Wanaume tuelimishane ulinzi, ni silaha gani nje ya bunduki ni nzuri kuimiliki sehemu unayoishi?

Wanaume tuelimishane ulinzi, ni silaha gani nje ya bunduki ni nzuri kuimiliki sehemu unayoishi?

Umenena hapo, maana sikuhizi hata simu za mifukoni zina tochi.

Ila kuna mdau kachangia kwamba silaha yake mojawapo ni tochi yenye mwanga mkali, nadhani kwa tuliowahi kusoma shule za boarding tunajua zilivyotumika, usiku taa zikizimwa mtu akipigwa mwanga mkali anakula mikanda bila kujua inatoka wapi
Hapo sawa mdau
 
Chukua mfano wavamiaji wameishafanikiwa kuingia sebuleni wewe upo chumbani ama upo na wanafamilia chumbani, kwenye situation kama hiyo ni silaha ipi nzuri kukabiliana na wavamiaji?

Binafsi nina rungu kama la komredi kipepe kwa mashambulizi ya ana kwa ana man to man, lakini ningependa tuelimishane zaidi.

Kupitia uzi huu tuelimishane silaha za kuwa nazo, kuzificha, matumizi sahihi, n.k.
Kanunue kifaa wanachotumiaga polisi kupiga shoti mtu..vinauzwa siku hizi..kariakoo vipo kibao..!!
 
Mungu ndie mlinzi wangu na wa nyumba yangu.
Mtegemeeni Mungu kwa kila jambo...

Mkishimdwa kumtegemea Mungu basi tumieni uchawi..

Sasa wewe uko peke yako afu njemba kama kumi zenye uzoefu wa ujambazi zikiwa na silaha za kisasa na za jadi.... unategemea utatoka na kipanga chako ukawakabili afu utoke salama?
 
Well umeongelea manati ni sawa yanaweza kukusaidia kwa mbali,lakini chukua mfano wameishafanikiwa kuingiza sebuleni wewe uko chumbani, kwenye situation kama hiyo bastola ni muafaka haswa kama umejificha kwenye Kona fulani unawadondosha mmoja mmoja, lakini swali je ni Kila mmoja wetu ana sifa ya kumiliki bastola jibu ni hapana,

trick inayoweza kukusaidia ni kuwa na switch inayoweza kuzima umeme nyumba nzima, halafu unavaa miwani Yako ya night vision, huku umeshika chupa ya plastic ya nusu Lita, zile za maji ya kunywa, ikiwa imejaa maji yaliyochaganywa na pilipili ya unga Kali kabisa kifuniko kikiwa kimetobolewa tundu dogo unene wa njiti mbili za kiberiti, kwa sababu hawakuoni wewe unawaona unawaminyia maji ya pilipili kwenye macho, wakati wanafikicha macho unamaliza game na silaha za jadi halafu unawasachi mifukoni kama walitembea na hela'then unaripoti tukio kwa vyombo vya usalama.
Pilipili umemamliza Kila kitu, Mimi huwa sikosi Acidic ndani kwa hio huwa namaliza, nina chemicals za hatari sana ambazo nawadondosha taratibu
 
Binafsi najua sana kutumia silaha na ngumi za ana kwa ana nashauri mazee kuwa na silaha pekee sio tija ila tujue namna za kuzitumia kwa kumjeruhi mbaya wako

Ndani nna kisu kimoja hatari sana
 
Chukua mfano wavamiaji wameishafanikiwa kuingia sebuleni wewe upo chumbani ama upo na wanafamilia chumbani, kwenye situation kama hiyo ni silaha ipi nzuri kukabiliana na wavamiaji?

Binafsi nina rungu kama la komredi kipepe kwa mashambulizi ya ana kwa ana man to man, lakini ningependa tuelimishane zaidi.

Kupitia uzi huu tuelimishane silaha za kuwa nazo, kuzificha, matumizi sahihi, n.k.
mungu alijua ayo mambo yapo ndomaana akakupa sauti. iyo ndo silaha kubwa kuliko zote.

si unaonaga mtoto akizaliwa ni lazma alie kwanza? sasa iyo ndo silaha namba moja zingine zote zinafata baadae.

iyo sauti yako ndo silaha kubwa! km una sauti ndogo tumia filimbi!

wale wahalifu wa usiku ukiwapigia makelele lazma wapoteane.
 
Silaha yangu kubwa ni kutokuishi Keko, Temeke, Vinguguti, Tandale, Mbagala na maeneo yote yasio na watu waliostaarabika. Hio ndio silaha ya kwanza.

Ya pili sipendagi vurugu vurugu kwahio sijiweki katika mazingira ya kutibuana na watu. Nahakikisha marafiki na jamaa ni wengi kuliko maadui.
 
Chukua mfano wavamiaji wameishafanikiwa kuingia sebuleni wewe upo chumbani ama upo na wanafamilia chumbani, kwenye situation kama hiyo ni silaha ipi nzuri kukabiliana na wavamiaji?

Binafsi nina rungu kama la komredi kipepe kwa mashambulizi ya ana kwa ana man to man, lakini ningependa tuelimishane zaidi.

Kupitia uzi huu tuelimishane silaha za kuwa nazo, kuzificha, matumizi sahihi, n.k.
do not carry a weapon "be a weapon" kacheze taekwondo"
 
Back
Top Bottom