Wanaume wanaokataa ndoa wana matatizo yafuatayo...

Wanaume wanaokataa ndoa wana matatizo yafuatayo...

sanalii

JF-Expert Member
Joined
Oct 1, 2018
Posts
1,639
Reaction score
5,767
1. Wamekulia katika familia zenye migogoro ya ndoa hivyo wana experience mbaya (Adverse Childhood Effect).

2. Ni wachoyo au waoga wa maisha wakiamini wakioa watakua na majukumu, au maisha yatakua magumu hawatayamudu au mke atatumia mali zake.

3. Wanauelewa mdogo wa binadamu, wakiamini ili waoe basi wapate mtu ambae hatakua na dosari hata moja, huu ni ujinga, hakuna aliekamilika.

4. Hawana imani ya dini na wamejihalalishia zinaa.

5. Ni malimbukeni wa kufata mkumbo.

6. Wao wenyewe ni wenye tabia mbovu, hivyo kila wanaemuona wanaamini anatabia mbovu kama za kwao.

7. Wanauwezo mdogo wa ku jaji mambo, wakiona mwenzao anasumbuliwa basi wanamini nao itakua hivyo, au waliumizwa huko mbeleni.

Kwanini ni muhimu mwanaume kuoa?
1. Kupata watoto na kuwatengenezea umoja, kuwa na watoto bara na pwani, kila mtoto na mama yake, ni chanzo cha mgawanyiko wa familia nyingi. Unapooa unatulia na familia yako.

2. Kupata safe sex na halali, unapooa, unasex kwa halali na unakua na uhakika wa uwena wake na usalama, hamsaidii mwanaume kusex na wanawake hivyo hovyo.

3. Kupata mashirika wa karibu, kitu amambacho wanaume hawajui, kadri unavyozeeka ndo unahitaji mtu wa karibu sana kua na wewe, mtoto wako wa kike au wakiume hawezi kukuhudumia ukishazeeka, mke wako atafanya hivyo. Pia ni raha kuwa na mwandani wako mnaeshare mambo yenu mbali mbali.

Kuna mambo nakubali si ya kuvumilia hata kidogo, hasa suala la usaliti, lakini kwa asilimia kubwa mambo mengi ni kuvumiliana, hakuna aliekamilika na hatatokea, cha msingi ni kupata ambae anamapunguvu unayoweza kuyavumilia, pia uamini pia wewe mwenyewe unamambo ambayo mwenzio anakuvumilia.

Ndoa ni raha, ndoa inaleta utulivu.

My dedication to my beloved wife is " One friend" by Dan Seals
 
Hyo namba 1 hapo iliniathiri tokaa nikiwa na miakaa 5 nilikuwaa namwonaa b mkubwaa akimnyanyasaa mzee mpk mzee aliamua kujinyongaa kuondokana na KERO ya mama yetu na mwanamke yule baada ya mzee kujinyongaa hakukaa hata miez miwilii likaolewa na kijana ambayee umri n sawà na kaka ytu wa Kwanzaa nakututelekezaaa Moja kwa mojaa mpk leo,alafuu uniongopee kuhusu wanawakeee na nioee ili nipitiee manyanaso ya mzee aliyopitiaa kwa mama yetu. Aiseeeeee hapana ndoa ni utumwa.
 
Wanaume wa Jf watakuja kukupopoa sasa hivi. Wanajazanaga ujinga hivi hivi😂😂😂 na wengi wanaoanzisha mada za msioe ni wale waliooa na wana familia zao zinaenda vizuri tu. Na mapoyoyo wanaoitikia ni wale ambao vischana vyao vinaliwa na hao waume za watu😂😂akili kumkichwaaa
 
Wanaume wa Jf watakuja kukupopoa sasa hivi. Wanajazanaga ujinga hivi hivi😂😂😂 na wengi wanaoanzisha mada za msioe ni wale waliooa na wana familia zao zinaenda vizuri tu. Na mapoyoyo wanaoitikia ni wale ambao vischana vyao vinaliwa na hao waume za watu😂😂akili kumkichwaaa

Mwanaume anayeogopa kuoa ni mwanaume wa kuogopwa.....yaani ni mwanaume anayeogopa kuwa mwanaume
 
Hyo namba 1 hapo iliniathiri tokaa nikiwa na miakaa 5 nilikuwaa namwonaa b mkubwaa akimnyanyasaa mzee mpk mzee aliamua kujinyongaa kuondokana na KERO ya mama yetuu...na mwanamke yule baada ya mzee kujinyongaa hakukaa hata miez miwilii likaolewa na kijana ambayee umri n sawà na kaka ytu wa Kwanzaa nakututelekezaaa Moja kwa mojaa mpk leo,alafuu uniongopee kuhusu wanawakeee na nioee ili nipitiee manyanaso ya mzee aliyopitiaa kwa mama yetuu,,,aiseeeeee hapana ndoa n utumwaa
Kwahiyo ndio mnakujaga kuanzisha uzi wa kutukana wanawake kwa experience mlizoona kwa mama zenu?

Basi ndio nimeelewa sasa , nikiona mtu ameanzisha mada ya kutukana mwanamke au kukashfu ntaelewa kayaona kwa mama ake basi anadhani wanawake wote wako hivyo.

Na sisi tuwe tunawa grade wanaume wote sawa. Kwamba baba anabaka mtoto wake wa kumzaa basi wanaume wote ndio wako hivyo. Wababa wangapi wametelekeza wake na watoto kwa ujinga wao. Kwahiyo tuwa group kwamba ni wanaume wote duniani wako hivyo.

Pole kwa yaliyokukuta ila mama yako sio kama wanawake wote.
 
Kweli kabisa mkuu familia ni kitu Cha mhimu Sana katika maisha ya binadam,mfano mm familia ilisafiri likizo hii ya krismas yaani maisha yalikua magumu sn linyumba unaona halina maana hata kurudi nyumban unaona uvivu,ukizeeka pia familia yako ndio ya kupambana mpaka mwisho ndugu wanaweza wasionekane ila hauwezi ukamtelekeza mzazi labda unatafuta laana.
 
Back
Top Bottom