Wanaume wengi tunapigwa na wake zetu ila hatusemi

Wanaume wengi tunapigwa na wake zetu ila hatusemi

Juzi ilikuwa sisi wanaume hapa wengi wetu ni rejected huko mitaani ndiyo maana tukakujanMMU kupooza machungu na leo hii ingine eti tunapigwa na wake zetu daaah!

Tunaomba mtuwache tafadhali ehehehehehehe
 
Kama hukuzingatia suala zima la size namaanisha umbo kama umeoa mtu ana uzito kuliko weye watagemea nini? sababu kuna watu wana maumbo madogo anaenda kuoa jimama la nguvu mi naona mpigwe tu.
We mtu unamuowa Chausiku au Mwajuma ndalandefu unategemea nn.. Yaani huyo akikushindwa kwa mangumi anabomoa nyumba apate matofali ya kukutwangia... Au atafusha flampeni ..TV ...deki ... Huku akikutolea maneno mwenyewe utanywea
 
kweli kabisa wanaume wembamba na wafupi kupenda majimama ndio kunawapoza
 
hii haiwahusu nyie wakurya maana iko vice versa mademu wenu wenyewe ndio wanaomba wapigwa japo kofi kabla ya kulala

Hahahahhh,Hahahahhh umenichekesha hiyo japo kofi moja,nitawaletea mada muda si mrefu why wakurya wanapiga wake zao,naamini mtaelewa sababu kuu ni ipi.
 
hahahahahaha heading imenifurahisha! yule mkenya wallahi naanzia wapi kumnyanyulia mkono??? nitakuwa marehemu before, poleni kaka zangu wote mnaotembezewa kichapo kwa ukorofi wenu! na hongera kwa wamama wenzangu, ongezeni dose!
 
Da jamani Mimi wangu Anibondaga sana,mpaka nilishawahi kushonwa,nyuzi tisa
 
Back
Top Bottom