Wanaume wakati mwingine mnataka tuwaroge

Wanaume wakati mwingine mnataka tuwaroge

So sad, sijawahi kuwaza kufanya hivi ila hapa nilipofika sina namna, otherwise nachanganyikiwa bure. Huu ni mwaka wa tatu wa ndoa, na miaka miwili ilikuwa ya furaha na amani hadi mwaka wa tatu ulipoanza, nimeona mapicha picha ya kila namna kutoka kwa huyu mwanaume.

Nimekonda nimechakaa kiufupi sina nuru hata biashara na kazi zangu zimeyumba sana. Miaka mitatu ya ndoa sijawahi kuchepuka hata kuwa na ukaribu na mwanaume yoyote, namuheshimu mume wangu.

Ni mwanamke ambae mwaka mmoja uliopita hata ungeniletea ushahidi mume wangu anachepuka nisingekuamini, namna nilivyokuwa na imani nae[emoji28].

Sasa kwa matukio ninayopigwa toka mwaka jana kufuma nguo za wanawake, condom na takataka nyingi kwa huyu mume amenifanya moyo kuwa mgumu, kila unapomfuma anakumbembeleza lakini baada ya week chache mambo ni yale yale.

Nimeamua sasa ni deal nae kwa namna nyingine, maana sasa nashindwa ku concentrate na mambo yangu mengine ya muhimu.

Ni kweli hakuna mwanaume asiechepuka nimekubali, Ila kuna wanawake hatuwezi kuvumilia huu ujinga bora awe ndondocha kuliko haya maumivu.

Nimempiga makombora matatu makali, moja kafungwa kwenye chupa hatakuwa na kauli kwa lolote kuanzia sasa, ataona wanawake wengine ila ataniwaza mimi tu na hatosimamisha kwa mwanamke mwingine.

Nampenda sana mume wangu ila tabia zake zimetufikisha hapa. Wanaume kuweni makini, nyie ndio mnatubadili tabia zetu kwa matendo yenu.

Haya wale wa mapovu mje mnipopoe, ila for once toka mwaka uanze nimepata amani ajabu, kuanzia sasa mume ni wangu peke angu.
Kubalini tu uke wenza muishi kwa amani........ Umeenda kuweka password huku mwingine nae kamuwekea acha jamaa awe ndondocha kwakweli........ Mama mzazi tu ndo mmoja mengine mbele kwa mbele
 
Hii mimi nakwambia serious kuwa sio wanaume wote huchepuka. Binafsi nimewahi kuishi na mwanamke wangu kwa miaka 18 bila kuchepuka, nilimpenda, nilimheshimu, nilimpa kile nilichopata lakini kwa sasa tumeachana tunatimiza miaka 2 mwezi ujao.
Usiseme hakuna mwanaume asiechepuka.
 
Walahi vile uchawi haufanyi kazi ni utapeli.....sitoelezea ila ngoja uone kaa atabadilika kwa hicho kimbola.

Akibadilika uje uniambie
Mkuu ukisema uchawi haufanyi kazi jua hujakutwa, mshukuru Mungu, tunza hili akilini.
 
Matatizo kama haya ndyo yaliyomfanya yule DJ wa Kenya aone Bora amrekodi mtu anayejitoa uhai ni pasua kichwa Hawa wanawake.Bora kuweka sumu standby kabisa wanywe .KATAA NDOA.

##NYWA
 
Faida ya limbwata ni mwanaume kupoteza uwezo wa kutimiza majukumu yake, jiandae kuwa mume.



Ni kweli na wengine huharibu kazi , anakuwa hataki kwenda kazini anataka kubaki nyumbani tu mwisho anakuwa jobless.

Na mama Kama ni wanyumbani au Mwalimu ndio ujipange kulea familia usimkimbie Mwanaume wa watu maana umeyataka mwenyewe [emoji108]
 
Hii mimi nakwambia serious kuwa sio wanaume wote huchepuka. Binafsi nimewahi kuishi na mwanamke wangu kwa miaka 18 bila kuchepuka, nilimpenda, nilimheshimu, nilimpa kile nilichopata lakini kwa sasa tumeachana tunatimiza miaka 2 mwezi ujao.
Usiseme hakuna mwanaume asiechepuka.
Khaaa Sasa mmeachanaje Tena jamani....
 
Back
Top Bottom