Wanawake ambao hatujajaliwa kuzaa licha ya kuwa na wanaume tukutane tufarijiane

Wanawake ambao hatujajaliwa kuzaa licha ya kuwa na wanaume tukutane tufarijiane

Masikini Ndege Tausi hana tu mtoto ila ni mrembo sana!
10e7a62a20fc1cbb7e9b693c88561e0eb9eea585.jpeg
 
Mada inahusu wanawake ila cha ajabu wanajibu wanaume kwa mihemko na chuki swala la mtoto Mungu ndiye apangae na kutoa mimba sio sababu mwanamke kutopata mtoto.
Sasa sisi si ndio sababu ya nyinyi kupata watoto ? Au kuna mwanamke bila mwanaume na mwanaume bila mwanamke katika suala la uzazi ?
 
Oohh kumbe mnalijua hilo ?? Sasa mbona linapotokea tatizo kwenye uzazi wanaume huwa mnawabebesha lawama wanawake ??
Sasa sisi si ndio sababu ya nyinyi kupata watoto ? Au kuna mwanamke bila mwanaume na mwanaume bila mwanamke katika suala la uzazi ?
 
Dada yangu ameolewa kwa zaidi ya miaka 15 na alibeba mimba moja tu ndani ya miezi saba akajifungua mtoto njiti akafariki. Aiseee stress za mwanamke anaetafuta mtoto omba sana Mungu zisikupate, kaenda kila hospital aliyotajiwa inasaidia, makanisa, dawa za kienyeji lakini wapi. Machozi na stori za kukata tamaa kila utakapokutana nae hofu ikiwa kama mume wake ana mtoto pembeni na hajawahi kumwambia. Mwaka jana mtu akamwambia aende KSMC kujaribu na akaapa hii ndio mara ya mwisho kwake kuhangaika. Mungu si athumani after miezi ya kunywa dawa sasa hivi ni MJAMZITO, Mungu anakupa kwa wakati wake hawai wala hachelewi, msichoke msikate tamaa.
 
Kuna watu wanatoa mimba usiku na mchana na bado Kinga wanatumia Sana ila akikaa vibaya mimba hiyo usiishi kwa kukariri.
acha kujifariji, kachome sindano kwa miaka miwili alafu uje ulete mrejesho kama ikishika haizidi miezi mitatu itaharibika au ndiyo hizo unazosemea.
 
Back
Top Bottom