Wanawake kwa hizi akili, Mna haki ya kupigwa matukio

Wanawake kwa hizi akili, Mna haki ya kupigwa matukio

Wako sawa, unajua haya mataratibu wanaume tuliyaweka kidikteta sana na hawa watu hawakuwahi kuyakubali ila walilazimishwa kukubali.

Leo mwanamke amepewa fursa za elimu, biashara na uongozi, kwa lugha rahisi umemsogeza karibu napesa. Unapomzuia haushindani tena na mwanamke ila unashindana na uwezo wa elimu au exposure iliyoko ndani yake.

Wanaume tumelishwa mentality ya kuwa control hawa viumbe ila tunakoelekea haiwezekani, tuanze kujifunza kuishi na mwanamke mwenye elimu na mwanamke ambae anao uwezo ndani yake wa kutafuta pesa.

Ukimtafuta mwanamke wa zamani aliyekuwa kifungoni, hana maamuzi kwenye familia, anafata chochote anachoambiwa kwa mwanamke wa sasa mwenye elimu hutampata.

Wanaume tulijiachia sana na kudanganyana sana ila tukubari wanawake kujengewa uwezo hii ni challenge tunayopaswa kuikubali sio kuanza kupigana vita isiyo na maana.

Wewe unasomesha mtoto wakike Ile iweje? Unataka asome akaishie tu kuwa mama wa nyumbani anapika na kumfulia mmewake? Hiyo investment unayoweka kwa mtoto wako wa kike inastahili tu kwenda kukaa ndani bila kujishughulisha?

Mwanamke aolewe ila Uwezo anaopewa haupaswi kukaa tu ndani, ukatumike kwa manufaa ya familia yake na Taifa
Sahihi kbsa
 
Hatimaye Rose kanisemea upuuzi nisioufagilia wa kufua viboksa na kuacha kutafuta pesa..!!

Wanaume sijui mtamuendesha mwanamke gani karne hii 😹

Kila siku mnakula za uso 😹
Kwani kuoa lazima

Hebu kila mtu ashinde mechi zake tuone nani bingwa.
 
Kwenye haya maswala ya kijamii na kifamilia, hamna vita yoyote ile atakayo ianzisha mwanamke akamshinda mwanaume hamna kwani mara zote wao ndio uhumia. Halafu wanaume vita zetu tunapigana kimya kimya tena bila kuongea ongea ila output utaiona na huwaga tunaongea mara chache baada ya hapo ni kimya na kuendelea na mambo yetu.

Hivi tunavyo vidiscuss si vipya ukitizama jamii za ulaya (hapo ndio ujue duniani kote wanaume tunafanana),walianzisha haya mashindano matokeo yake talaka zimekuwa nyingi na wanao initiate ni wanawake na wanaume hawa wakatalii, ila baadae wao wanakuja kujuta. Wanaume wa ulaya wanawakimbia wanawake wanaenda kuoa Asia na Afrika wanawake wa kawaida ambao wanyenyekevu na wana heshima,japo huwakejeli kwa Kuwaiti passport bros ila wao wanatafuta amani ndani ya nyumba. Matokeo yake makwao rate ya ndoa imedrop, wale wanawake waliokuwa na misimamo ya kifeminist, leo ndio wanaongoza kutafuta wanaume kwenye single event na mara nyingi single events kwa nchi za Ulaya asilimia zaidi ya themanini wanao hudhuria ni wanawake.

Ila ninacho shangaa huyo mchungaji ,hajui hata huu ukristo umejengwa kwenye misingi ya familia na ndoa,misingi ya mmoja kunyenyekea, tena anaye nyenyekea alikuwa ni chaguo la Mungu (Maria na Yosefu). Ubaya anatumia madhabau kuishambulia misingi ya ndoa. Ndio maana huwaga nawaona Catholic wapo sawa kabisa, kila wanacho kiongea na kuhubiri huwaga Kina miongozo, hata kama akireference vitabu vingine, havimtoi nje ya miongozo ya kanisa,wamefanya hivi sababu wanajua siku padri anaweza akawa na mood mbaya au mtu kamtibua basi siku hiyo mood yake ndio itakayo muongoza.

Tatizo walokole wao hawana miongozo anahubiri kutokana na mood na anavyo jisikia kwa siku hiyo, mtu akimtibua matokeo yake ndio haya.Yeye anamsuguano na mme wake basi hapo anahubiri akiwa na maumivu ambayo yamemfanya mpaka aende kinyume kabisa na imani yake. Ila hao wasomi na wenye hela tunawaona wanavyo badilisha badilisha na kuwalea marioo na siku hizi kuna mtindo unakuja kwa kasi kwani hao vijana/marioo huwa rekodi wakati wakiwa faragha baadae wanawablackmail na kuwapiga hela.
 
Back
Top Bottom