Wanaume ni dhaifu na hawajiamini mbele ya wanawake

Umeelewa kweli mkuu swali nililo kuuliza ?
Unaelekea bado umetekwa na elements za ubeberu na ubepari!

Nimekujibu kulingana na madaa husika na sio swali lako kwakua swali lako linavishiria gandamizi vya mwanaume dhaifu mbele ya mwanamke!
 
Mtoa mada umetumia point nyepesi sana kutetea heading yako neno 'Dhaifu' lina maana zaidi ya ulivyoelezea hebu kachimbe vizuri madesa ujue maana ya udhaifu na relate kati ya mwanaume na mwanamke na ukielewa utakuja kuomba kufutwa kwa huu uzi
 
Feminists wanazidi kuongezeka nchi hii.
 
Unaelekea bado umetekwa na elements za ubeberu na ubepari!

Nimekujibu kulingana na madaa husika na sio swali lako kwakua swali lako linavishiria gandamizi vya mwanaume dhaifu mbele ya mwanamke!
Jitahidi kuji elimisha kwanza kabla ya kuandika thread humu jifunze kuhusu wanawake na jifunze pia kuhusu wanaume. udhaifu ulio nao wewe usiufanye kuwa udhaifu wa jamii nzima.

N.b: Pia kaa tambua kuwa mwanaume hapaswi na ni marufuku kwake yeye kujiaminisha ni dhaifu hii ni hasara kwa familia yake, tambua kuwa mwanaume ni imara na uimara wa mwanaume una anzia kichwa[ akilini ] mpaka mwili mzima[ nguvu ], mke na watoto hawato jihisi na amani kama wana baba dhaifu weka kichwani kwako hili na anza kujitambua kuanzia sasa kuwa wewe ni mwanaume na haupo special group kama walipo wanawake.
 
Kuna aibu na udhaifu

We umezungumzia aibu!!
Huwezi kuwa na aibu kama sio dhaifu
Aibu ni dalili kubwa ya udhaifu (psychological)
Na hata title umesema wanaume ni dhaifu hawajiamini mbele ya wanawake.
Sasa aibu si ndio kutojiamini kwenyewe?
 
Kwa kawaida mtu anayeamini kwamba, ni dhaifu, hujaribu kwa kila njia kuficha udhaifu wake, na moja ya njia hizo ni kujikweza ili kujaribu kumshusha yule ambaye anadhani anamzidi. Mtu asiye na nguvu anaweza kujitahidi kupiga kelele, kupiga ‘mikwala’ na vitisho, na watu wanapomwogopa, hupata nafasi ya kuwakandamiza hadi pale inapotokea bahati watu hao wakamshtukia kwamba hana nguvu anazodai anazo. Hata hivyo, ule woga kwa mtu huyo utaendelea kuwepo kwa watu wengi.
View attachment 2414670
Kwa miaka mingi mwanaume aligundua kwamba, ni dhaifu mbele ya mwanamke na katika juhudi za kufidia pengo hili alipitiliza mipaka na kujikuta anafanikiwa kumkandamiza mwanamke. Eneo ambalo mwanaume anaweza kusema ni bora kuliko mwanamke labda ni mabavu ya kimwili, ambayo kwa bahati mbaya kwenye zama hizi hayana tena maana, yamepitwa na wakati.

Ukiangalia maeneo mengine yote, mwanamke ndiye bora zaidi. Mwanamke huishi miaka mingi zaidi ya mwanaume (kati ya miaka mitano hadi kumi) na mwanamke huugua au kupata maradhi kidogo zaidi kuliko mwanaume. Wanaume wengi zaidi, kwa kiasi cha mara mbili zaidi hupata matatizo ya kiakili ukilinganisha na wanawake, huku idadi ya wanaume wanaojiuwa ikiwa kubwa zaidi kuliko ile ya wanawake.
View attachment 2414680
Ni kweli, mwanaume anaweza kuringia mabavu yake, lakini huo siyo ubora ambao binadamu anatakiwa kuuringia sasa hivi, kwani unahusu zaidi wanyama kuliko binadamu. Enzi za kuuwa wanyama kwa mawe, mabavu yalikuwa na maana, si leo. Mwanaume kwa karne kadhaa amejitahidi kutumia mabavu yake kumwonyesha mwanamke kwamba, yeye siyo dhaifu. Kwa bahati mbaya mwanamke naye akadhani ni dhaifu. Yeye kukosa mabavu akadhani ni udhaifu. Kwa wakati huo ilikuwa ni sahihi kwa sababu binadamu aliishi kama mnyama. Mtu aliyeheshimiwa alikuwa ni yule aliyekuwa na nguvu za kuuwa mnyama kwa jiwe, lakini bila shaka, leo mambo ni tofauti.
View attachment 2414684
Hebu ona, hadi leo mwanaume anaweza kuhatarisha maisha yake au hata kupoteza maisha akijaribu kutafuta njia za kumfanya mwanamke amwone kuwa ni wa maana. Atasema uongo, atajikweza, atajifaragua, akitafuta kukubaliwa na mwanamke. Huu ni udhaifu mkubwa na unaonyesha ni kwa kiasi gani jinsia hii isivyojiamini. Udhaifu huu na mwingine ndiyo ambao mwanaume amekuwa akitafuta kuuficha ili mwanamke asiuone, ambapo ameamua kumkandamiza kwa mabavu.

Mwanazuoni mmoja wa utambuzi alipata kusema, wale wanaume wote ambao walijitahidi kuifanya dunia hii kuwa mahali penye kupendeza, walikuwa na tabia ambazo ni wanawake zaidi wanaokuwa nazo. Walikuwa na huruma, upendo, unyenyekevu, kusamehe, kusaidia na kujali. Leo hii mwanaume ukitaka kuitwa mwanamke, onyesha huruma, onyesha upendo, onyesha usamehevu. Unaweza kuona ilivyo, kwamba, bila kuonyesha mabavu manaume anahisi kuumbuka.
View attachment 2414686
Kuna wakati tulikuwa tukizungumza na ndugu yangu ambaye alikuwa anatarajia kufunga ndoa. Mmoja kati ya ndugu zangu waliokuwepo alisema, ‘inabidi huyo mchumbako tumuone, kwa upole wako anaweza kukukalia ukimwoa.’ Unaona? Kinachomlinda mwanaume ni kitu kimoja tu, kuwa mbabe na mkali, basi. Hana silaha nyingine na hajawahi kuwa nayo, hivyo akiiachia hii ya mabavu, anajua atakuwa amekwisha……
labda wanaume wa Daslam.!
 
Mwanamke wa sasa atakutoa jasho broh!

Assuming mfano mdogo juzi kwenye ile ajali airhostess alivyopamba na majaliwa hadi kuufungua mlango wa ndege ilikuaje hebu jaribu kuvuta taswira ilikuaje kwenye tukio juu ya huyo mwanamke na ujasiri wake
Kwa taarifa yako tu aliyemuumba Ke mwenyewe alikiri dhahiri kuwa "KE NI KIUMBE DHAIFU"

Mi ni nani haswa hata nipingane na kauli yake Mungu?
 
Kwa kawaida mtu anayeamini kwamba, ni dhaifu, hujaribu kwa kila njia kuficha udhaifu wake, na moja ya njia hizo ni kujikweza ili kujaribu kumshusha yule ambaye anadhani anamzidi. Mtu asiye na nguvu anaweza kujitahidi kupiga kelele, kupiga ‘mikwala’ na vitisho, na watu wanapomwogopa, hupata nafasi ya kuwakandamiza hadi pale inapotokea bahati watu hao wakamshtukia kwamba hana nguvu anazodai anazo. Hata hivyo, ule woga kwa mtu huyo utaendelea kuwepo kwa watu wengi.
View attachment 2414670
Kwa miaka mingi mwanaume aligundua kwamba, ni dhaifu mbele ya mwanamke na katika juhudi za kufidia pengo hili alipitiliza mipaka na kujikuta anafanikiwa kumkandamiza mwanamke. Eneo ambalo mwanaume anaweza kusema ni bora kuliko mwanamke labda ni mabavu ya kimwili, ambayo kwa bahati mbaya kwenye zama hizi hayana tena maana, yamepitwa na wakati.

Ukiangalia maeneo mengine yote, mwanamke ndiye bora zaidi. Mwanamke huishi miaka mingi zaidi ya mwanaume (kati ya miaka mitano hadi kumi) na mwanamke huugua au kupata maradhi kidogo zaidi kuliko mwanaume. Wanaume wengi zaidi, kwa kiasi cha mara mbili zaidi hupata matatizo ya kiakili ukilinganisha na wanawake, huku idadi ya wanaume wanaojiuwa ikiwa kubwa zaidi kuliko ile ya wanawake.
View attachment 2414680
Ni kweli, mwanaume anaweza kuringia mabavu yake, lakini huo siyo ubora ambao binadamu anatakiwa kuuringia sasa hivi, kwani unahusu zaidi wanyama kuliko binadamu. Enzi za kuuwa wanyama kwa mawe, mabavu yalikuwa na maana, si leo. Mwanaume kwa karne kadhaa amejitahidi kutumia mabavu yake kumwonyesha mwanamke kwamba, yeye siyo dhaifu. Kwa bahati mbaya mwanamke naye akadhani ni dhaifu. Yeye kukosa mabavu akadhani ni udhaifu. Kwa wakati huo ilikuwa ni sahihi kwa sababu binadamu aliishi kama mnyama. Mtu aliyeheshimiwa alikuwa ni yule aliyekuwa na nguvu za kuuwa mnyama kwa jiwe, lakini bila shaka, leo mambo ni tofauti.
View attachment 2414684
Hebu ona, hadi leo mwanaume anaweza kuhatarisha maisha yake au hata kupoteza maisha akijaribu kutafuta njia za kumfanya mwanamke amwone kuwa ni wa maana. Atasema uongo, atajikweza, atajifaragua, akitafuta kukubaliwa na mwanamke. Huu ni udhaifu mkubwa na unaonyesha ni kwa kiasi gani jinsia hii isivyojiamini. Udhaifu huu na mwingine ndiyo ambao mwanaume amekuwa akitafuta kuuficha ili mwanamke asiuone, ambapo ameamua kumkandamiza kwa mabavu.

Mwanazuoni mmoja wa utambuzi alipata kusema, wale wanaume wote ambao walijitahidi kuifanya dunia hii kuwa mahali penye kupendeza, walikuwa na tabia ambazo ni wanawake zaidi wanaokuwa nazo. Walikuwa na huruma, upendo, unyenyekevu, kusamehe, kusaidia na kujali. Leo hii mwanaume ukitaka kuitwa mwanamke, onyesha huruma, onyesha upendo, onyesha usamehevu. Unaweza kuona ilivyo, kwamba, bila kuonyesha mabavu manaume anahisi kuumbuka.
View attachment 2414686
Kuna wakati tulikuwa tukizungumza na ndugu yangu ambaye alikuwa anatarajia kufunga ndoa. Mmoja kati ya ndugu zangu waliokuwepo alisema, ‘inabidi huyo mchumbako tumuone, kwa upole wako anaweza kukukalia ukimwoa.’ Unaona? Kinachomlinda mwanaume ni kitu kimoja tu, kuwa mbabe na mkali, basi. Hana silaha nyingine na hajawahi kuwa nayo, hivyo akiiachia hii ya mabavu, anajua atakuwa amekwisha……
Feminism [emoji706][emoji706]. Yan mwanaume umekaa unahaikweza mbavu (ya kushoto) eti iuzidi mwili. Mwanamke atabaki kuwa mbarara tu mpaka jua litapochomozea magharibi.
 
Mtoa mada umetumia point nyepesi sana kutetea heading yako neno 'Dhaifu' lina maana zaidi ya ulivyoelezea hebu kachimbe vizuri madesa ujue maana ya udhaifu na relate kati ya mwanaume na mwanamke na ukielewa utakuja kuomba kufutwa kwa huu uzi
Nimekupata vyema mkuu Singano jr ila hapo kwenye hii mada
Jitahidi kuji elimisha kwanza kabla ya kuandika thread humu jifunze kuhusu wanawake na jifunze pia kuhusu wanaume. udhaifu ulio nao wewe usiufanye kuwa udhaifu wa jamii nzima.

N.b: Pia kaa tambua kuwa mwanaume hapaswi na ni marufuku kwake yeye kujiaminisha ni dhaifu hii ni hasara kwa familia yake, tambua kuwa mwanaume ni imara na uimara wa mwanaume una anzia kichwa[ akilini ] mpaka mwili mzima[ nguvu ], mke na watoto hawato jihisi na amani kama wana baba dhaifu weka kichwani kwako hili na anza kujitambua kuanzia sasa kuwa wewe ni mwanaume na haupo special group kama walipo wanawake.
Inaelekea mkuu binafsi nakuona kuwa hujiamini sana ukiwa na familia yako hata inakupelekea kuwatisha kwa ukali ilikuficha udhaifu wako licha ya kuwa unatambua unachokifanya sio sahihi.

Siri kubwa ya kuweza kujenga familia yenye furaha ni kuwa honest with them only na si kuwakoromea kila unapokua nao ili huwa inawajengea hofu na chuki so kuamakini na hili, Wewe ni sawa na baba anaerudi nyumbani halafu watoto wote wanakimbilia vyumbani kwa hofu hivi unaona hapo kutakua na upendo kweli au ni heshima ya usoni tu!
 
Mkuu kua na jitambue kuwa wewe ni nani na ni jinsia gani ?
 
Kuna mchungajii aliwahi sema mwanamke anaweza pita sokoni bila nguo, na kesho yake akarudi ameva vizurii akasifiwa na Kila mtuu ... Ila mwanaume hawezi rudia pita hapo tena hata nyasi ziotee pawe msituu hapiti kamwe
 
Huwezi kuwa na aibu kama sio dhaifu
Aibu ni dalili kubwa ya udhaifu (psychological)
Na hata title umesema wanaume ni dhaifu hawajiamini mbele ya wanawake.
Sasa aibu si ndio kutojiamini kwenyewe?
Aibu ni hali ya kuona (HAYA)

Udhaifu ni unyonge na huu unyonge unatokana na mabavu ambayo wengi wetu tumekua tukiyaonyesha mbele zao na kujikweza lkn inapofikia tu siku umekosa kidogo mbele yao huwa wanaanza na kukudharau na kisha unakua dhaifu mbele Yao.
 
Mkuu kua na jitambue kuwa wewe ni nani na ni jinsia gani ?
Wakiume na si dhaifu mbele yao kwa kua sina unyanyasaji wa kubepari natumia terminology sahihi kuwaelekeza hata wakiniona wanapata faraja lkn wewe mkuu utapata shida sana na hizi attitude zako za miaka ya Sabini(70) ambapo ilikua tanzania ya Giza!
 
Back
Top Bottom