Wanawake mnaojenga nyumba kwa siri bila mwenza kujua huwa mnamaanisha nini?

Ukweli mchungu ni kuwa Mwanaume anapaswa kuwa na hela kumzidi mwanamke wakati wote
Sasa akiwa Nazo hizo kidogo ndio atajenga Kwa Siri Kwa hizo ndogo bila mwenza wake kujua!!?

Labda kama unamaanisha wasiwe na Hela kabisa hapo sawa!!
 
Ukweli mchungu ni kuwa Mwanaume anapaswa kuwa na hela kumzidi mwanamke wakati wote
Dunia imebadilika sana mkuu,tunazaa watoto wa kike na wanasoma na wanapata nafasi kubwa tu serikalini au wanakojiajiri na kuajiriwa,wengine wanaingia kwenye mihangaiko ya maisha na wanafanikiwa sana kuliko hata wanaume.Sijui hali ikoje kwa zile nchi ambazo wanawake hawaruhusiwi hata kufanya kazi wanakaa tu nyumbani.Kifupi ndoa sasa hivi kwa wanaume ni mwiba...
 
Kama hao watoto tayari Wana kwao wameshajengewa ndio ajenge kisiri siri!!?Ina maana Kuna mwanamme Dunia hii atafukuza mama na watoto kwenye nyumba halafu akae na mchepuko!!?

Hebu eleza hili!
 
Kama hao watoto tayari Wana kwao wameshajengewa ndio ajenge kisiri siri!!?Ina maana Kuna mwanamme Dunia hii atafukuza mama na watoto kwenye nyumba halafu akae na mchepuko!!?

Hebu eleza hili!
😳😳😳😳
Uko serious au unatetea tu hoja yako.

Ni kweli hujawahi kuona mama na watoto waliofukuzwa na mwanaume nyumbani?
 
Ni kwa maisha ya zamani. Maisha ya sasa haya kwanza wanaume wengi hawafanyi majukumu yao ipasavyo na mwanamke akiwa hana kipato ndio kabisaa wanapata sababu ya kumkamdamiza. Wacha tu mwanamke awe na hela yake kuhusu kukaa vyema na mumewe itategemea utashi wake na aina ya mume alienae na kumbuka pia wanaume sio malaika na nyie na mapungufu yenu.
Mkuu ndio maana mwanamke alipaswa kukaa nyumbani azae na kulea watoto. Kwa sababu tunakiuka sheria za mungu ndio maana haya yanatokea.
 
Mkuu ndio maana mwanamke alipaswa kukaa nyumbani azae na kulea watoto. Kwa sababu tunakiuka sheria za mungu ndio maana haya yanatokea.
Matalibana walizingatia hili ndio maana wao migohoro ya ndoa husikii kabisa
 
Majukumu gani hayo hatutimizi
 
Kama akili zenyewe ndio hizi acheni tu vijana wa siku hizi wawe wagumu kuoa.Sasa mtu yupo kwenye ndoa anatelekeza vipi mtoto? Ila cha ajabu siku wakija kuachana zinagawanywa na mwanaume ila mali a mwanamke haziguswi,halafu kesho mnalamika mnataka 50/50 ,haki sawa ila vya kwenu hamtaki usawa.

Kama bado unaroho ya UBINAFSI ndoa haikufai achana nayo, endelea kukaa mwenyewe ujenge nyimba zako ,ufungue biashara zako uendelea na maisha yako binafsi.
 
Wanajiahami siku mkiachana vitu vyake visiwekwe kwenye mgao.

Jirani yetu anajenga tokea muda ila nyumba bado haijaisha huku mkewe tayari amejenga na nyumba imeisha kaweka wapangaji.
Mume hajui ila majirani tunajua.
Na siku zote mtu anapotembea MTAANI anakuwa yupo uchi maana mambo mengi yake hajui ila watu wanayajua🤔
 
😳😳😳😳
Uko serious au unatetea tu hoja yako.

Ni kweli hujawahi kuona mama na watoto waliofukuzwa na mwanaume nyumbani?
Mimi mama yangu kajenga mikoa tofauti na hadi mshua anaenda kaburini hajui lolote. Wakati wa uhai wake kampiga sana matukio hataki afanye kazi na hataki awe na maendeleo yoyote eti mke wa mtu na alimkuta kasoma na ana kazi tayari. Mtu hawazi ya mbele na ukoo wake ni ule wanaamini cha ndugu yoyote ni cha ukoo mzima. Akaona isiwe kesi katafuta mahala pengine kimya kimya. Na mzee alipofariki tu fujo zikaanza haya niambie kama hakua kajiongeza mapema hali ingekuaje.
 
Were ni Me au Ke tabia ya ubinafsi
 
Unafikiri wanaume wote wapo kama mzee wako?.

Kiasili mwanamke ni MBINAFSI,hela yake ni chungu haijawahi kuwa tamu.Hela yake inamatusi na masimango.Yaani nyinyi sio watoaji hata mkiwa nazo na mkitoa hata senti moja kuna siku utaitumia kumkejeli au kumsimanga mmeo kupitia hiyo senti moja.

Halafu unakuta nyie mnajenga kwa siri na tena inawezekana akawa ana mali nyingi, ila siku ya kuachana zinagawanywa za mwanaume.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…