Wanaume tuelimishane ulinzi, ni silaha gani nje ya bunduki ni nzuri kuimiliki sehemu unayoishi?

Wanaume tuelimishane ulinzi, ni silaha gani nje ya bunduki ni nzuri kuimiliki sehemu unayoishi?

Chukua mfano wavamiaji wameishafanikiwa kuingia sebuleni wewe upo chumbani ama upo na wanafamilia chumbani, kwenye situation kama hiyo ni silaha ipi nzuri kukabiliana na wavamiaji?

Binafsi nina rungu kama la komredi kipepe kwa mashambulizi ya ana kwa ana man to man, lakini ningependa tuelimishane zaidi.

Kupitia uzi huu tuelimishane silaha za kuwa nazo, kuzificha, matumizi sahihi, n.k.
Kama una idea ya UMEME hatua a kwanza ni kukipiga short kitasa cha chumbani,unaunga waya kwenye socket unagusisha kitasa ,akishika tu anajiground
 
Silaha nzuri ili usalimike na wale majamaa ni kuwa na HELA.
Wakikuvamia ujue wana clue kwamba una mzigo ndani na pengine hadi amount kamili.
Sasa ili kunusulu uhai wako na familia kwaujumla yapasa uyasikilize yale majamaa hayana maskhara.
Huku kumiliki bunduki sijui manati na podo ni kubahatisha na timing tu!
Kumbuka jambazi mpaka anaingia ndani ujue kauza roho.

Mbinu nzuri ya kujizatiti na majambazi ni kuishi na majirani zako vizuri pasipo kujenga mazoea yanayopita kiwango cha ustaarab.
Pindi majambazi wakikuvamia, chap una escalate incidency kwa majirani. Kelele au kuvizia kwa kutokea nje ni rahisi sana kutibua mipango na kuzua taharuki kwa majambazi waliojipanga kwa uvamizi.
 
Chukua mfano wavamiaji wameishafanikiwa kuingia sebuleni wewe upo chumbani ama upo na wanafamilia chumbani, kwenye situation kama hiyo ni silaha ipi nzuri kukabiliana na wavamiaji?

Binafsi nina rungu kama la komredi kipepe kwa mashambulizi ya ana kwa ana man to man, lakini ningependa tuelimishane zaidi.

Kupitia uzi huu tuelimishane silaha za kuwa nazo, kuzificha, matumizi sahihi, n.k.
Waweza weka pia chombo kama beseni chenye maji chumvi ,ukakipiga short pia ili muhuni wa kwanza akutane na uchawi wa mzungu,ukilegeza mmoja wengine wanapotea
 
Ni timing tuu, nani anajua Kitu kinaitwa Dohani?

Nyumba za zamani hasa za wazungu zilikua na sehemu ya kuwashia moto ndani sbb ya baridi[emoji116]
Screenshot_20230823_184040_Google.jpg

Halafu ile sehemu ina vent(chimney)ya kutoka juu kwa ajili ya moshi[emoji116]
Screenshot_20230823_184312_Google.jpg
Sasa mimi nilishawahi kupita pale kati kati nikanata juu huku chini moshi unapanda.
Screenshot_20230823_183621_Gallery.jpg
 
Silaha yangu kubwa ni kutokuishi Keko, Temeke, Vinguguti, Tandale, Mbagala na maeneo yote yasio na watu waliostaarabika. Hio ndio silaha ya kwanza.

Ya pili sipendagi vurugu vurugu kwahio sijiweki katika mazingira ya kutibuana na watu. Nahakikisha marafiki na jamaa ni wengi kuliko maadui.
Kuna nyumba nimeiona Mbezi Beach hajaweka grills bali madirisha tu na elwctric fence, cctv, SGA security
 
Majambazi hawavamii mtu wa kawaida, majambazi wanavamia wafabiashara au mtu ambaye ameuzwa na informer wao kama kuna pesa ndani.

Wezi wengine waliobaki kutokana na maendeleo ya teknolojia ni wezi wa timing ambao wanaspray Dawa ya usingizini shida yao kubwa ni flat screen tu.

Kwa sasa wezi wa kuvamia kundi ndani ya nyumba bila kujuwa wanakwenda kuiba nini labda maeneo ya ushenzini sana ambalo mtu hupaswi kuishi maeneo hayo au maeneo yenye makazi mapya nyumba bado ziko mbalimbali napo si sehemu Salama kuishi.

Kwa sasa ni muhimu sana kuwa na mifumo ya teknolojia ya camera na alarm hii itakusaidia hawa wezi wa timing kuwadhibiti.

Watu wenye mtihani wa self ni defence ni matajili na wanafañyabiasha hata ukiwa na bastola na bunduki bado unahitaji mifumo mingi ya kujilinda.

Kuna Mzee mmoja wa Kizaramo mitaa yangu ana maduka makubwa tu na hajawahi kuvunjiwa kuna simulizi zina sema ameyazindika, lakini mwaka Jana walimlia timing na Bodaboda ile ametoka bank tu anashuka kwenye gari baraza ni akawekwa ranch zilipigwa risasi tatu akamuuliwa akabidhi ile bahasha kubwa yenye akatii Amri jamaa wakabeba bahasha na Bodaboda yao wakasepa.

Kwahiyo hata kwenye mabenki nadhani kuna tatizo possibly mtandao wa majambazi unaanzia benki.
 
Kuna nyumba nimeiona Mbezi Beach hajaweka grills bali madirisha tu na elwctric fence, cctv, SGA security
Grill zinaharibu shape ya nyumba, material za hiyo milango na madirisha waweza kuta drill zinasubiri.

Huyo ni mtu anaona mbali, kwa sababu wakidhamilia kuingia ndani wanakuja na mitungi Midogo ya gesi grill inatolewa fasta tu wanaingia ndani, na kuna ile mikasi mkubwa inakata mpaka nondo.

Kikubwa kwenye maisha maintain low profile, na kama unataka uwe high profile basi uwe na pesa kweli unalindwa na system zote camera na security guards wenye silaha.

Kuna tajiri mmoja kariakoo anaitwa Imma mchaga wa Rombo amekaa sana kwenye nyumba za pale keko ambazo zimeingiliana na Polisi barracks kwa sababu ya usalama wake lakini hakuwa na hadhi ya kuishi keko.
 
Waweza weka pia chombo kama beseni chenye maji chumvi ,ukakipiga short pia ili muhuni wa kwanza akutane na uchawi wa mzungu,ukilegeza mmoja wengine wanapotea
Pumba pumba pumba.

Kwamba kila siku ukitaka kulala unajaza maji na chumvi kwenye beseni unaliweka mlango wa chumbani! Halafu unaweka waya wenye moto!

Kila siku????
 
Grill zinaharibu shape ya nyumba, material za hiyo milango na madirisha waweza kura drill zina subiri.

Huyo ni mtu anaona mbali, kwa sababu wakizamilia kuingia ndani wanakuja na mitungi Mdogo ya gesi grill inalewa fast a tu wanaingia ndani, na kuna ile mikasi mkubwa inakata mpaka mondo.

Kikubwa kwenye maisha maintain low profile, na kama unataka uwe high profile basi uwe na pesa kweli unalindwa na system zote camera na security guards wenye silaha.

Kuna tajiri mmoja kariakoo anaitwa Imma mchaga wa Rombo amekaa sana kwenye nyumba za pale keko ambazo zimeingiliana na Polisi barracks kwa sababu ya usalama wake lakini hakuwa na hadhi ya kuishi keko.
Watanzania tubadilike, tuachane na grills tuwekeze kwenye mifumo na walinzi hata wa 300000 kwa mwezi
 
Habari Extrovert

Mbona leo umeni disappoint kinoma!

Umeandika pumba kishenzi 😅 😅

Mbona hata sehem za ushuani majambazi huwa wanavamia kama kawa!

Msela wangu Hassan alivamia Goba.

Francis jembe langu alivamiwa Kimara Temboni (ingawa hakuwepo siku hiyo)

Kigamboni matukio ya kutosha!

Tena afadhali ushwahilini wanaingia vibaka wavaa yeboyebo.

Ushuani, majambazi/wezi wanaingia na silaha kabisa.

Kwamba kuishi vizuri na watu, ndio Kinga ya kutovamiwa?

Kwamba majambazi ni wale watu wenye ugomvi na wewe?
Kuna kitu kinaitwa "Mitigation of risks" hauwezi kuzizuia hatari ila unaweza kutengeneza mazingira ya kuziepuka to some extent.
 
Umenena hapo, maana sikuhizi hata simu za mifukoni zina tochi.

Ila kuna mdau kachangia kwamba silaha yake mojawapo ni tochi yenye mwanga mkali, nadhani kwa tuliowahi kusoma shule za boarding tunajua zilivyotumika, usiku taa zikizimwa mtu akipigwa mwanga mkali anakula mikanda bila kujua inatoka wapi
Kuna tochi maalumu ambayo ukimulikwa nayo machoni huoni unaona maluweluwe nusu saa nzima,walikuwa wanatumia wanajeshi wa Marekani,sijui kama zimeishafika kwenye masoko kama Amazon.
 
Back
Top Bottom