WANAUME WENZANGU: Umewahi kufanya jambo ukaja kujuta baadae kama mimi ninavyojuta mpaka sasa?

Umeongea nilichowaza
 
Inaposemwa wazee wana busara haimaanishi walizaliwa nazo

Ila kuishi kwingi ni kuona mengi na kujifunza mengi

Matukio kama haya yanapotupata au tunapoona yanawapata wengine yanatujengea uzoefu na busara

Mama yako ana uzoefu ndio maana aliona mbali alikwambia umuoe yule binti uliyemtia mimba chuo

Sometimes we have to learn things the hard way
 
Yaap
Huyo binti yako mm nitamsubiri akue nimuharibie maisha kama ulivyoharbu maisha ya mtoto wa watu.

Mpaka unalala na binti wa watu hukujua kuna mimba+magonjwa ya zinaa?

Nyie ndio wasomi hewa hata serikalin hamtakiwi kuwepo maana mtatusainisha mikataba ya ulaghai.

Mrudie mtoto wa watu umuombe mthamaha na hakikisha uwe sehemu ya mafanikio yake kiuchumi+kiafya.

Pumbavu zako.
(JOKE)

Mm najutia kumlala binti ambaye hakuwa my dream wife na kusababisha kuniharibia plan zangu za mbeleni, vijana tuache tamaa za kijinga tujitahidi kucontroll hisia za kijinga[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Daa wee jamaa japo unaonesha kujutia lakini kwa kweli roho yangu imegoma kufunguka as if linanihusu...

Angekua ni hawa mabint wa One night ningesema potelea kote, ila alijitahidi sana ila ukamrubuni kupita uwezo wake..

Ulizingua sana, Mimi msamaha naweka kama hatua ya mwisho,

Tafuta namna ya kumsaidia huyo binti kisaikolojia, Hakikisha unapata hio namna kwa namna yoyote mpka ukingo wa uwezo wako, msamaha kwa baadhi ya makosa ni kelele, kuna mambo msamaha unapokelewa kwa resolution na sio Blah blah...

Ndugu, muelewe kuna mambo kwa sisi binadamu ni ngumu sana kusamehe kwa mdomo, vitendo ndio vinaomba msamaha.
 
Ndio umemuharibia maisha...
 
Pole sana mkuu, ninependa kujua kwanini hukumuoa yeye mama mtoto wako wa chuo?
 
Hiki kitu mara nyingi kinaniumiza sana , maana naona kama nimemuaribia maisha binti wa watu.
Ni kweli uliharibu maisha ya huyo binti, hivi uliwahi kutubu na kuomuomba radhi huyo binti ?.....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…