Wanaume, watoto wako hawawezi kukugeuka ikiwa ulishiriki malezi Yao tangu mwanzo

Huu ndio uhalisia na tunatakiwa Kuishi
Kuwa baba ni uhalisia wa matendo Yako Kwa wanao otherwise utaambiwa ulitoa mbegu tu
Alafu
Bond ya mama na watoto ni ya asili kabisa
Yani hata ukute mama mlevi watoto wanajipikia utasikia ndio mama yetu Sasa tunafanyaje 😀
Baba awe mlevi Sasa khe 😃😃😃
 
Last weekend tar 6 jumamos, tulikua tunapiga stori za hapa na pale na madogo, nikaanza kuwasimulia namna ambavyo sisi tukiwa katika umrinkama wao zaman tulilelewa vipi.

Nikawa nawaambia namna tulivyokua tuna develop skills katika michezo yetu ya utotoni tofaut na wao.

Nikawaambia zaman sis wengi hatukua na uwezo wa kununuliwa toys za magari hivyo watoto wa kiume tulikua tuna uwezo wa kutengeneza magari yetu wenyewe kwa kutumia malighaf zinazotuzunguka na tunayaendesha kwa kuyakokota for kilometers.
Magari ya mbao
Magari ya waya
Magari ya bati/makopo.

Nikawafundisha kwa kuwaonyesha namna tulikua tunafanya kwa vitendo siwezi kuweka clip hapa but nikakusanya makopo yoote matupu ya maziwa for demonstration...

Dogo akasema "tengeneza Kirikuu kama hayo unayosema ni ya kweli" 😂



Wakawa very inspired.
 
Mimi Niko tofauti kidogo kwakweli sipo na ukaribu sana na watoto but watoto wangu nawachukulia kama roho yangu...!

Na Nina jitahidi sana watoto wangu wasiishi maisha kama niliyo ishi...!​
 
Rudiana na mama yao
 
Umecheki DNA lakini?
Sina haja ya kucheki DNA kitanda hakizai haramu, kupiwa hakukwepeki, tulio enda jando wazee wetu walitufundisha ukirudi nyumbani toa taarifa...!

Hivyo ukilielewa Hilo somo utagundua kuwa mambo ya kuchapiana yalikuwepo tokea dhama za kale ila wenzetu walichapiana kwa kuheshimiana...!​
 
Nawapenda sana kwakweli najitahidi kupambana usiku na mchana...ili watoto wangu wajione kweli baba wanae...!

Kitendo Cha kuwatafutia ilikuwa Raha, kwenye malezi tupate Raha pia🤣🤣🤣​
🤣🤣🤣🤣
 
Huu ndio uanaume sasa...! Wanaume tuuishi uanaume kwa vitendo
 
Mimi wa kwangu kwake sipakumbuki. Na hajui nafanya nini, exactly naishi wapi na nilisomaje. Mambo yangu simwambii maana huwa hayatiki, nikimwambia kitu tu lazima nifeli sijui huwa anayasema kwa wenye nia mbaya.
Kwann Sasa
 
Changamoto ni watoto wetu wa michepuko hasa wakiwa wavulana. Anataka uishi Nyumba moja na mama yake. Bila hivyo hata ufanye nini, haoni kitu. Mama yake anakuwa anamtumia kama chambo!

Jambo la msingi ni kutimiza wajibu wako kama baba, mengine mbele ya safari. Ila ukumbuke watoto si wa kutegemea uzeeni, akikupa shukuru, akikunyima pambana na hali yako. Nasema hii inaapply kwa multi party, siyo mume aliyezaa na kuishi na mke mmoja!
 
Uko sahihi kabisa, malezi ya watoto sio kutoa pesa tu. Wanaume tumekuwa watu wa kutoa pesa tu, watoto hawajui malezi yetu physically, hatujihusishi moja kwa moja.
 
Iyo ni ngumu kweli aisee
Kunawakat wamama wanapandikiza chuki Kwa watoto au kuwafanya kitega uchumi kupata wanachotak hapa ni kusimsma tu

Ongea na mwanao mara Kwa mara Mpe anachotaka bila kupitia nyuma ya mtu
Msaidie kiakili pia kumpa nasahau mara Kwa mara ajijue yeye ni nani na aweze kujisimamia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…