Wanaume tuache ubahili tuwatunze wapenzi wetu

Wanaume tuache ubahili tuwatunze wapenzi wetu

Jembemtaji

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2014
Posts
1,193
Reaction score
926
Kwanza nianze kwa kukiri kuwa maisha ni magumu sana nadhani kila mtu anajua.

Na katika mahusiano ya mapenzi kati ya me na ke lazima kunakuwa na tofauti ya kipato, yaani Mara nyingi wanaume wanakuwa na hali mzuri kimapato kuliko mwanamke.

Nieleweke vizuri kuwa simaanishi kuwa wanawake wote wana kipato duni la hasha.

Ningependa kuwashauri wale wenye wapenzi wa kike mambo haya yafuatayo:-

1 Ujue tofauti ya kuchunwa na kuhudumia, unapokuwa na mpenzi ujue ni jukumu lako kumpendezesha anapopendeza watu watajua wewe ndio kidume uliemwezesha.

2 .Sio mpaka akuombe ndio umpe. jaribu kumfaamu hali ya maisha na kipato chake ujue kukisia cha kumpa kwa matumizi yake.

3.Usiulize ya nini,ikitokea mpenzi amekuomba HELA usiulize ya nini ye ni MTU mzima awezi kukuomba HELA akaenda kuchambia.

4. Kutumia pesa nyingi sehemu ya starehe.
Kuna watu wanaenda mpaka hotel ya nyota 5 kustarehe akitumia zaidi ya laki tano.Cha ajabu baada ya kutoka hotel anamwacha mpenzi wake 10000 ya nauli.

Huu ni ujinga bora ungeenda ata lodge ya nafuu yeye ukamwacha na HELA ya kutosha.

5.Tenga ata 10% ya mshahara MPE yeye aangalie kama kuna kitu cha kurekebisha arekebishe.

NB.
APA ni kwa wale Wanaume wanaowazidi kipato wanawake wao sio wanawake wenye vipato vizur.

Tusiwe wataalam wakutafuta Gspot wakati ukiombwa ata 1000 unanuna mapenzi ni pamoja na kupunguzia makali ya maisha.

Yeyote mwenye chochote anaweza kuongezea apo.
 
watu wengine bwana shughuli hajui,sura ile ya waliokosa shule siku wenzie wakipewa sura nzuri,ni mfupi,kauli mbaya, bado hakupendezeshi eeeh cjui naye huyu wanini?
 
Jembemtaji

samahani,we mwanamke au mwanamme?nilitegemea unasema tuwatunze wake zetu,kumbe wapenzi ambao ni waleo wa kesho?ebo!!!
 
Last edited by a moderator:
Kumpa pesa mpenzi ili kumhudumia kama mke? Hivi wanawake unawajua au unawauliza? Hudumieni, yangu macho.
^^

mkuu umemaliza,huyu atakuwa anawashwa na vijisenti baada ya kuuza pamba,hivi lile jembe langu nani nani cjuil likowapi lisafishe account za huyu mtu.siku moja tu milioni mbili tuone kama anaweza hudumia
 
Aisee... 10%, mapenzi yana kamisheni siku hizi?!
 
Watu wafikiri kwa kutumia makalio! yaani nitenge 10% kwa ajili ya mtu ambaye sijamuoa!! ninyi ndio mnawaharibu mabinti wa sasa na kuwafanya watangulize pesa mbele.
Yaani mshahara wangu nishindwe kufanya biashara au kusaidia kwetu eti nimsaidie hawala! kweli watanzania tuna safari ndefu kufikia kitu tunachoita maendeleo.
Nimekumbuka msemo mmoja kwenye biblia unasema "Amwajilie mpumbavu ni sawa kuajili wapita njia".
 
wakichoka kutembea/kucheza mziki MUWABEBE hata mgongoni
16137-RhondaWalkerandRobertShumake3.jpg
 
Nilijua tu watu povu litawatoka..mna nini enyi wanaume? Eti siwezi kumhudumia wakati sijamuoa.....mbona papuchi ukinyimwa unanuna ? Kwani mkeo huyo? We kunihudumia kama mke utata ila wewe unataka uwe treated kama mume.....msiwe selfish kiasi hicho loh
 
Jembemtaji

Iko vizuri sana, Mimi nadhani tunapokuwa na mahusiano ambayo yapo komited tunapaswa kufanya zaidi ya hapo, kwa mfano kama gal wangu kapanga basi nijue anaishije na anakosa nini? Kwa kawaida wanaume tunapenda wanawake wenye wivu(fear to loose you by any cost), lakini pia wenye kututhamini(Hata ukiwa naye hotel yeye ndiye anakumiminia juice), Ambao hutumisi(Kwa mfano umetoka job anakuambia Leo tunaondoka wote kuna kitu nitakuambia kumbe kakumisi), But also mwanamke mwenye Upendo(Kwa mfano anapita smwhere anakuchukulia shati zuriii, siyo yeye muda wote anajifikiria, I swear zawadi ya mwanamke kumpa mume ni nzito, it means a lot) ...kwa mambo haya usishangae mpenzi anaendesha BMWX8 halafu kidume anadunda na infinity Q56
 
Last edited by a moderator:
Nilijua tu watu povu litawatoka..mna nini enyi wanaume? Eti siwezi kumhudumia wakati sijamuoa.....mbona papuchi ukinyimwa unanuna ? Kwani mkeo huyo? We kunihudumia kama mke utata ila wewe unataka uwe treated kama mume.....msiwe selfish kiasi hicho loh

Kila mwamba ngozi....
 
Back
Top Bottom