Wanawake kwa hizi akili, Mna haki ya kupigwa matukio

Naunga mkono hoja
 
Kajua kuwapanikisha. Wanaume milio kila kona, nyuzi kila wakati🀣🀣🀣
Mimi ni moja ya hao wanaume aliowapanikisha aisee. She's an idiot. Ni type ya wale wanawake wanashindana na trauma zao ila wao wanaamini wanashindana na mwanaume. Ni asilimia ngapi ya wanaume wanawazuia wake zao wasijiendeleze au wasiwe na careers zao? Ni wachache sana. As a matter of fact wanaume majority wana support wazo la mwanamke kujishughulisha. Aache propaganda zake za ki feminist mara moja. Anachangia kutuharibia jamii.
 
Wacha bwana!!!
 
Tunapoelekea wanawake walio tayari na majukumu ya kumtunza mume watakuwa wachache sana.
 
Hilo bao lako litakalolelewa na mwanamke mwenye mentality hiyo umeshajiuliza litakuja kuwa nani ktk maisha yake?maana kutia mimba na kumkacha siyo kazi kazi ni mama wa aina hii amlee mwanao uje kweli kumwita mwanao itawezekana?
 
Hatimaye Rose kanisemea upuuzi nisioufagilia wa kufua viboksa na kuacha kutafuta pesa..!!

Wanaume sijui mtamuendesha mwanamke gani karne hii 😹

Kila siku mnakula za uso 😹
Hakuna mwanaume mwenye akili timamu anaoa mwanamke ili amuendeshe/amnyanyase. Yaani ni hayupo duniani kote. Vita yenu ni vita dhidi ya mila na desturi, siyo dhidi ya mwanaume. Msichokitambua ni kwamba mwanaume mwenyewe naye ni mhanga wa hizo mila na desturi.
 
She is not an idiot, you are
 
I gave reasons for calling her a moron. And, yes, she's an idiot. Give me your reasons for thinking that the opposite is true. Leta hoja bibie.
Kwanza aliposema kufua boxer hakumaanisha kufua boxer literally, aliweka kufua boxer kama kiwakilishi tu cha majukumu ya mke yeyote (msomi na ngumbaru). Ila kwa mtu aliyesoma hatakiwi tu kuishia hapo, elimu yake inatakiwa ilete matokeo chanya kwake binafsi na jamii inayomzunguka, akiridhika tu kuitwa Mrs Strategist ni hasara kwa taifa na wale waliowekeza kwenye elimu yake maana kama ni suala la kuwa mke wa mtu hakuhitaji mamilioni ya ada. Huwa unaona hata humu Jf wasomi wanavyobezwa kwa kufanya kazi za uchuuzi ambazo hata asiyejua kusoma anafanya hizohizo.
Point nyingine aliyoingelea ni kuwa mwanamke unatakiwa ujenge jina lako wewe binafsi, kuwa Mrs fulani is good lakini mimi kama Khantwe ni nani? Ikitokea huyu niliyenaye hayupo tena kwenye maisha yangu au hayupo duniani kwa ujumla nilazimike kutafuta mwingine ili anipe identity? Mnataka kusema ameongea kitu kigeni sana? Tunawaona wabunge, mawaziri, wataalamu mbalimbali wanawake, wangekuwepo kama wangekuwa wameamua kukalia degree zao wakakaa jikoni kupikia waume zao?
 
Sasa mbona unaongea kitu kilekile nimeongea, best? Nimesema ni wanaume wachache sana wanawakataza wake zao kujishughulisha. Tena siku hizi wanaume mpaka wanaitwa siju "mario" kwasababu ya ku prefer wanawake wanaoweza kuchangia gharama za maisha ya familia. Huyo sijui mnamwita "Rose" kwenye hii video yeye mwenyewe anakiri kwamba kasomeshwa na mwanaume (Mzee Mushi/Baba yake). Wale 'mama ntilie" unawaona mjini wengi wameolewa na wanaungwa mkono na waume zao kujitafutia kipato. Mabinti wa kike wengi wasomi wanakiri kwamba baba zao wamewasomesha. Sasa ni nini misingi wa tuhuma kwamba sisi tunawaoa ili mkae nyumbani tu kuhudumia sisi na mabinti zenu, ambao pia ni mabinti zetu na tunawatunza na kuwasomesha ili wajitegemee huko mbeleni?
 
Sasa hebu niambie kosa la Rose ni lipi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…