barafuyamoto
JF-Expert Member
- Jul 26, 2014
- 32,378
- 29,739
Habari.
Wakuu sina lengo la kukashifu watu ila naomba niweke wazi mtazamo wangu kuhusu wanaume wenzangu tulioko MMU.
Kwa muda ambao nimekua mwanachama humu,nimegundua kua wanaume wengi wa humu ni reject mtaani.
Idadi kubwa ya wanaume humu huwa ni kulalamika tu hawakubaliki,wameachwa,hawapati wachumba nk japokua idadi ya wanawake ni kubwa kuliko wanaume,huwa najiuliza hao wanawake wasiopatikana ni wapi? Nimekuja kugundua kwamba vidume wenzangu humu wengi ni reject,hawana sifa wanawake wanazozitaka.
Nenda love connect,mwanamke ataandika anataka mwanaume,akaambatanisha vigezo vichache,tena vya kawaida sana lakini ataishia kukatishwa tamaa na wanaume kua vigezo hivyo ajiumbie mwanaume wake maana hawezi kumpata.
Utakuta mwanamke kaandika anataka mwanaume mrefu,mwenye elimu kuanzia diploma,miaka 30,awe na ajira au kazi binafsi,masharti ya kawaida kabisa,ataishia kuambiwa ajiumbie,najiuliza kweli watu wenye sifa hizo au zaidi hawapo MMU?
Maana yake ni kwamba wanaume wengi wa humu ni wafupi,wasio na kazi,walioishia sekondari.
Sasa nimekubali kwamba wengi wetu humu ni reject.
Cha msingi nionacho hapa ni kwamba ume-FAKE ID na kujifanya mwanaume!! Inauma sana kuwa Ke, umri unaenda alafu unakuwa reject kila kona, sasa umekuja na ujio mpya wa jinsia!
Wewe kama ungekuwa Mwanaume unaletaje hoja ya mwanaume kuwa reject kwa wanawake????
Labda sijui maana ya reject! Ila Ngoja nikwambie kuhusu sisi wanaume, ukitongoza wanawake sita, sio wote watakubali, kwa hiyo, we were made to be rejects at some point inapokuja suala la mahusiano!! Ndo maana tukikataliwa, hatuachi mpaka kieleweke! Sasa kama wewe 'mwanaume' unatongoza mwanamke mmoja, ukikataliwa unakuja kulalamika huku, wewe ni mwanaume suruali!
Vinginevyo wewe ni SUPU YA MAWE weird tafiti zako!
Last edited by a moderator: