Wanaume tunaopenda kuwa smart tusikose package hii

Mtu anayefanya kazi za mikono, inachafuka. Au mwalimu na Chaki. Anafanyaje kuweka mikono yake smart?
Hawawezi kukuelewa, unakuta mtu amevaa vizuri ila vidole vya mikono vinatoa harufu ajabu. Mtu anayejitambua hawezi kukubali mikono iwe na hali hiyo.

NB: Hayo uliyoyaita mafuta huwa yanatumika sehemu gani ya mwili?.
 
Mwasibu CPA uchwara SUNZU BOBAN OKW umehamia huku tena?
 
Sisi wanaume ambao hatuchagui mpaka povu la sabuni ya unga tunaogea mnatuweka kundi gani, kuna kuna kina sisi tunaooga chukuchuku kama hakuna sabuni, ama tunaita kujimwagia maji.

Ila kiukweli kabisa, mambo ya kupaka lotion ama mafuta kumenikalia kushoto mnooo, siwezi kabisa, na sijawahi kutoa hela yangu nikanunua lotion,
Mke wangu alijaribu jaribu mwanzoni, akaona huu mti mkavu kwenye suala la kupaka mafuta ama lotion nimemshindwa.
Mie ni body spray tu baasi.

Labada niende mkoa wenye baridi sana, na huko sipaki mafuta mwilini, ni mdomo tu sababu huwa unachanika chanika.
 
Hivi kwa joto hili watu mnapaka lotion kweli
 
Yani kabisa Mkuu unatumia muda wako kunifafanulia kuhusu vipodozi mimi? Umenichekesha sana, mie ni jabali hakuna utakachoniambia kwenye hii sekta.

Huyo niliyemuita anatumia products nyingine bora zaidi ya hata hiyo Dove, na tulishazungumza kwa alipo na nikamwambia vya kutumia.

Good day.
 
Nipe packages ya pamba.

Sabuni natumia ya Unga/Kipande ya kufulia.
 
Bora useme wewe! Mimi wameniita mshamba
Mwanaume na hand cream loooh🙌
Hand cream ni hapana na nimemwambia mtu hapa loud & clear, huo mstari asiuvuke.

Kuna products naweza kumuelewa, face wash, showe gel, moisturizer za kiume zipo kibao, deodorant & perfumes zote awezavyo.

Ila serum, toner, hand cream, sunscreen, lip balm, face mask zimpite mbali.
 
Hadi sunscreen mbona unamuonea😂
Mimi sijawahi kununua sunscreen hua nategea ya babe wangu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…