Wanavyofanya Musukuma na Polepole ni ushahidi wa ukomavu wa Rais Samia kisiasa

Wanavyofanya Musukuma na Polepole ni ushahidi wa ukomavu wa Rais Samia kisiasa

Polepole na Musukuma ni watu wanaopingana na Rais Mama Samia kwenye kila kitu. Wanabweka kwenye mitandao kupinga maamuzi ya Rais.

Walipinga chanjoweeeeee lakini mwishowe nadhani na wawo walichanja kimyakimya.

Sasa hivi wanapinga uwamuzi wa mama Samia wa kuisafisha miji, eti miji isisafishwe eti kuwatetea wavamizi na wachafuzi wa maeneo wasiondolewe mitaani.

Kwenye awamu ya Tano hawakuwa hivyo hata kidogo, kule barabara ya ubungo kimara maelelfu ya watu wakiwemo wamachinga waliondolewa kinyama kabisa kupisha upanuzi wa barabara tena walivunjia hata kule ambako barabara haitafika lakini Polepole na Musukuma hawakunyanyua midomo Yao hata millimeter moja kupinga na kutetea.

Leo hii eti miji isisafishwe ili watembea kwa miguu wawatunze wamachinga kwa kuwaachia njia zao za kukwepea magari kuepuka ajali. Kwa akili za Polepole na Musukuma wamachinga Wana haki kuliko watanzania waliozibiwa njia zao za kutembelea na kuchafuliwa mazingira yao.

Hizi ni Chuki za wazi ambazo ni kiongozi mkomavu TU ndiye anaeweza kuzivumilia.

Wamachinga ni sehemu ya jamii yetu, hawako pale kwa msingi ya dini, kabila Wala mkoa. Ni WA dini zote, makabila yote na kutoka mikoa yote ya bara na visiwani, hakuna mwenye Chuki nao binafsi, lakini huwezi kuchukua haki za watanzania wengine ukawapa wamachinga eti kwakuwa wanatafuta riziki. Lazima tuanzie pahala katika kutatua kero za makundi yote bila upendeleo.

Polepole na Musukuma hawatoi njia mbadala ya kuhakikisha usalama wa watembea kwa miguu, mitaro iliyozibwa, vibanda vya wamachinga wanamokimbilia vibaka kukwepa kukamatwa wanapowaibia watanzania wenzao au maji yanaotuama na kufurika nyakati za mvua kwa njia za maji kuzibwa.

Hizi ni siasa uchwara kabisa, Maana haki yako lazima ikomee pale inapoanza haki ya mwenzio. Kwanini haki ya mmachinga isikomee pale haki ya mtembea kwa miguu inapoanzia?

Heshima ni kujiheshimu, Mama Samia kaletwa na Mungu kwetu hakupiga kampeni ya kuwa Rais, kila mtu analifahamu hilo, tumheshimu, wacha atengeneze pale wenzake waliposhindwa. Mama Samia ni mwanamke, na tabia ya akinamama ni usafi, Wacha asafishe maana hakuna sheria yoyote anayokiuka kwa kuwaondoa, huwezi kuendesha nchi kwakutumia moyo badala ya akili/ubongo.

Rais Samia atapigiwa kura za kishindo na wale watanzania ambao:
1. Wanaopenda utaratibu kwenye kila jambo.
2. Wanaopenda uhuru wa kutoa mawazo bila kubugudhiwa.
3. Wanaoamini kwenye haki za binadamu bila kujali jinsia yake.
4 wanaopenda usafi na miji safi
5. Unaopenda utawala wa sheria.
6. Wanaopenda kuona mihili yote inafanyakazi kazi zake bila kuingiliwa.
Ongeza bidii ya post zako, infact SAHAU, labda za kabari

2024 tutaona kama Mungu akituweka hai, hawa wanaodharilika Leo nawaza wanaweza kuja pigiwa magoti wawasamehe watu
 
Hahahaha yote uliyotaja 1-6,hakuna linalogusa moja kwa moja wapiga kura ambao ndo huamua Nani apite.

Hizi ni hoja za ujuajijuaji wa JF.

Kama chanjo siyo issue mbona Watanzania wameigomea?
Kama wamachinga siyo issue subiri 2025.
Bahati mbaya tu hakuna watu smart upande mwingine lakini kwa huu mwendo ndio awepo Dr. Slaa, asubuhi mapema
 
Samia hapo alipofika hata asipochaguliwa tena hataacha kumshukuru MwenyeziMungu, Kuna watu wanaomba wawe Marais japo kwa wiki moja tu na haiwezekani. Mama asiache kufanyakazi mzuri eti kwasababu ya 2025.

CCM sio wapiga kura wanaosababisha mtu achaguliwe, ukiwaza hivyo umejidanganya. Wacha tuisuke vizuri safu ya uongozi ndani ya chama chetu. Mbona wasiokuwa na vyeti, watumishi hewa, na wasioongezwa mishahara walitishiaga hayohayo ya kupiga kura, kwani hukuona kilichotokea?

Wamachinga hawana muda wa kupiga kura na kulinda wewe tusidanganyane.
Kwa Mungu sio kwa mganga.
 
Na kama unaweza mshauri mama basi mwambie aishi hivyo, kama ni urais -tayari ameshaupata.
Na kingine alifanyie kazi suala la kujenga taasisi imara.
 
Ongeza bidii ya post zako, infact SAHAU, labda za kabari

2024 tutaona kama Mungu akituweka hai, hawa wanaodharilika Leo nawaza wanaweza kuja pigiwa magoti wawasamehe watu
Hivi kwa akili zako timamu, ni watanzania wangapi wenye afadhali ya maisha miaka 60 ya uhuru? mbona watu wanachaguliwa tu miaka yote? Hebu kwenda zako huko, msimtishe mama.

Watanzania hawakuwa na maji, umeme, elimu bora, mishahara mikubwa, hospital, nyumba bora, pembejeo za kilimo, na hata masoko ya bidhaa zao za makondeni. Mbona hiyena hiyena ni kila mwaka? Msimtishe mama hata kidogo, hata yeye sio mgeni nchi hii.
 
Samia ataangukia pua Wala asihangaikie urais. Makundi yafuatayo yatamkwamisha...
1. Wasiopenda tozo. Hapa ni watanzania wote.
2. Wasiopenda ukandamizaji.
Haya ni maneno tu mkuu.

Yamekuwepo miaka na miaka
 
Hahahaha yote uliyotaja 1-6,hakuna linalogusa moja kwa moja wapiga kura ambao ndo huamua Nani apite.

Hizi ni hoja za ujuajijuaji wa JF.

Kama chanjo siyo issue mbona Watanzania wameigomea?
Kama wamachinga siyo issue subiri 2025.
Juzi nilipanda bodaboda kwa umbali mrefu nikawa nazungumza na muendesha bodaboda. Aiseee watu wanamsapoti sana mama

Usiskie ya kuambiwa
 
Samia hapo alipofika hata asipochaguliwa tena hataacha kumshukuru MwenyeziMungu, Kuna watu wanaomba wawe Marais japo kwa wiki moja tu na haiwezekani. Mama asiache kufanyakazi mzuri eti kwasababu ya 2025.

CCM sio wapiga kura wanaosababisha mtu achaguliwe, ukiwaza hivyo umejidanganya. Wacha tuisuke vizuri safu ya uongozi ndani ya chama chetu. Mbona wasiokuwa na vyeti, watumishi hewa, na wasioongezwa mishahara walitishiaga hayohayo ya kupiga kura, kwani hukuona kilichotokea?

Wamachinga hawana muda wa kupiga kura na kulinda wewe tusidanganyane.
Watu wasiojua mambo wanadhani mtu unaweza tu kuwa Rais wa nchi.

Wanadanganyana eti ni haki yako kuchagua na kuchaguliwa.
 
Walipinga chanjoweeeeee lakini mwishowe nadhani na wawo walichanja kimyakimya.
Mkuu wapo watatu wanaomkwamisha Rais, ongezea na Mzee Gwajiboy . Yes inasemekana wamechanja kimya kimya tena ile Johnson and Johnson vaccine wakaiwahi kabla haijaisha sababu yenyewe unachanja mara moja tu.
 
Juzi nilipanda bodaboda kwa umbali mrefu nikawa nazungumza na muendesha bodaboda. Aiseee watu wanamsapoti sana mama

Usiskie ya kuambiwa
Labda kwenye nchi ya kusadikika ambako,Bei ya sabuni,mafuta ya kula,mabando,bati,simenti zimeshuka Bei.
Bila kusahau machinga ambao wamegeuka mtaji wa kusaka vyeo zaidi.

Tofauti na hapo nafikiri ulibebwa na jini lililojigeuza bodaboda.
 
Hivi ulikuwepo wakati wa kodi ya kichwa mkuu? Au kodi ya kipande cha baiskeli? Tozo ya miamala ni njia nzuri ya kumfanyia kila mmoja alipe kodi bila kutumia njia za kibabe kama za kodi ya kichwa na kodi ya kipande. Watanzania hamjazoea civilization.
Watanzania ni watu wagumu sana kuwaongoza.

Hivi ninavyokwambia nipo nchi flan hapa hapa Africa najionea namna watu wanavyochajiwa kodi huku.

Jana tulikwenda kubadili fedha za kigeni tupate fedha za hapa na tukajifunza zaidi na zaidi why rais Magufuli aliamua bureau de change azipige pini.

Watanzania wengi hawana exposure na hawajui mambo yanavyoendeshwa.

Tanzania ni nchi Bora kabisa na nafuu kuishi
 
Chanjo 1m, Watanzania 60m,zimegoma kuisha mpaka zimeshaexpire tu,imebidi walete za mchina nazo doro tu.
Hiii ndo TZ ya JPM,ukijitenga naye utaangukia pua.
Wajinga wa marehemu bwana kafa katuachia Wafuasi wake wajinga
 
Bahati mbaya tu hakuna watu smart upande mwingine lakini kwa huu mwendo ndio awepo Dr. Slaa, asubuhi mapema
Kwa kuwa Dr. Slaa ni mtu smart, aliona na kujiridhisha kwamba njia pekee ya kuipeleka Tanzania mbele ni kupitia utawala wa Chama cha mapinduzi (CCM).

Yes chama kina changamoto zake lakini for the next 10p years to come, CCM is the only and best party to take this country further economically, socially and Politically.
 
Back
Top Bottom