Wanaume tuamke tusihonge sana kwa michepuko, mbele tuna majukumu mazito.

Wanaume tuamke tusihonge sana kwa michepuko, mbele tuna majukumu mazito.

Baba ni baba tu

Baba ni kichwa cha familia, na mama ni shingo katika familia.

Kichwa kazi yake ni kuongoza, na shingo kazi yake ni kuzungusha kichwa kutazama kulia, kushoto, mbele na nyuma.

Kuwa na watoto katika familia ni jambo la muhimu sana, na linaimarisha uwepo wa uzao wako hapa duniani, na wakati mwingine tunaamini ni baraka hasa pale utakapo wahitaji katika msaada wao.

Kuwapa elimu bora, chakula kizuri, mavazi safi, huduma bora za kiafya, malazi mazuri ni jukumu la wazazi katika kufanikisha hilo.

Chukulia mfano wewe ni muajiriwa/mfanya biashara; mshahara wako/faida yako kwa mwezi ni milioni moja.

Na una watoto wanne, ambao wote wanasoma, aliyepo chini labda yuko darasa la kwanza. Ada kwa kila mmoja kwa wastani ni milioni 2.

Ikiwa na maana kuwa, kwa mwaka unatakiwa ulipe milioni nane (8) kwa ajili ya kusomesha; kama utawahudumia kwa miaka 20 mpaka wajitegemee,ina maana utatumia zaidi ya milioni 160 kwa kuwapa elimu tu.

Hapo bado hujafikiria vitu vingine.

Kwa mahesabu hayo, unatakiwa ujenge pia, ufungue vyanzo vingine vya mapato n.k, je hizo pesa utapata wapi?

Ukiona watu wanataka wazeekee maofisini au kwenye uongozi, ni kwa sababu ya mambo kama hayo.

Ukisubiria kiinua mgongo, ambapo umetumika miaka mingi kwenye ajira, hakikidhi gharama za kusomesha hao vijana.

Kwa mazingira hayo, wababa tushtuke mapema, tupunguze uwekezaji kwa michepuko.

Karibu kwa mjadala.
​
Mimi nimeshazama kwenye huu uraibu wa michepuko cha ajabu sasa siogopi kuhonga kama zamani wakati kiuchumi nina hali mbaya kuliko kabla
 
Kulitambua hili ni muhimu
Jamii huwa haina huruma na Mwanaume kabisa.

Kwahiyo usipojihurumia utakufa unajiona .


Last week kuna jamaa amefariki kagongwa na gari Mbagala.

Huyu jamaa around mwezi wa 05 aligongwa na bodaboda akazimia kabisa na kushonwa n.k

Ila kabla hajapona Mke wake akawa anamlazimisha arudi mzigoni kupiga bodaboda na akarudi na akafa .



Nataka kusema nini ile kupata ajali ilitosha either kumbadilishia Kazi au Ku force apate mtaji .


Na alikuwa rafiki yangu nilimwambia Mkuu unabidi kuachana na hii Kazi kwakuwa IPO na high risk

Akasema nikiacha mke atakula nini

Kumbuka huyo hakuwa mke bali Malaya tu kamuweka ndani wala hajapata nae mtoto so is about shit


Jamii yetu imemtengeneza mwanaume Kama mtumwa
 
Baada unikataze mazima wewe ndo unipa moyo of course nahonga asilima 20 ya kipato changu
Kwa mwanaume aliyekamilika, kuacha kabisa ni ngumu; ila ni muhimu kuhonga kwa kiasi huku ukijua kuna majukumu mazito mbele.
 
Jamii huwa haina huruma na Mwanaume kabisa.

Kwahiyo usipojihurumia utakufa unajiona .


Last week kuna jamaa amefariki kagongwa na gari Mbagala.

Huyu jamaa around mwezi wa 05 aligongwa na bodaboda akazimia kabisa na kushonwa n.k

Ila kabla hajapona Mke wake akawa anamlazimisha arudi mzigoni kupiga bodaboda na akarudi na akafa .



Nataka kusema nini ile kupata ajali ilitosha either kumbadilishia Kazi au Ku force apate mtaji .


Na alikuwa rafiki yangu nilimwambia Mkuu unabidi kuachana na hii Kazi kwakuwa IPO na high risk

Akasema nikiacha mke atakula nini

Kumbuka huyo hakuwa mke bali Malaya tu kamuweka ndani wala hajapata nae mtoto so is about shit


Jamii yetu imemtengeneza mwanaume Kama mtumwa
Jamaa alizingua sana yaani hana hata mtoto anajitesa hivyo?
 
Back
Top Bottom