Wanaume wengi wameharibu mahusiano yao bila kujua kwa kufanya makosa haya

Wanaume wengi wameharibu mahusiano yao bila kujua kwa kufanya makosa haya

Infinite_Kiumeni

JF-Expert Member
Joined
Jan 23, 2023
Posts
382
Reaction score
687
Ni muhimu kujua makosa ili usiyarudie/usiyafanye.

Ukishaondoa makosa, kinachobaki ni vitu vizuri. Pia kuna makosa yatakayomfanya mwanamke wako kupoteza mvuto kwako. Ataanza kujitenga nawe. Nawe utaanza kulazimisha penzi mwisho wa siku anakublock, anakunyima penzi au anakuchunia kabisa.

Hivyo ni muhimu kuepuka haya, usije kuumia moyo.
.
Kutumia simu kama chombo cha kujuana.
Kweli simu ni chombo cha mawasiliano.
Kweli simu ni muhimu katika kujuliana hali.
Lakini linapokuja suala la mahusiano, huwezi kuwa na mahusiano na simu. Huwezi kuoa na kufanya mapenzi na simu. Lengo lako ni kuwa na mwanamke pamoja sehemu mnayotaka.
Hivyo punguza kuongea na mwanamke kwa masaa 2. Huo muda tumia kujiendeleza au kusoma. Huo muda tumia kuongeza thamani yako kama mwanaume. Pia huo muda ni heri utumie mkiwa pamoja.

Ukiongea naye sana kwenye simu anaishiwa hamu ya kukutana.
Simu uiweke kwa ajili ya kupanga kukutana.
Mwambie ungependa kuonana naye muongee vizuri, muulize siku na muda atakaokuwa na nafasi.

Kama ni mapenzi muda mrefu/ ya mbalimbali, mikoa tofauti. Unaweza kuongea naye kwa muda kidogo. Lakini isiwe mnaongea kiasi kwamba mwanamke anaishiwa hamu ya kuonana nawe.
.
Kutojiamini katika upendo.
Hili jambo linasemwa kila kona.
Mwanaume jiamini.
Usikae kumuuliza mwanamke wako kama anakupenda kila saa. Au unamwambia “nakupenda” alafu unakaa kusubiri jibu. Au kumuomba akupende. Acha kumwambia mwanamke “niambie basi unanipenda nijisikie amani”.
Acha kumuuliza mwanamke kuhusu nafasi yako. Ni kama vile unamuomba ruhusa ya upendo, jambo ambalo atakuona hujiamini kama unaweza kuwa naye.
.
Kumgeuza mwanamke wako mama ako/ mshauri wako/ bega lako la kulilia.
Kuna kipindi maisha yatakua mrama.
Kuna kipindi mambo yanakua ndivyo sivyo.
Kuna kipindi pesa inakupiga chenga, lakini kamwe usiende kulia lia kwa mwanamke wako. Au kulalamika mbele ya mkeo. Utamfanya ajihisi wasiwasi kama unaweza kuhimili misuko suko. Atakuona dhaifu. Japo utaambiwa mshirikishe mkeo, lakini sio kumlalamikia au kumlilia. Baa, marafiki au washauri wapo kwa ajili hiyo, sio mwanamke wako.
Mwanaume vaa ujasiri.
Vaa ujasiri haijalishi ni jambo gani unalipitia. Ukiona yanakushinda tafuta rafiki yako wa kiume muongee mambo. Wengi huenda baa.

Angalia tofauti ya hawa wanaume wawili.
Wa kwanza. “mke wangu, nimechoka aisee, kazini tumepata hasara na tumefungiwa akaunti ya benki, yani apa sijui tutafanyaje, yani naona kabisa tunafilisika. Sa sjui yule mhasibu naye alikua anafikiria nini kutoa toa tu hela kwa watu mpaka tumefilisika, yani ametuharibia maisha kabisa, ata sielewi hapa …”

Wa pili. “mke wangu yani apa najisikia kuchoka kweli, kazini tumepata hasara na akaunti ya benki imefungiwa, acha kwanza nipumzike kwanza. Kesho najua tutaanza kulishughulikia, lazima tutakua na cha kufanya tu”.
Utaona kabisa kuwa wa pili ameuvaa ujasiri na mke wake anamuona ni mtu anayeweza kukabiliana na changamoto.
.
Kubweteka.
Hali ya mazoea kwenye mahusiano.
Kiasi kwamba hakuna tena mapenzi kwenye mahusiano.
Kuna kipindi kinachoboa kwenye mahusiano.
Ndio maana ni muhimu unapoingia kwenye mahusiano, uwe na kitu cha kukufurahusha tofauti na mahusiano. Na sio mwanamke kuwa chanzo cha furaha yako. Ili usije ukamezwa na kubweteka kwenye kipindi cha mazoea.

Wengi tukishaeka mwanamke ndani tunaona ndo tumemaliza.
Lakini sio kweli, kila siku inabidi umfanye azidi kuvutiwa nawe.
Wewe mwanaume ndo kiongozi, wewe ndo uanze kujichangamsha. Ufanye vitu unavotaka kufanya. Sio kulala na kuangalia TV kila muda. Siku zingine toka na mkeo kwenda kula kwingine. Siku zingine wewe toka nenda mbugani/ sehemu nzuri ukasafishe macho.

Unapobweteka kuna mtu uko anachangamka. Mkeo/ mwanamke wako anaweza kuvutiwa na huyo mtu kirahisi maana maisha yake yana kitu sio matupu.

Unapobweteka pia, mwanamke wako anakosa furaha.

We kazi yako ni kumfanya afurahi akiwa na wewe, kufanya naye mapenzi na kufanya mapenzi yawe mazuri na kumpeti kadri unavyoona sawa. Iyo kazi yako ni mfumo rahisi. Mfumo ambao utakusaidia kuepuka makosa wakati huohuo kuongeza upendo wa mwanamke kwako.
 
Back
Top Bottom