Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Wakuu
Mwenyekiti wa kijiji cha Mloda kata ya Mlowa barabarani, wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma, Adam Philemon amesema miongoni mwa malalamiko yaliyokithiri katika kijiji hicho ni wanaume kunyimwa unyumba, huku akiwataka wanaume kutoa taarifa za vitendo hivyo kwenye sehemu husika ili kutokomeza janga hilo.
Philemon pia alibainisha kuwa wanaume wanaendelea kunyanyaswa na wake zao hasa wenye vipato vikubwa, hasa kipindi cha mwisho wa mwaka wanapovunja vikoba vyao. Aidha, wanawake wa kijiji hicho, wakiongozwa na Mariam Mahajile, wameeleza kuwa changamoto hizi mara nyingi husababishwa na wanaume kushindwa kuwajibika kifamilia au kuwa na uhusiano nje ya ndoa.
Nuru Mpanda kutoka Jukwaa la Wakulima Wanawake amewashauri wanawake kuwaheshimu waume zao hata wanapokuwa na vipato vikubwa, huku Mratibu wa Mradi wa TIF, Happy Itros, akielezea juhudi za mradi huo katika kusaidia wakulima wadogo hasa wanawake katika kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi kupitia kilimo endelevu.
Mwenyekiti wa kijiji cha Mloda kata ya Mlowa barabarani, wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma, Adam Philemon amesema miongoni mwa malalamiko yaliyokithiri katika kijiji hicho ni wanaume kunyimwa unyumba, huku akiwataka wanaume kutoa taarifa za vitendo hivyo kwenye sehemu husika ili kutokomeza janga hilo.
"Na kuna kesi moja ya mwanamke alikuwa hampi mume wake unyumba na haki hiyo anampatia mtu mwingine ambaye sio mume wake yaani ni kama anaishi na mume lakini unyumba anapewa mtu mwingine."
"Mwezi huu wa Desemba wakati akina mama wanavunja vikoba vyao tumekuwa tukipokea malalamiko mengi ya wanaume kunyanyaswa na wake zao sisi kama serikali tunayapata sana malalamiko haya kutoka kwa wanaume wengi," amesema Philemon.Nuru Mpanda kutoka Jukwaa la Wakulima Wanawake amewashauri wanawake kuwaheshimu waume zao hata wanapokuwa na vipato vikubwa, huku Mratibu wa Mradi wa TIF, Happy Itros, akielezea juhudi za mradi huo katika kusaidia wakulima wadogo hasa wanawake katika kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi kupitia kilimo endelevu.