utoto wao na baba yao.
Mtoto ukimchekea sana utotoni akahisi ni marafiki basi katika balehe yake lazima atakupanda kichwani akihisi mnawezana.
Mtoto hapaswi kumuogopa mzazi ila kunapaswa kuwe na uelewa kuwa japo mzazi haogopewi ila nafasi yake ya uzazi haina mjadala, kwamba anachoamua mzazi ndio cha mwisho na hakihojiwi.
Haipaswi mtoto kuwa na nafasi yeyote ya kukaidi, kuhoji ama kujibizana na mzazi as long as bado anaishi katika himaya ya mzazi na bado anategemea mzazi.
Pia watoto wanapaswa kutambua kuwa wazazi wote wawili ni kitu kimoja sio kwamba mmoja ni 'fair' na mwingine ni mkuda.
Nyumba nyingi utakuta mzazi mmoja anajifanya mwema sana hasa mama na kumrushia uhaini wote baba. Hii inajenga taswira mbaya kwa baba mbele ya watoto.
Inapaswa itambulike kwa watoto wote kuwa maamuzi ya wazazi wote ni mamoja na kuwa ikitokea hukumu/agizo/maamuzi ni la wazazi wote.
Inapaswa wazazi waepuke kubishana juu ya maamuzi ya watoto wao mbele ya watoto. Hata kama hamkubaliani kuhusu jambo, inapaswa mfanyie pembeni mabishano sio mbele ya watoto.
Kubwa na la muhimu zaidi, mtoto hatakiwi kuwa na uhuru wa kuongea ujinga wowote juu mzazi mmoja kwenda kwa mzazi mwingine pasi na uwepo wa mzazi huyo. Yani haijalishi mtoto kakerwa kiasi gani, hatakiwi kuwa na ujasiri wa kwenda kuongea shiti juu ya baba mbele ya mama na mama nae aka support.
Nguvu ya ulezi bora inapatikana kwa umoja wa wazazi wote wawili.
Sio baba anatoa hukumu/adhabu, mama anamuita mtoto pembeni na kumbembeleza.
Asante kwa ushauri, nimeupokea 🙏Na mzee wao apunguze mihemko au hafaham wapo stage gani? Anyway hayo yote ni matokeo ya malezi ya awali ndio yanaleta majibu, pia kama wazazi mnapaswa kuwapa darasa swala la upevukaji na maadili ili wajue athari zake na faida maana kwenye hatua za ukuaji wanapitia mengi Sana hasa kwenye kufanya majaribio,, baba avae viatu vyake na mama avae viatu vyake inapopendeza zaidi kaeni kama Familia toen elimu ya ukuaji na uzazi kwa watoto!
Nimekuelewa mkuu, asante 🙏Huo muda wa balehe ni hatari sana na ndiyo hupima uimara halisi kimalezi kwa wazazi.Hapo baba anapaswa awe baba kweli/father figure mwenyewe!Akili nyingi zitumike.Na,ni vema wazazi wawe mbele kiakili kuliko hao teenagers.Sijui unanielewa @bintiwazamani?
Kwenye upande wa malezi mzee hakuwa mkali sana ila alikuwa na misimamo yake na ukiikiuka ndio utajikuta unaumia.💯 💯 💯 💯 💯 💯
Daaah 😆😆😆😆😂😂😂Hao watoto wanakuonea wew wivu,hawataki baba yao akubandue.
Sawa, asante 🙏Hiyo kawaida, wakikua zaidi wataanza kuelewa,
Tusimulie tujifunze, ilikuwaje wewe ukawa shahidi wa haya.Ngojeni wawasumbue na kuwaonea.Ni zamu yao.Ila,wakae wakijua na wao yatawakuta tu ukubwani.Mimi shahidi.
NB;Kuweni nao makini sana na akili nyingi zitumike kulea magangwe/new kids on the block.
Daaah uko kwa mfalme, haya jumapili njema, furahia sebene la Mungu mtu.Anyway karbu hapa kwa zumaridi tucheze sebene na kupiga ramli.
🤦♀️ Haya yote umeyajuaje mkuu?Wewe ndio tatizo hapa!
Baba anapaswa kuwa final say, na subjects wake ndani ya nyumba ikiwemo wewe mnapaswa kujua Hilo!
Inaonesha wewe, ndiye kijogoo humo ndani, na baba ni fala tu! So watoto wameshasoma mchezo!
Hapana sijui, karibu unielezee vizuri.Unajua chimbuko la tatizo ni wewe?
Nilikuwa gangwe na jeuri yawezekana kuliko hao wa kwako.Kuna siku,nikiwa darasa la tano nakumbuka,nilitaka kuzipiga na mjomba wangu.Utovu wa nidhamu wa hali ya juu.Si hivyo tu.Elewa tu,nilikuwa jeuri si nyumbani,mtaani hadi shuleni.Ngumi mkononi.Nikiweka jina langu wazi,wanaonifahamu watacheka sana kwa kumbukumbu za kale.Tusimulie tujifunze, ilikuwaje wewe ukawa shahidi wa haya.
Pole mamie 🤗Mtoto wangu wa kiume alivyo balehe ukaribu na mimi ukapungua akawa karibu na baba yake. Wakati alivyokua mdogo mama this mama that na a.k.a ya mtoto wa mama aliitwa.
Sasa ni busy na baba ake nyumbani akiwa na issue mbio kwa baba ake, akiwa shule simu kwa baba ake 😪
Ni kawaida hutokea pale baba anaponirekebisha kila kitu huku najiona kukijua zaidi yake, nilimsumbua hicho Kipindi.Ulivyokua kijana na kipindi cha balehe (teen age), mahusiano yako na baba yako yalikuwaje?
Nina watoto wa kiume wapo kipindi cha balehe na hawaivi kabisa na baba yao, japo hapo zamani walikua wana ukaribu sana. Ugomvi hauishi, kila kitu kidogo lazima watoto wapate mihemuko au wapate hasira na baba yao naye anakasirika (they trigger each other kupita kiasi). Watoto pia hawana uoga kuongea mbele ya baba kama wakiambiwa kitu na hawana utayari (japo huwa hawavunji heshima au kutukana).
Hii hali ni mpya (kwa miaka kadhaa sasa) tokea waingie kwenye balehe (teen years). Wazazi ambao mmeshalea male teens (vijana wa kume wakiwa kwenye balehe) uzoefu wenu ulikuwaje na je baada ya balehe, ukaribu na mahusiano huwa yanarudi tena kama zamani?
Na wanaume wa JF, vipi na wakati unakua mahusiano yako na wazazi yalikuwaje?
Asanteni na Jumapili njema!
View attachment 3360276
Hili sio sebene la Mungu,ni sebene la Zumaridi.Daaah uko kwa mfalme, haya jumapili njema, furahia sebene la Mungu mtu.
Asante sana 😍Kwenye upande wa malezi mzee hakuwa mkali sana ila alikuwa na misimamo yake na ukiikiuka ndio utajikuta unaumia.
Kukwepa maumivu ni kubehave inavyotakiwa, binafsi sikuwa mkorofi na kila ilipotokea sababu ya kutofautiana na mzee mtu wa kwanza kunionya na kunikumbusha ya hekima na heshima ni mama. Hata kama anakwaza vumilia huyo ndio baba yako mheshimu, mjali na umpende. Siwezi kuandika yote ila wamama mna mchango mkubwa sana kuepusha machafuko baina ya watoto na wazazi.
Mimi kipindi nabelehe mzee aliniagiza nimuwekee maji ya kuoga, nikaenda kuchukua maji ambayo yalikuwa na uchafu wa majani ya miti,nikaweka hivyo hivyo bila kujali ule uchafu.Wewe uliyepata malezi mazuri, wakati unakua mahusiano yako na baba yako yalikuwaje.
Ulikulia nyumbani kipindi cha balehe au walikutupa huko shule za bweni?