Wanaume wa kiislam hii inawahusuu

Wanaume wa kiislam hii inawahusuu

Kwangu mimi dini ni katiba yenye kuonyesha taratibu na tamaduni za eneo husika, miongozo hiyo ilitegemea pia aina ya maisha kijamii, kimazingira na kiuchumi ni fikra pana za wachache wenye akili waliosimika tawala hizi za kiitikadi za kuabudu Miungu, inaonyesha watu hawa walikuwa wanatambua ili jamii hii tuitawale au itawaliwe basi ipewe miongozo. Baada ya itikadi kusimikwa hata mataifa yakapenda kuweka sheria za kuongoza watu hata leo ndio maana kuna katiba za kuongoza nchi na nchi, maeneo na mazingira yao ndio maana kila uchao sheria mpya zinaibuka ili kuendelea kulinda,kutawala na kuongoza watu.
Wakristo & Waislamu, Wapagani hata Buddhism nk wote wana miongozo ili kulinda,kuongoza,kuepusha na kutetea jamii zao unfortunately muafrika hakubahatika kusimika chochote kwasababu alikubali kuacha tamaduni yake sababu ya uvivu wa kufikiria akabeba tamaduni za kigeni zilizoletwa na waarabu pamoja na wakristo nia yao wote ni kutawala jamii sizizo na miongozo mfano halisi waafrika sisi dhahiri hatukuwahi kujidadisi na kujipangilia.

1. Wamagharibi waliona watu wao wanatabia zipi, jeografia yao na shughuli zao za kiuchumi, hivyo kitendo cha kuvaa pete ni ishara ya kuonyesha ya kwamba tayari uko na mwenza si halali kwako kuwa na mwenza mwingine nia ni kuilinda jamii dhidi ya watu wasio waaminifu, walaghai pia kuepuka ueneaji wa maradhi ya kingono yanayochochewa na ushawishi kati yetu hivyo mlaghaiwa ataweza jiepusha na uzinzi usio na tija hilo sasa lilikuwa ni wazo zuri sababu binadamu ni kiumbe anayebadilika badilika, wakristo kimaono yao wakaona muoaji tumpe alama, kinga ni bora kuliko tiba..rejea amri 10 za Mungu nia ilikuwa ni kuongoza jamii iliyoonyesha tabia fulani fulani hivyo ili kui' regulate ili hitaji miongozo ambayo ilikuwa mizuri.

2. Kupiga marufuku wake wengi nia ni kuzuia tamaa, ueneaji wa maradhi hatarishi toka kwa mtu mmoja asiye na alama ya utambuzi kama ana mwenza tayari ili hasimlaghai jinsia nyingine washiriki zinaa lakini pia nafsi imeumbwa na wivu uliojaa ubinafsi kutopenda kuchangia penzi na binadamu mwingine waliona hili ndio maana leo hii watu uuana sababu ya usaliti wa kimapenzi kuna matukio mengi sana kila siku nafsi haiwezi vumilia usaliti...mtu yupo ndoani lakini michepuko kibao sababu kuu tamaa & kipato nk. Tambua sababu ya kipato ni umasikini na mtindo wa maisha.

3. Waarabu waliona watu wao kitabia, jeografia yao na shughuli zao za kiuchumi wakatengeneza modality za kikwao. Kuoa wake wengi ni baada ya kuona mtu kaoa lakini bado anapepesa macho nje ilikupunguza tamaa basi aoe wake wanne wa aina tofauti ili tu kumridhisha kwasababu waliona haiepukiki kesi ni nyingi, sometimes sheria huja kutokana na wingi wa shutuma au kulegeza au kukazia jambo husika.
Jamii kuvaa niqab,ushungi nk na kutawaza wakati wa kuingia ibadani sababu kuu ni jeografia na urembo na kiafya, sehemu kubwa ya Asia ina ujangwa na joto lakini hawakujali sababu usiku kulikuwa na baridi kali,wingi wa upepo na vumbi jamii ikaona bora kuweka kizuia vumbi na mchanga kwa kuvaa niqab kwa wanawake na watoto wa kike sababu ya urembo na kiafya, pia wanawake sio wafanyakazi ngumu lakini pia kimaumbile wanawake ni tofauti na wanaume, hutamanisha wanaume hivyo bora pia kuyaficha ili kuepusha au kupunguza ushawishi wa kimapenzi, huu utamaduni waafrika hatukuwa nao tumeletewa tu tukaubeba tena tunavimba kabisa kumbe imani pandikizi tu sisi tulivaa ngozi za wanyama, imani zao leo hii zimedumu vizazi na vizazi na baada ya kupata maarifa mtu mweusi kazikomalia cha ajabu yeye hakuwa na utaratibu wake wenye maono yajayo [emoji23]

4. Kutawaza wakati wa ibada na kuvaa kanzu fupi, jamii nyingi za Asia sehemu kubwa uchumi wao enzi hizo ulitegemea ufugaji na umiliki wa mazizi hivyo mtu huyu sehemu kubwa ya maisha yake atakanyaga kinyesi cha wanyama pia wakati mwingine atabeba wanyama hivyo atatoa harufu kali mwilini wakati wa ibada kiustaarabu bora anawe wakati wa kuabudu kupunguza kero kwa wengine walio ibadani, huu ustaarabu waafrika hatukuwa nao sababu shughuli zetu za kiuchumi hazikuwa ufugaji bali kilimo ndio maana tuliabudu mizimu ili kuomba mvua tu.

5. Tuna mazuri yetu kitamaduni ambayo yangeweza kuwa sehemu ya dini ya kiafrika mfano mwanamke akiwa mjamzito asile vitu vinono atanenepa yeye na mtoto kuzaa itakuwa shida njia itakuwa ndogo mtoto ataongezeka ukubwa hivyo anaweza poteza maisha hili lilikuwa wazo lenye maono sababu vifo vilivyo tokea zama hizo wakati hawana teknolojia ya upasuaji viliwapa wakati mgumu kutatua changamoto ile sababu walipoteza wanawake wengi, amini nakwambia wazo hili lingelikuwa kwenye msahafu au biblia tungeikomalia waafrika, bado naamini vitabu hivyo vya kuweka ustaarabu na miongozo ya kimaisha ya mwanadamu kuna mazuri yake na mengine sio Sahihi sababu hatuna mazingira rafiki na huu sio wakati sahihi kuyakubali.

6. Maisha yamebadilika waafrika kwakuwa bado hatujaamua tumia maarifa yetu tumebakia kuwasikiliza waliotuletea itikadi zao za kidini, kibiashara na kimtindo wa maisha bado wanatupelekesha tazama leo hii taasisi za dini kama bakwata na wachungaji walifanya ibada ya kuomba mvua [emoji23][emoji23]
Wakati wenzetu wanatumia kilimo cha umwagiliaji wanatulisha sisi wameshatoka kwenye kufanya ibada za kuomba mvua ambazo bado mtu mweusi anazo, ni dhahiri hatuna maono ya kutafuta njia mbadala sisi tumekomalia dini na yale waliyotuachia tukiamini bado tunahitaji miongozo yao [emoji23][emoji23] ndio maana leo hii whites are pressurezing us tuukubali ushoga ilihali wanajua sio utamaduni wetu, wanajiamini sababu kama tulipokea dini zao why not kwa ushoga ndio maana walianzia kwenye haki za binadamu ili tuingie mtegoni kwanza. Naamini Mungu yupo ili hizi dini naamini zilikuwa ni kwa faida zao tu.

Nb: Mungu alimuumba binadamu mfano wa package iliyokamilika yenye kutambua changamoto ya kila jambo na kulitafutia utatuzi ili aishi vyema, la msingi tu tutambue yupo aliye nyuma yetu ambaye ametuumba
 
Back
Top Bottom