Baba ni baba tu
Baba ni kichwa cha familia, na mama ni shingo katika familia.
Kichwa kazi yake ni kuongoza, na shingo kazi yake ni kuzungusha kichwa kutazama kulia, kushoto, mbele na nyuma.
Kuwa na watoto katika familia ni jambo la muhimu sana, na linaimarisha uwepo wa uzao wako hapa duniani, na wakati mwingine tunaamini ni baraka hasa pale utakapo wahitaji katika msaada wao.
Kuwapa elimu bora, chakula kizuri, mavazi safi, huduma bora za kiafya, malazi mazuri ni jukumu la wazazi katika kufanikisha hilo.
Chukulia mfano wewe ni muajiriwa/mfanya biashara; mshahara wako/faida yako kwa mwezi ni milioni moja.
Na una watoto wanne, ambao wote wanasoma, aliyepo chini labda yuko darasa la kwanza. Ada kwa kila mmoja kwa wastani ni milioni 2.
Ikiwa na maana kuwa, kwa mwaka unatakiwa ulipe milioni nane (8) kwa ajili ya kusomesha; kama utawahudumia kwa miaka 20 mpaka wajitegemee,ina maana utatumia zaidi ya milioni 160 kwa kuwapa elimu tu.
Hapo bado hujafikiria vitu vingine.
Kwa mahesabu hayo, unatakiwa ujenge pia, ufungue vyanzo vingine vya mapato n.k, je hizo pesa utapata wapi?
Ukiona watu wanataka wazeekee maofisini au kwenye uongozi, ni kwa sababu ya mambo kama hayo.
Ukisubiria kiinua mgongo, ambapo umetumika miaka mingi kwenye ajira, hakikidhi gharama za kusomesha hao vijana.
Kwa mazingira hayo, wababa tushtuke mapema, tupunguze uwekezaji kwa michepuko.
Karibu kwa mjadala.