Msanii
Platinum Member
- Jul 4, 2007
- 25,252
- 36,513
Silaha nzuri kuliko yote ni kuishi na majirani vizuri, hasa wale third class.Chukua mfano wamefanikiwa kuingia mipaka ya eneo lako, wewe ndio mwanaume upo chumbani ama upo na wanafamilia chumbani, kwenye situation kama hiyo ni silaha ipi nzuri kukabiliana na wavamiaji?
Binafsi nina firimbi zile za walinzi na sungusungu, zinasaidia kumpa wenge mvamiaji kudhani kwamba pana ulinzi shirikishi, filimbi hizi hazizidi elf 2 kwa machinga.
Kwa mashambulizi ya mbali nina manati na golori za chuma, sio ya kuyachukulia poa hata kidogo, nikivuta hadi mwisho nikiachia, lazima ukae ama ubebwe.
nina rungu kama la komredi kipepe kwa mashambulizi ya ana kwa ana man to man, lakini ningependa tuelimishane zaidi.
Kupitia uzi huu tuelimishane silaha za kuwa nazo, kuzificha, matumizi sahihi, n.k.
Hautakaa uvamiwe.