HOJA Wanausalama wa Barabarani Mkata hizi tuhuma za rushwa mnazisawazishaje? Mnaonea sana madereva wa Lori

HOJA Wanausalama wa Barabarani Mkata hizi tuhuma za rushwa mnazisawazishaje? Mnaonea sana madereva wa Lori

Hoja ya Mdau inayopendekeza maboresho au mabadiliko ndani ya jamii, inayotakiwa kuangakiwa kwa mapana na Mamlaka husika
A

Anonymous

Guest
IMG_7390.jpeg
IMG_7387.jpeg
IMG_7391.jpeg
Kituo cha Police Mkata Kitengo cha Usalama Barabarani kumekuwa na ukiukwaji mkubwa wa maadili ya kazi yaani rushwa pale ni halali yao kabisa ndio sehemu wameona pakupatia hela ukio-overtake pale wanakuweka mahabusu wanakutoa wanakupeleka kwenye chumba chao kuna askari.

Katika hicho kituo wanakaaga mule na mama mmoja wanakuambia 'live' tunakufungia leseni ama utoe laki 4 fikiria dereva wa malori laki nne... ukishatoa wanarudi kaunta kule wanakuandikia umelipa fine ya Sh 30,000 ilihali umeshatoa hela na mbaya zaidi gari ndogo hawaangaiki nazo ama kwasababu sisi wa malori hatuja soma hatujui haki zetu?

DTO wa pale ameshalalamikiwa sana lakini hakuna hatua zozote zinachukuliwa mambo ni yaleyale kila wakati kuna dereva aliwapiga picha akiwa anaenda sheli kuwatolea rushwa yao.

Yule dereva akapost Tiktok walivyoona wakamtuma dereva mwenzao akaenda akamsimamia yule dereva akafuta video wakamrudishia na kile kiasi walichochukuwa kwa yule dereva lakini bado ama kuna mradi wanafaidika mpaka wakubwa.

Ndiyo hiyo risiti ni ya kuzugia ili ionekana uliandikiwa fine baada ya kutolewa mahabusu zao lakini hapo na hela umeshatoa hatukatai makosa yapo lakini kwanini wawafanye wa malory mtaji mbona hakuna wa v8 anakaa mahabusu.

Pale mahabusu mtu wa Lori huwekwa ila kuongeza dau akiambiwa kiasi fulani yeye sawa na kutishiwa mahakamani ama kufungiwa leseni.

Kama ni fine iandikwe dereva wa lori ukimuandikia elfu 30 tayari ni adhabu tosha kuchukuwa hela tena nyingi zaidi ya kipato chake unamfanya anaenda kuiba mafuta ya bosi.

Huwa wanatembea na gari binafsi Subaru nyeupe, nyeusi na Harrie ya silver mnaongozana nao wakifika sehemu ya overtake wanapunguza mwendo uwapite ukiwapita tu unakamatwa Mkata.
 
Nchi ngumu hii, sekta hizi zishakuwa za kinyonyaji sana.
 
Rushwa n CCM, police damu damu. Poleni Sana.
Kazi ni kipimo cha utu
 
Back
Top Bottom