Moisemusajiografii
JF-Expert Member
- Nov 3, 2013
- 43,960
- 77,533
Sasa,hayo maarifa ya kisaikolojia ndiyo uchawi/ulozi mwema unaotakiwa katika jamii.Kuna ya kujiuliza.Je,watu huwa wana uelewa/mbinu njema za kuishi na wenza?Ametokea makuzi gani?Anawachukuliaje watu ambao ni jinsi tofauti na yake?Anao uvumilivu na kumchukulia mwenza kwa asili kitabia au amejifunza ukubwani?Huwa anayachukuliaje mambo yakitokea ambayo yeye aliamini hayawezi kutokea kinyume na matarajio yake?Anachukulia au kufananisha kuishi au kuwa na mwenza ni kama kitu gani?Mambo ya kiimani(dini) anayo kwa kiasi gani?Tukipata jamii inayoweza kujibu hayo positively,at least,tunaweza kuongea lugha moja.Yanahitajika maarifa ya saikolojia ya mahusiano.
Kuna ombwe kubwa sana kwenye jamii zetu.